Kampuni za Blandina Nyoni zinavyofanya ufisadi serikalini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni za Blandina Nyoni zinavyofanya ufisadi serikalini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by autopilot, Jan 31, 2012.

 1. a

  autopilot Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Sasa wakuu wa JF tunasema kuwa WE SPEAK OPENLY sasa naomba thread iachwe hapa tukate zote bila kuogopa kitu

  Huyu mama ndiye aliyehusika na kuileta ile software ya ASYCUDA Tanzania ambako alichukua fungu kubwa sana za kamisheni toka serikalini

  Lakini pia msisahu kuwa ana kampuni ya Catering ambayo kila wizara anayohamia au kila warsha anayokwenda lazima kampuni hiyo ipewe tenda ya kulisha chakula

  Lakini msisahau kuwa duka la nguo la Mariedo ni lake.... duka ambalo hata mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) alitoa ripoti kulishutumu kwa kugawa staff uniform zilizo na ubora hafifu kwenye wizara na idara mbali mbali za serikali pamoja na fenicha za ofisi ya spika kwa bei za juu kuliko uhalisi wa bei........... sasa hapa kidogo kulitokea matatizo........ Ludovick Utoh (ambaye PASCO huja kumtetea humu) sijui hakujua kama lile duka la Mariedo ni la Nyoni au la mpaka ripoti ikatolewa kwenye public jambo ambalo ni aibu sana kwa mama Nyoni

  Tazameni track record ya huyu mama kila wizara aliyopita na procurements za kwenye idara za hizo wizara utaweza kuona connection ya ufisadi wake.

  Kwenye public anakuwa mkali kwenye matumizi ya fedha lakini ukweli ni kuwa alikuwa anataka yake pekee yaende

  Lakini kwa kumalizia tuu ni kuwa anatokea Iringa kwenye kijiji kimoja na aliyekuwa katibu mkuu kiongozi Ikulu bwana PHILEMON LUHANJO.......
   
 2. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  naona biashara anazifahamu vyema kuliko kazi za serikali
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kumbe ni mteule wa Luhanjo ndo maana ana kibri ya kuongea vile!

  Yana mwisho hayo!
   
 4. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Lete habari
   
 5. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo zile suti feki za anazo vaa jerry slaa zinatoka kwa huyu mama?? aixee
   
 6. a

  autopilot Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lakini pia tusisahu kuwa:

  Idara za procurements katika irada za wizara zote anazopita blandina huwa anakuwa influence ya ajabu

  Mfano wizara ya Afya, wizara ambayo inatakiwa na matumizi makini ya fedha lakini huyu mama hakuona taabu kupitisha bajeti ya ya zaidi ya bilioni 6 kwa ajili ya maonyesho ya 77 na 88

  Mfano mdogo mmoja ni STAFF UNIFORMS ambazo mama Nyoni alilazimisha wizra ya afya kuwanunulia washiriki wapatao 1,000 suti jozi 6,ambazo thamani yake ni BILIONI 3..................!

  GUESS WHO SUPPLIES HIZO NGUO?

  Yap you guessed it.......ni lile dula la MARIEDO BOUTIQUE ambao wao wanachokifanya ni kununua nguo kutoka China lakini wanaandika lebo za UK.

  Jiulizeni kwa nini Mariedo hawakuwahi ku supply suti BENKI KUUU enzi za LIUMBA?


  Sasa kumbukeni kuwa hizo BILIONI 3 zingenunua vitanda vingapi kwenye hospitali za wilaya ngapi Tanzania?

  jibu ni rahisi.....tungeweza kununua vitanda 3,000 kwa bei ya shilingi 1,000 kwa kila kitanda! shemeji,wifi,wake ,mama,shangazi zetu wasingekuwa wanajifungulia chini sakafuni kama ilivyo sana lakini Blandina hayo yooote kwake sio muhimu...muhim MARIEDO wapewe tenda za staff Uniforms!

  btw

  I just wanna point out kuwa duka la huyu mama la Mariedo pamoja na kusupply vitu FEKI lakini pia tazameni mikataba yake ni endelevu kwenye kila idara ya serikali so unakuta Mariedo lina contract ya miaka mpaka 3 hata kama wanaleta bidhaa ambazo ni hafifu!

  Now Mzee Luhanjo hayupo tena na as it is MTOTO WA MKULIMA hawezi kuendelea kumlinda huyu mama....at some point itabidi ajiuzulu nyadhifa zote inluding kule WAMA ambako aliingizwa na PHILEMON LUHANJO.................!

  In short waingereza wanasema kuwa HER POSITION IS UNTENABLE
   
 7. a

  autopilot Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe kweli unajua ku connect the dots JF style
   
 8. a

  autopilot Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Luhanjo wanatoka kijiji kimoja lakini mhimili wake mkuu ni MTOTO WA MKULIMA

  sasa hivi news toka ndani ni kuwa hata mtoto wa Mkulima anafurahi JF inamfanyia kazi maana kumwambia aachie ngazi haiwezekani kwa sasa so its an open season kwa mama
   
 9. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  hawa kiama chao kiko njiani siku kikinuka tunapumzikia kwao
   
 10. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  lile duka liko pale benjamini mkapa towers ndugu zangu mbona napata giza nchi hii tunaenda wapi?
   
 11. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kupeana vyeo kindugu kutaipeleka nchi ya tanzania kubaya kwani hii inasababisha watumishi wengi umma kushindwa kuwajibika ipasavyo.
   
 12. a

  autopilot Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sawa sawa na nyuma ya lile Jengo ana kafungua SAUNA na duka la vipodoziNgoja nikuonyeshe duka lake liko wapi nipe 5 minute nikuwekee picha
   

  Attached Files:

 13. W

  We know next JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wakati mwingine unakuwa na point, sijui akili zako zikoje wewe FF. Yaani upo kama kinyonga vile anavobadili rangi.
   
 14. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli japo umeomba thread iachwe lakini ina hadhi kabisa ya kufutwa!, unaongea kama vile umekamatwa ugoni. huleti hoja ikaeleweka wala huoneshi ukweli wa kile unachokisema. Kwa wale wanaomfaham Blandina Nyoni utendaji wake wa kazi ni Kiongozi makini sana na ni mwepesi wa kusikiliza na kutoa uamuzi haraka na sahihi. Najua ujio wake wizara ya afya ulitokana na kutokuelewana kati yake na huyo Ludovic utouh katika hoja za ukaguzi. pia najua kwamba baada ya kuingia aliziba mianya mingi sana ya wizi wa fedha kupitia kule msd, kwenye tafiti feki za maralia na katika miradi mingi feki iliyokua ikifanyika kabla.

  Sawa, huo unaweza kuwa ni mtamo wangu tu na jinsi nivyomfaham. Tuje katika hoja zako, Mama nyoni aliingiza mfumo wa ASYCUDA akiwa kama nani na alisababisha hasara au aliiba kiasi gani cha fedha?,

  utaratibu wa manunuzi ya umma ni kwamba tenda zinatangazwa na makampuni yanaomba, sasa kama mariedo wanapewa halafu wakileta bidhaa zinakaguliwa na kuthibitishwa ni sawa, mariedo wana kosa gani?, huoni kama ni chuku binafsi za Utouh kuishambulia Mariedo wakati anajua watendaji walionunua?

  Katika hoja ya tenda za chakula hujataja kampuni yake ni ipi na inafanya ufisadi gani. kwa ujumla naona we una chuki tu binafsi kwa sababu mama anafanya biashara zinenda vizuri na kazi zake pia au amegusa maslahi yako sehemu flani. Leta hoja tuijadili acha majungu.

  Mama nyoni alikua mhasibu mkuu wa serikali kabla luhanjo hajawa katibu kiongozi, amekua na nyadhifa nyingi tu kabla luhanjo hajawa hapo alipo, sasa kutoka nae kijiji kimoja ndio hoja gani?. Jadili mtu kutokana na anafanya nini sio anatoka wapi?

  Mwisho kama una ulilokua umelificha lilete hapa ili uzi wako uwe na maana, vinginevyo haya ni majungu tu!
   
 15. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Lakini huyu ni mwana CCM FF tokea lini CCMwakasema mambo hadharani ? Maana katiba inaongelea siri tu na si zaidi .
   
 16. W

  We know next JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  JF BRAVOO.......

  Autopilot na haya je??

  1. kuhamisha mashine ya kufanya scan toka muhimbili kupeleka hospitali binafsi ili apate chochote...

  2. Kununua AC za mamillioni na kizifunga ktk mabanda ya 88 Dodoma mwaka jana.. karibu million 70

  3. Kila mwezi anapata cheki ya Sh. Mil 10, toka Muhimbili National Hospital, fuatilieni muone yule Dr aliyehamishiwa mbeya kwa kukataa kutoa hizo pesa...

  4. Ongezeni na ninyi nyingine.......
   
 17. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Dakika tano imekua siku sheikhe vipi
   
 18. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,002
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Wa kwanza kuwagawana ni hao.
   
 19. a

  autopilot Member

  #19
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina mengi sana:  Katibu mkuu wa Wizara ya Afya lawamani (BLANDINA NYONI)

  • Atuhumiwa kusababisha hasara serikalini
  KATIBU Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni ametengua uteuzi wa Mwambata wa Afya katika ubalozi wa Tanzania nchini India katika mazingira ya kutatanisha, MwanaHALISI limeelezwa.

  Tarehe 6 Agosti 2008, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Wilson Mukama alimteua Daktari Msaidizi Mwandamizi katika wizara hiyo, Edward Sawe, kuwa Mwambata wa Afya nchini India.

  Taarifa zinasema uteuzi wake ulitenguliwa miezi minane baadaye kwa madai kuwa Dk. Sawe hakuwa na “sifa za kushika nafasi hiyo.”

  Tayari uamuzi wa Nyoni umeisababishia serikali hasara ya dola 25,000 (sawa na Sh. 30 milioni) zilizolipwa kwa ajili ya pango la nyumba mjini New Delhi ambako Dk. Sawe angeishi na familia yake. Nyumba hiyo ilipangwa tangu tarehe 1 Oktoba mwaka jana.

  Gazeti hili limepata taarifa kuwa tarehe 6 Januari 2009, Nyoni alimuandikia barua Dk. Sawe kumtaka aripoti Ofisi ya Damu Salama (National Blood Transfusion Services) wakati akisubiri kukamilika kwa mipango ya safari.

  Lakini miezi mitatu baadaye Nyoni alimwandikia Dk. Sawe na kumweleza kuwa hakuwa na sifa ya kushika wadhifa huo.

  Barua ya Nyoni kwa Dk. Sawe inasema, “…Baada ya kupitia wasifu wako, imeonekana kwamba haukidhi matakwa ya kuwa Mwambata wa Ubalozi kuhusu masuala ya Afya nchini India...Kwa msingi huo, tutakupangia kazi nyingine hivyo uripoti kwa katibu mkuu kwa kupangiwa kazi nyingine.”

  Akizungumza na MwanaHALISI wiki iliyopita, Nyoni alikiri kutengua uteuzi wa Sawe, lakini alisema hatua hiyo haikulenga kubeba mtu, bali kwa sababu “Serikali inataka kupeleka mtu mwenye sifa.”

  “Uteuzi wake umetenguliwa kwa mujibu wa kanuni za utumishi. Mimi kama mwajiri ndiye ninayepanga kazi. Hivyo ndivyo nilivyofanya kwa Sawe. Kule India, hatupeleki karani. Tunapeleka daktari bingwa ili kutimiza lengo lililokusudia,” alisema kwa sauti ya ukali.


  Nyoni alisema daktari anayehitajika ni yule atakayeweza “kujadiliana na madaktari wa India ili kujua wagonjwa tunaowapeleka wanahitaji huduma gani na kuhakikisha wanahudumiwa kutokana na magonjwa yanayowasumbua.”

  Alikuwa akijibu hoja kwa nini Dk. Sawe ambaye amekuwa katika kitengo cha kusafirisha wagonjwa wa Tanzania kwenda nchi za nje asiweze kuwa na sifa za kuwa mwambata wakati kazi hiyo haihusishi ubingwa katika tiba.

  Alipong’ang’anizwa kutoa maelezo zaidi kuhusu mashaka yake kwa Dk. Sawe, na kwa nini Mukama aliona anafaa au yeye alitaka kuweka “mtu wake,” Nyoni alisema “Naomba uje ofisini kwangu tuzungumze.”

  “Ninakuheshimu sana kwa sababu ya msimamo wako. Siwezi kuzungumzia mambo ya ajira katika simu. Nakuomba uje ofisini kwangu tuzungumze,” alisema kwa upole.

  Alisema, “Kaka yangu hapa kuna majungu mengi sana. Watu wa hapa hawataki mtu wa kuwasimamia. Kuna majungu kila kona hapa. Watu wananisakama. Nakuomba usiingie huko.”

  Alipoambiwa kwamba tayari kuna madai kuwa ameteua “mtu wake,” mwanamke aliyetajwa kwa jina la Dk. Chale na ambaye hana sifa ya kushika nafasi hiyo kwa kuwa si mtumishi wa serikali, mara hii Nyoni aling’aka akisema:

  “Hapana. Njoo hapa, nitakuonyesha CV zake. Ni mtumishi wa serikali. Huyu unayemtaja yupo Muhimbili (Hospitali ya taifa). Anafanya kazi pale kama daktari bingwa,” alisema.

  MwanaHALISI ilimuuliza Mukama kutaka kujua iwapo aliteua mwambata asiyekuwa na sifa, naye alisema, “Muulizeni mhusika. Mimi sipo huko tena.”

  Taarifa za ndani ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Hazina zinasema Sawe alishagharamiwa safari pamoja na familia yake kwenda India na kwamba alijulishwa usitishaji dakika za mwisho.

  Sawe alijulishwa mabadiliko baada ya kusubiri ruhusa ya Nyoni kwa muda mrefu kinyume na matarajio yake kwa kuwa mipango mingine ilikuwa imekamilika ikiwemo mkewe kupata likizo kazini kwake.

  Daktari mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe aliiambia MwanaHALISI kuwa kazi ya mwambata haihitaji daktari bingwa. “Hiyo itakuwa kupoteza mtaalamu anayehitajika zaidi nchini. Hapa anahitajika daktari wa kawaida anayemudu kutambua magonjwa mbalimbali,” amesema.

  Uzoefu unaonyesha kwamba madaktari wanaofuatana na wagonjwa waliotoka nchini huwa hawatibu isipokuwa kutoa maelekezo tu ya historia ya mgonjwa na kuratibu tiba yake itakavyokuwa inafanyika.

  Serikali imeamua kuteua daktari wa kushughulikia jukumu hilo nchini India kwa vile ndiko wagonjwa wengi wanakopelekwa baada ya tiba zao kushindikana kwenye hospitali za nchini.

  Tanzania inapeleka wagonjwa wengi wa maradhi mbalimbali kila mwaka nchini India.

  Uteuzi wa mwambata wa afya unafuatia ziara ya Makamu wa Rais, Mohammed Shein nchini India, Machi mwaka jana alipoagiza ubalozi uwe na ofisa wa kushuhgulia masuala ya afya (Medical Attache).

  Barua ya ubalozi wa Tanzania mjini New Delhi, Kumb. THC/ND/PF.186 ya tarehe 23 Oktoba 2008 iliyosainiwa na Yahya A. Mhata kwa niaba ya balozi inatoa mchanganuo wa gharama za pango la nyumba ya mwambata.

  Kwa mujibu wa barua hiyo, Rupia 80,000 ni pango kwa mwezi na kwa mwaka inakuwa Rupia 960,000, wakati gharama ya wakala wa nyumba ni Rupia 40,000. Jumla ni Rupia 1,000,000 (sawa na dola 25,000 wakati huo).

  Barua ya balozi ilikuwa ikijibu barua ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Kumb. AB 226/580/01/114.

  MwanaHALISI inayo mawasiliano yote kuhusiana na suala hili.
   
 20. MANI

  MANI Platinum Member

  #20
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Kwani hawajui mabaya na mazuri ila ni basi kubisha tu .
   
Loading...