Kampuni ya Peter Noni wa EPA ndiyo inakusanya michango ya CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni ya Peter Noni wa EPA ndiyo inakusanya michango ya CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Asprin, May 3, 2010.

 1. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,033
  Likes Received: 23,967
  Trophy Points: 280


  KAMPUNI iliyopewa kazi ya kukusanya fedha za kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) – Push Mobile Media Limited – inahusishwa na watuhumiwa wa ufisadi nchini, MwanaHALISI limegundua.

  Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo katika ofisi ya Wakala wa Usajili wa Makampuni na Biashara (BRELA), mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo ni Peter Noni.

  Hivi sasa Noni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Raslimali ya Taifa (TIB); nafasi aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete yapata mwaka mmoja sasa.

  Kabla ya uteuzi wake, Noni aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Utendaji katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), amekuwa akisakamwa kwa tuhuma za ufisadi ndani ya benki hiyo.

  Kwanza, mlipuko wa ufisadi ndani ya BoT ulitokea Noni akiwa mtu wa madaraka makubwa na wa karibu na Gavana Daudi Balali aliyebebeshwa mzigo wote wa wizi wa aina yake nchini.

  Pili, kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Timu ya Rais Kikwete aliyoiunda kuchunguza wizi BoT, karibu watuhumiwa wote wa ufisadi waliofikishwa mahakamani walimtaja Noni kuwa mshirika mkuu katika kufanikisha wizi huo.

  Leo hii, moja ya makampuni mawili yanayounda Push Mobile Media Limited, iliyopewa kazi na CCM, inamilikiwa na Peter Noni.

  Kampuni hiyo ambamo Noni ni mkurugenzi inaitwa Six Telecoms Company Limited (STC) iliyosajiliwa Dar es Salaam kwa hati Na. 50940.

  Mkuu huyo wa TIB ana hisa 700 kati ya hisa 1,000 za STC. Hisa zilizosalia zinamilikiwa na wenzake wawili, Dk. R. W. Tenga na Hafidh M. Shamte.

  Ni Noni aliyekuwa bosi wa Esther Komu, Imani Mwakosya na Bosco Kimela ambao ni miongoni mwa wafanyakazi wa BoT waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi.

  Watumishi hao wa benki wamekuwa wakidai kuwa Noni ndiye alikuwa mwidhinishaji wa malipo yote ya fedha zilizokombwa na wanashangaa kwa nini hayuko kizimbani.

  Rais Kikwete alimteua Noni kuwa bosi wa TIB katikati ya tuhuma hizo.

  Kana kwamba rais hasikii tuhuma hizo, akasema fedha zote zinazokusanywa kutoka kwa mafisadi waliokiri na hivyo kuepushwa kupelekwa mahakamani, zitapelekwa TIB ambako zitasimamiwa na Noni.

  Hadi sasa Noni hajafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zozote zile za ufisadi na malalamiko ya wafanyakazi wenzake hayajafanyiwa kazi.

  Kwa hiyo Noni wa BoT ndiye yuleyule wa TIB anayeshughulikia fedha zilizoibwa BoT; na kampuni yake ndiyo inashughulikia ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya kampeni za CCM mwaka huu.

  Kampuni nyingine inayounda Push Mobile Media Limited ni Opera Telecoms. Kila kampuni inamiliki asilimia 50 ya hisa za Push Mobile.

  Wiki mbili zilizopita, CCM ilizindua mpango wa kutafuta fedha za kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu, ambapo imepanga kukusanya zaidi ya Sh. 40 bilioni zikiwamo zile za kupitia ujumbe mfupi wa simu za mkononi (sms).

  Six Telecoms ina ofisi katika jengo la Barclays, mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam. Inatumia anwani ya S.L.P 11133, Dar es Salaam.

  Anuani ya kampuni ya Opera Telecoms ni 3 Brindley Place, Birmingham -1 2JB nchini Uingereza.

  Kuwapo kwa Noni katika umiliki wa Push Mobile, kunajenga uwezekano mkubwa wa kuwapo ubia au ushirikiano na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.

  Noni na Rostam ni wabia katika biashara – kwa pamoja wanamiliki hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

  Noni na Rostam walikuwa wanamiliki asilimia 35 ya hisa katika kampuni ya hiyo.

  Noni alikuwa anamiliki hisa zake kupitia kampuni ya Planetel Communications Limited, huku Rostam akimiliki kupitia kampuni ya Caspian Construction Limited.

  Hivi sasa hisa hizo 35 zinamilikiwa na kampuni ya Mirambo Limited ambayo taarifa za mtandao hazionyeshi iwapo zinamilikiwa kwa pamoja au na Rostam peke yake.

  Miaka miwili iliyopita wamiliki wa Mirambo walipeleka maombi kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutaka kuuza hiza zao katika Vodacom kwa wawekezaji wa nje; lakini imeripotiwa serikali iliwakatalia.

  Rostam anamiliki makampuni mengi nchini, lakini hakuna hata moja ambako jina lake linaonekana wazi isipokuwa katika hisa za Vodacom.

  Hata katika kampuni ya uchapishaji magazeti ya New Habari Corporation Limited, ambayo amekiri hadharani kuimiliki, jina lake halionekani.

  R.W. Tenga anayetajwa kuwa mkurugenzi wa Six Telecoms, sasa ndiye mwanasheria wa BoT.
   
 2. S

  SHAMTE Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni hatari
   
 3. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Binamu siku hizi umehamia huku? angalia haya mambo yatakupa pressure ooh hooo!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  CCM imejengwa juu ya msingi wa Ufisadi, na hilo ni wazi...Wanaoshangaza ni wale wanaochaji simu zao, na kujaza fedha, na kuzituma huko CCM ili kuwastawisha watu ambao tayari MATUMBO YAO hayabebeki kwa vitambi.....
  Mi nasema wanaotuma pesa huko ni wapumbavu!
   
 5. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,033
  Likes Received: 23,967
  Trophy Points: 280
  Acha tu binamu. Mambo mengine yanatisha mpaka tunajisahau tunaingia vyoo vya wenzetu.
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,033
  Likes Received: 23,967
  Trophy Points: 280
  Mi hapo nimesoma Machizi!
   
 7. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye red nakubaliana na wewe.. hao jamaa ni majuha ama mazuzu kabisaa!
   
 8. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  mh! CCM? kazi kwelikweli, huyu Tenga saini yake ipo katika yale makabrasha ya wizi wa EPA na usajili wa kampuni ya kagoda. Tenga anaijui vizuri sana kagoda.
   
 9. M

  Msindima JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mamboz binamu,siku hizi umehamia kwenye siasa? naichukia sana siasa ya nchi hii.
   
 10. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mi natamani 'Natural hazards zitusaidie kutuondolea watu hawa'biashara za kupiga kura, tutapiga lakini hawatang'oka!
   
 11. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  mi hata siwaelewi watu wanaotuma hizo sms, hivi akili zinawatosha?
   
 12. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kirefu cha CCM ni Chukua Chako Mapema. Wakati wa mabadiliko ndio huu.
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Uzuri tu ni kuwa hakuna atakaye kufa akazikwa na pesa.....wote akina RA, JK, Mkapa, mwinyi, makamba, n.k. watakufa na kuacha kila kitu juu ya ardhi, kwani Ditopile yuko wapi????
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  MODS:
  Hii topic imerudiwa, na ni bora ikaunganishwa na ile iliyotangulia chini ya 'Uchaguzi Tz 2010' yenye heading 'Mafisadi waziteka kampeni za Kikwete'. Source ya topic hii ni gazeti la Mwanahalisi, current issue.
   
 15. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  nimekubali kwamba hii ni JF MPYA..........!
  maanake dah!
  enewei NOTED WITH MANY THANKS
   
 16. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #16
  May 3, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  PJ nimwkusoma kwa heshima na taadhima uko sahihi, kuwa CCM imejegwa juu ya msingi wa Ufisadi.
   
 17. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2010
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ni Mungu peke yake aliyekuwepo, aliyepo na atakayekuwepo hata milele. Hawa wanaojilisha upepo watapita na maiti zao zitaliwa na kunguru. Hakika, siku yaja wana wa Nchi hii hawatawaimbia na kuamini katika wanasiasa MATUMBO
   
 18. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  PJ nimekupata.
   
 19. j

  jingoist Member

  #19
  May 3, 2010
  Joined: Mar 24, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yani kama yalomkuta mkuu wa poland au?? hahahaaa
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu Magezi,
  Na heshima zote mbele kwa mbele. Maneno kama haya ndiyo yanatuumiza sana sisi Waafrica. Mafuriko yakitokea ni MAPENZI YA MUNGU. Watu wanaiba pesa zetu watu mnasema "watakufa wataziacha", wakina mama wanazaa kama nguruwe kule Temeke na wanakufa kama nzi, na sisi tunasema ni MAPENZI YA MUNGU.
  Naomba tuachane na hiyo mila na tuwe na fikira kubwa kuwa:
  1. Mungu hayupo na hakuna AHERA wala pepo. Kila kitu kinaanzia duniani na kuishia hapa.
  2. Hakuna lisilowezekana.
  3. Ili uvune Mahindi mengi, basi kubali Mahindi kadhaa yaoze, yaote na yakue na hapo utapata Mahindi mengi zaidi.
  4. Maisha yako si Kitu ila maisha ya wanao. Sasa wee, umewaandalia nini wanao kwa siku za mbele?
  5. Ili uende PEPONI basi lazima UFE.
  6. Hakuna UCHAWI.

  Ukiweza kuvunja hizo imani chache na nyingine kadhaa kama nimezisahau, utaona kuwa ni MAKOSA YA HALI YA JUU kusimama na kusema "Acha tu waibe maana wataziacha......" Sasa hata wakiziacha, watakuwa wamefaidi sana maisha yao na watoto wao, na wajukuu zao. Wewe utabaki Matonya milele, watoto wako hivyohivyo na Wajukuu zako..... Hapo sasa inabidi uwe na msemo wa KIFARANSA kuwa "WE HAVE NOTHING TO LOOSE......", tukose wote.
   
Loading...