Kampuni za madini na mafuta zina maslahi gani kwa bajeti yetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni za madini na mafuta zina maslahi gani kwa bajeti yetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mudavadi, Jul 21, 2011.

 1. m

  mudavadi Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati taifa likiendelea kutokomea gizani kila uchao, na wakati shauku ya kusubiri kuona au kusikia hatma ya Jairo na Ngeleja ikiendelea, ziko habari za uhakika kwamba makampuni ya madini na yale yanayojishughulisha na uuzaji, usambazaji na utafiti wa mafuta nchini yalituma viongozi wao waandamizi kwenda Dodoma kufanya lobbying ili kuhakiksha kwamba bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini inapitishwa na wabunge. Inaarifiwa pia kwamba katika mchakato huo, mamilioni ya shilingi yalitumika katika kujaribu kuwaweka sawa wabunge na wadau wa bajeti hiyo na hadi sasa hivi baadhi ya wawakilishi wa makampuni hayo bado wako Dodoma wakiendelea kutoa kile kinachoitwa usaidizi katika kujibu hoja mbalimbali na kuikarabati bajeti hiyo kabla haijawasilishwa tena.

  Mwenendo huu wa kushangaza na usio wa kawaida umezua maswali mengi, lakini lililo dhahiri ni je, makampuni haya yana maslahi gani katika bajeti yetu hata waingie gharama ya muda na rasilimali katika kuhakikisha kwamba wabunge wanaipitisha bajeti hii? Kama kweli ina maslahi kwa watanzania, ni kwa nini kutumike nguvu ya ziada kuipitisha? Tukijua kwamba bajeti ni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara husika, makampuni binafsi yanawezaje kuingilia mchakato huu wakati kupitishwa kwake hakuna faida au madhara ya moja kwa moja kwao kwa vile utekelezaji wa shughuli zao unategemea na kuzingatia sera, na sheria mbalimbali zilizopo nchini? Fedha wanazotumia leo, zitalipwa na nani na kwa njia ipi?
   
 2. T

  Tiote Senior Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nchi hii napata shida kuielewa. Hawa jamaa (Ngeleja na Jairo) walitakiwa kuwa wameondoka toka juzi lakini nashangaa bado wanadunda na tayari wameanza kueneza taarifa kwamba Waziri Mkuu amepotoshwa na kwamba hizo ni chuki tu za january Makamba na wenzake.
   
 3. w

  watenda Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya makampuni ndiyo ambayo yamekuwa yakiwapa rushwa hawa mabwana wawili na haishangazi sasa kusikia kwamba wana maghorofa ya kumwaga hapa mjini na hata kufikia hatua ya kuhonga wanawake majumba yenye swimming pool na gari za rav 4.
   
Loading...