Kampuni ya Uchimbaji mafuta Uganda yavunja Mkataba na TOTAL. Je, maslahi yetu kwenye Bomba la Mafuta yatakuwaje?

lwidia2k

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
396
1,000
Kiukweli kuna kitu nimekipata leo, some time miradi iliyoanzishwa awamu hii nilikua naichukulia negative kimazoea tu kuwa Africa and Tz in particular kuwa hatuwezi kitu labda ulaya,
Kumbe mambo yakikamilika yatakua mazuri tu. Time will tell, let us wait for it.
 
Duduwasha

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,714
2,000
Panda panda bei.. kila siku vitu vina panda bei... mwenye huo wimbo nauomba tafadhali
 
Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,502
2,000
Swala ni simple makampuni matatu yameingia mkataba wa kufanya Exploration and Production (kutafuta) kila mtu anatakiwa atoe equal capital na wamegawana equal shares.

Kati yao CNOOC na Total wana business interest za kutafuta, kuchakata na kuuza, isitoshe wanamitaji mikubwa. Tullow ni kampuni ambayo inashiriki kwenye kutafuta tu na wakishapata for the most part wanauza kisima na kusepa hawana interest kwenye value chain.

Tullow katika harakati zao za kukimbia gharama zingine za mbele kwenye partnership kama kuchangia bomba la mafuta na uwekezaji mwingine wa awali wanataka kupunguza share zao kwa kuwauzia wabia waliobaki na sehemu ya malipo itumike kama mchango kwenye kufanya hiyo shughuli. Hivyo kati ya $900m iliyokuwa wapate kwenye mauzo basi $700m wasipewe iende kwenye huo uwekezaji.

Na makubaliano yalikuwa yana muda baina ya wabia. Tullow na serikari ya Uganda washaelewana kwenye capital gain tax, tatizo wanunuzi pia wanatakiwa kulipa tax na wabia wanataka Tullow agharamie na upande huo hapo ndio mgomo ulipo.

Na jamaa walimpa deadline akishindwa option ya kuuza aweke hela yake mwenyewe uwekezaji uendelee anawachelewesha kuanza shughuli ya kutoa mafuta, jambo ambalo Tullow wanasema wapo committed nalo.
 
eliakeem

JF-Expert Member
May 29, 2009
11,073
2,000
Hiyo ni insignificant
Manamba wachache watakaotumika kujenga plus operators wachache watakaoajiriwa ni faida kiduchu sana kuliko makelele wanayotupigia Wanasiasa.
KAMA KWELI TUNANUFAIKA IPASAVYO KIASI CHA KUKUBALI KUTAKE RISK, WAAMBIE WAWEKE MKATABA WAZI TUUONE!. WANAFICHA NINI?

Kwa hiyo kwa kuwa mkataba hauko wazi basi ndiyo sababu inayokuonesha kuwa hakuna faida?

Kama ni hivyo, wewe umejuaje hizo hasara kama mkataba hauko wazi?

Lakini duniani kote mikataba ya kibiashara kati ya kampuni na serikali siyo nyaraka za wazi, ambazo zinapatikana kwenye public domain or gallery.
 
Adili

JF-Expert Member
Nov 3, 2007
3,142
2,000
Kampuni ya uchimbaji mafuta ya TALLOW ya nchini Uganda imevunja mkata wake na kampuni ya TOTAL ya Ufaransa na ile COON ya China kutokana na utata uliojitokexa kwenye maswala ya ushuru.

Source ITV habari

My take; Maslahi ya Tanzania kwenye bomba la mafuta yanaweza kupata changamoto yoyote kutokana na jambo hili?.....najiuliza tu!
Mkuu, itabidi tusahau ilo bomba kwa muda!
 
KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,376
2,000
Mafuta... Natural Resources in Africa..., is it a curse or a blessing ? Tufike wakati tuache utegemezi wa hizi resources zinazokwisha kwa long term sustainable well being.. Pia ingependeza zaidi kama kungekuwa na transparency ya haya mambo na hii mikabata ingepunguza sana assumptions...

And when it comes to oil the beneficiaries are always the same corporations.. For more information check out the documentary
 
Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
7,324
2,000
Sio tuu tulitakiwa tujenge bandari tuu, bali serikali zenye long time vision, by now tulitakiwa tujenge oil refinery ili tusinunue tena mafuta Arabuni, tununue ya Uganda yatakuwa cheaper.
P
Yatakuwaje cheap wakati London na New York Stock Markets ndio the Benchmark.
 
french

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
2,871
2,000
Swala ni simple makampuni matatu yameingia mkataba wa kufanya Exploration and Production (kutafuta) kila mtu anatakiwa atoe equal capital na wamegawana equal shares.

Kati yao CNOOC na Total wana business interest za kutafuta, kuchakata na kuuza, isitoshe wanamitaji mikubwa. Tullow ni kampuni ambayo inashiriki kwenye kutafuta tu na wakishapata for the most part wanauza kisima na kusepa hawana interest kwenye value chain.

Tullow katika harakati zao za kukimbia gharama zingine za mbele kwenye partnership kama kuchangia bomba la mafuta na uwekezaji mwingine wa awali wanataka kupunguza share zao kwa kuwauzia wabia waliobaki na sehemu ya malipo itumike kama mchango kwenye kufanya hiyo shughuli. Hivyo kati ya $900m iliyokuwa wapate kwenye mauzo basi $700m wasipewe iende kwenye huo uwekezaji.

Na makubaliano yalikuwa yana muda baina ya wabia. Tullow na serikari ya Uganda washaelewana kwenye capital gain tax, tatizo wanunuzi pia wanatakiwa kulipa tax na wabia wanataka Tullow agharamie na upande huo hapo ndio mgomo ulipo.

Na jamaa walimpa deadline akishindwa option ya kuuza aweke hela yake mwenyewe uwekezaji uendelee anawachelewesha kuanza shughuli ya kutoa mafuta, jambo ambalo Tullow wanasema wapo committed nalo.
Unajua maana ya capital gain tax wewe? Kama hujui sema uamniwe. Capital gain tax hawezi toa mnunuaji hata siku moja. Hayo mawazo yako
 
french

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
2,871
2,000
Mkuu
Nyanjomigire, crude oil prices is set by OPEC to it's member states, and not LSE or NSE, Uganda is not OPEC member, therefore we can get the best deal.
P
Unafeli mkuu. Crude oil price is set by the market forces of demand and supply. Kama price per barrel ni $50 (sweet oil) brent or WTI. ugandan oil will be atleast bellow that because its oil is waxy. OPEC is there only to control supply. If opec finds that the oil price has gone up they will increase supply and when the price goes down they will cut supply inorder to boost the price. Still none opec countries will take an advantage of producing more when they find the price is high but they will not be able to saturate the market.
 
Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,502
2,000
Unajua maana ya capital gain tax wewe? Kama hujui sema uamniwe. Capital gain tax hawezi toa mnunuaji hata siku moja. Hayo mawazo yako
Sikushauri uingie kwenye malumbano, endelea kutoa somo lako.
 
Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,502
2,000
Kama unahitaji somo hapa pia niambie mkuu....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom