Kampuni ya TBL yakubali kufuata maelekezo ya Serikali kununua shayiri nchini

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
658
821
KAMPUNI YA TBL YAKUBALI KUFATA MAELEKEZO YA SERIKALI

Dodoma, Tanzania.

Serikali imewahakikishia wakulima wa shayiri kupata soko la uhakika kwa kuiuzia moja kwa moja Kampuni ya Bia Tanazania TBL .

Akizungumza baada ya kikao chake na viongozi wa TBL kilichohudhuriwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Anthony Mavunde, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema wamekutana na viongizi wa TBL kufuatia kauli iliyoitoa hivi karibuni jijini Arusha kuhusu TBL kiingia mikataba ya kununua shayiri moja kwa moja kutoka kwa wakulima

Mhe. Bashe amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 TBL imedhamiria kufanya uwekezaji mkubwa nchini na iliiomba serikali mambo kadhaa ambayo yangeirahishia kampuni hiyo kuwekeza.

Waziri Bashe ameyataja maombi hayo ikiwa ni pamoja na nafuu ya kodi kwa zao la shayiri kama malighafi na kupata ardhi mkoani Dodoma.

Aidha Mhe. Bashe amebainisha kuwa kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Wizara ya Fedha serikali imeikubalia TBL maombi waliyoomba.

Pamoja na kukubaliwa kwa maombi waliyoomba, TBL imekubaliana na serikali kuingia mikataba na wakulima ya kununua tani za shayiri zisizopungua 5,000 hadi 6,000 kwa mwaka kutoka kwa wakulima.

Katika utekelezaji wa makubaliano hayo tayari TBL imeingia mikataba ya ununuzi wa tani 3,000 moja kwa moja kutoka kwa wakulima.

Ili kukamilisha malengo kwa mujibu wa makubaliano serikali imeielekeza TBL kwenda wilaya ya Hanang mkoani Manyara na kuingia mikataba ya tani 2,000 na
wakulima wa huko ili kukamilisha kiwango cha chini cha ununuzi walichokubaliana na serikali ambacho ni tani 5,000.

Mbali na makubaliano hayo, Mhe. Bashe amesema serikali imekubaliana na TBL kwenye kilimo cha mkataba cha zao la zabibu.

Waziri Bashe amefafanua kuwa baada ya majadiliano TBL wamekubaliana na serikali kuingia mikataba na wakulima wa zabibu wa mkoani Dodoma na kuwaelekeza viongozi wa TBL kushirikiana na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde kukamilisha mchakato huo.

Waziri Bashe amebainisha kuwa Wizara ya Kilimo inaamini kuwa wakulima wakiwa na makubaliano ya moja kwa moja na wakulima itawasaidia wakulima wa Tanzania na TBL itarahisha kazi katika kumfikia mkulima kwani kwa sasa ili TBL imfikie mkulima.

Kuhusu hitaji la kupata ardhi, Mhe. Bashe amesema tayari serikali imeshawapa hekari 250 mkoani Dodoma.

Akitoa shukrani kwa Wizara ya Kilimo Mkurugenzi Mkaazi wa TBL Jose Moran
amesema watafuata makubaliano waliyokubaliana na serikali kwani wamejidhatiti kuunga mkono juhudi za wakulima wa Tanzania na wataendelea kufanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Kilimo.

_DSC2710.JPG


_DSC2695.JPG


_DSC2708.JPG


_DSC2701.JPG


_DSC2707.JPG


_DSC2714.JPG
 
Angalau Kuna matumaini kwenye kilimo, mavunde na Bashe wanafanya vizuri wasipo haribiwa na chama
 
Serikali inaielekeza vipi kampuni binafsi? Wangesema wamewashauri ingekaa vizuri zaidi.

Amandla...
 
Masikini Bashe, siasa imempelekea kusaidia haramu.
Unafiki tu umewajaa..ukute hapo unazini na wala nguruwe..ila unajikuta mtu wadini.

Acheni wafanye kazi madamu ameamua kuitumikia nchi..angetaka dini angekuja kuwa imamu.

Btw dini afrika zimejaa wanafiki watupu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Unafiki tu umewajaa..ukute hapo unazini na wala nguruwe..ila unajikuta mtu wadini.

Acheni wafanye kazi madamu ameamua kuitumikia nchi..angetaka dini angekuja kuwa imamu.

Btw dini afrika zimejaa wanafiki watupu.

#MaendeleoHayanaChama
Kumbe Hussein hana dini sikujua, ndio unaniambia.
Hayo ulionisingizia ni yangu binafsi, lkn ya ulevi ni ya wengi.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom