Kampuni yazuiwa kuchota bilioni 54; Ni ya wafanyabiashara wanandugu 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni yazuiwa kuchota bilioni 54; Ni ya wafanyabiashara wanandugu 3

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 17, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  *Ni ya wafanyabiashara wanandugu 3
  *Kampuni ya MeTL, TIB zatia ngumu
  *Mambo ya Nje, Ubalozi wahusishwa

  Na Waandishi Wetu
  KAMPUNI ya Mohamed Enterprises (MeTL), kupitia Mahakama Kuu, imekwamisha malipo ya dola milioni 34 za Marekani (Sh bilioni 54.4) ambazo zilikuwa zichukuliwe na kampuni ya MEIS Industries katika mazingira yenye utata.

  Kampuni ya MEIS Industries inamilikiwa na wanandugu watatu ambao ni Islam Ally Saleh, Merey Ally Saleh na Saleh Ally Saleh.

  MEIS ilikuwa imeamriwa ichukue fedha hizo mali ya Serikali ya Libya, ilhali kukiwa na kesi ya msingi namba 110/2010 iliyofunguliwa na MeTL dhidi ya Serikali hiyo.

  Kumekuwapo msukumo mkubwa wa kisiasa na kidiplomasia wa kutaka MEIS ilipwe mabilioni hayo, ilhali ikiwa haina haki hiyo kisheria.

  Duru za kimahakama zinaonyesha kuwa MeTL walifungua kesi hiyo na kupeleka samansi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyo chini ya Waziri Bernard Membe, ili kupitia kwake, afikishiwe Balozi wa Libya nchini.

  Hata hivyo, Wizara ya Membe katika namna ya kushangaza ilipokea samansi hiyo, lakini ikakataa kuiwasilisha kwa Balozi wa Libya.

  Imebainika kuwa, wakati kesi ya MeTL ikiwa inaendelea siku chache badaye MEIS Industries ilifungua kesi namba 124/2010 dhidi ya Serikali ya Libya ikitaka ilipwe dola milioni 20 za Marekani na gharama za usumbufu za dola milioni 14.

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ilitoa ushirikiano kwa kuhakikisha samansi inapelekwa kwa Balozi wa Libya nchini, tofauti na ilivyokuwa imeikatalia kampuni ya MeTL inayowakilishwa na wakili wa kujitegemea, Dk. Masumbuko Lamwai.

  Kesi hiyo ilisikilizwa upande mmoja wa walalamikaji na hukumu ikatolewa na Mahakama Kuu kwa kuamuru Benki ya TIB iilipe MEIS dola milioni 34 za Marekani.

  Katika namna ya kustaajabisha, Balozi wa Libya hapa nchini akijua wazi kwamba kuna kesi katika Mahakama Kuu dhidi ya Serikali ya Libya, hakuweka wakili wa kuitetea Serikali, na matokeo yake ndiyo yaliyowezesha kesi isikilizwe upande mmoja na kutolewa hukumu.

  Duru za uchunguzi zimebaini kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilikuwa bega kwa bega na MEIS Industries pamoja na Balozi wa Libya nchini kuhakikisha kesi hiyo inaendeshwa na kufikia tamati kama ilivyotokea.

  MEIS Industries inamilikiwa na watu wanaotajwa kuwa na uhusiano wa karibu mno na baadhi ya maofisa waandamizi kabisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Imebainika kuwa TIB baada ya kuamriwa ilipe kiasi hicho cha fedha, ilikataa kulipa kwa maelezo kwamba haikuwa na ruksa ya kuzitoa.

  Kutokana na msuguano huo, MeTL walilazimika kuweka zuio mahakamani ili TIB wasiilipe MEIS Industries.

  Aidha, utata wa namna fedha hizo zinavyotaka kuchukuliwa umejitokeza pia kwenye mchakato wa kisheria ambapo wakili Joseph Thadayo ndiye mwanasheria wa MEIS, ndiye wakili wa Membe na amekuwa pia akilipwa na TIB kwa kazi za kisheria anazowafanyia.

  "Hapa kuna maswali mengi ya kuuliza juu ya uhusiano wa MEIS, Membe na Thadayo," kimesema chanzo chetu cha habari.

  Wakati baadhi ya vyombo vya habari vikiripoti kuwa MeTL inataka ilipwe fedha hizo kinyemela, imebainika kuwa MeTL ndiyo inayojitahidi kuzuia malipo hayo ambayo MEIS wanahaha kuhakikisha wanalipwa.

  Wakati Membe na Balozi wa Libya wakinukuliwa wakisema Massoud Mohamed Nasr, hatambuliki, MTANZANIA imefanikiwa kupata waraka unaoonyesha kuwa Nasr ndiye anayetambuliwa kwa nyaraka rasmi za Serikali ya Libya kukusanya madeni ambayo Serikali hiyo imekuwa ikiidai Serikali ya Tanzania tangu Februari 12, 1983.

  Uhalali wa Massoud upo hata kwenye nyaraka ambazo zipo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Nasr alishalipwa dola milioni nne za Marekani kama kamisheni kwa kazi hiyo, jambo ambalo Ubalozi wa Libya hapa nchini unalifahamu, na hivyo kuondoa dhana kwamba hatambuliki.

  Dk. Lamwai amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akimpa tahadhari juu ya kutowajibika kwake katika suala la kesi iliyofunguliwa na MeTL.

  Amemwandikia pia Balozi wa Libya juu ya uamuzi wake wa kutotaka kufanya mipango ya kuitetea Serikali yake katika kesi namba 124/2010.

  Katika kesi nyingine namba 110/2010 walalamikaji MeTL wamewasilisha mahakamani pingamizi dhidi ya wakili Kamara na kampuni ya The Crest Professional Attorneys kwamba hawana sifa ya kuiwakilisha MEIS Industries, kwa vile mwaka 2009 walitoa ushauri wa kisheria kwa suala hilo hilo lililo mahakamani. Shauri hilo halijatolewa uamuzi na Mahakama.

  Katika kesi namba 124/2010, MeTL pia imewasilisha pingamizi kama hilo kwa Kamara na kampuni hiyo na Jaji amemtaka Kamara asiwajibike kwa shauri kati ya MeTL na MEIS Industries.

  Katika hatua nyingine kampuni ya MeTL imelalamikia kitendo cha baadhi ya magazeti kumhusisha Mbunge wa Singida Mjini, Mohamed Dewji kwenye sakata hili.

  Ofisi ya Mwanasheria wa MeTL, imesema Mohamed si Mkurugenzi wala mwanahisa katika MeTL, bali mhusika ni Ghulam Dewji ambaye ni baba yake.

  "Mohamed kuwa na uhusiano na Ghulam kwa sababu ni baba yake haina maana kwamba ni Mkurugenzi au mwana hisa wa MeTL, tena habari zinazoandikwa zinamhusu Ghulam, lakini kwanini iwekwe picha ya Mohamed? Huu ni mpango wa kuchafuana.

  "Hatutaki suala hili liingiliwe kisiasa, kirafiki au kidiplomasia, Mahakama iachwe iwe huru kuamua, vyombo vya habari visitumiwe kupotosha ukweli," imesema taarifa ya mwanasheria wa MeTL.
   
 2. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  haya yote ni majambazi yako kazini..... yamezidiana akili....
   
 3. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  always nilikuwa nasubiri membe aanze haribu, anajifanya msafi sana, sasa maovu yanaanza toka moja moja.
   
 4. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  urais mwaka 2015 ndani ya CCM na serikali ya Kikwete utaanika yooooteeeeeeeeeeee! Biblia Takatifu katika kitabu cha Isaya inasema kila lililofichwa darini litawekwa peupe.
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Democracy, which is a charming form of government, full of variety and disorder, and dispensing a sort of equality to equals and unequals alike...
   
 6. n

  niweze JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwanini wanaharakisha kutoa maamuzi sasa hivi wakati vita vya Libya vikiisha wanajua wazi serikali mpya ya Libya will have all rights to Libyan assets all over the world? Kilichofanyika ni kwamba UN na mataifa mengi duniani wamepitisha uamuzi unaoitwa 'freezing of assets'

  Njaa za viongozi wa serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na ofisi ya balozi ya Libya wanaonekana kama kawaida yao ni njaa zimejaa. Future Libya government will sue for their assets.
   
 7. p

  profkobayashi JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 224
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/120080-ministry-of-farce-affairs-aka-foreign-afairs.html
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hakuna mwenye nia njema hapo
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Haya sasa... Membe, Tadayo, Merei.... something really wrong even outside ufisadi wanaoufanya wa kugawana mali za marehemu kabla ya kifo chake


  Hii nchi sijui nani msafi
   
 10. Rocket

  Rocket Senior Member

  #10
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  makampuni yote hayo yalifanya biashara gani na Libya mpk walipwe hela zote hizo!!!!!tujuzeni
   
 11. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #11
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  biashara ya mabomu na siraha kama ak 47.
   
 12. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2014
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Tehteh!
  watu wabaya,
  washa MU-MMgimwa mtu huko! ila wachote mipesa yao.
   
Loading...