Kampuni ya NAFTALI ya Algeria Kuja kuwekeza nchini katika Usambazaji wa gesi

S

security guard

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Messages
708
Points
500
S

security guard

JF-Expert Member
Joined Sep 27, 2011
708 500
Miongoni mwa matunda ambayo yametokana na Ziara ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo nchini Algeria ni pamoja na Kampuni ya Umma ya Algeria, NAFTAL inayosindika na kusambaza gesi ya kupikia mijini na vijijini kukubali kuja kuwekeza nchini.

Nchi ya Algeria ambayo ina asili ya Jangwa na Nyika imeacha kabisa kutumia kuni pamoja na mkaa kwa mahitaji yao ya jikoni na badala yake wanatumia gesi ambayo inavunwa, kusindikwa na kusambazwa nchini mwao.

Kampuni Kubwa ya NAFTAL ambayo husindika gesi kiasi cha 2milion tons/year (LPG for domestic use) inasambaza LPG kutumia mabomba yenye urefu 2,886km, pamoja na magari na reli kuwafikia wanavijiji.

Kampuni hiyo sasa inajiandaa kuja nchini kufanya visibility study juu ya hatua muhimu za kuanza nazo katika uwekezaji huo mkubwa hapa nchini ambao utasaidia kuokoa maliasili nyingi zitokanazo na misitu. Tanzania imetoa ripoti ya maliasili na kubainisha hasara kubwa itokanayo na matumizi ya mkaa na kuni na uvunaji haramu wa mazao ya misitu ikiwemo mbao na magogo. Kuingia kwa Mradi huu hapa nchini kutapelekea Misitu yetu kubaki salama na hivyo kuchangia katika kudumisha hali ya hewa safi nchini.

Hongera Profesa Muhongo kwa hatua hii muhimu kwa maendeleo ya nchi na wananchi wa Tanzania.
 
N

NasDaz

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Messages
11,300
Points
2,000
N

NasDaz

JF-Expert Member
Joined May 6, 2009
11,300 2,000
Wakati mjadala wa vitalu vya gesi ukiwa umepamba moto; nilipata kuzungumzia opportunity iliyopo katika upande huu wa biashara ya gesi...kwamba kuwa na mtandao wa gas pipes across big cities like Dar es salaam for domestic consumption. Kutembea na mitungi ya gas barabarani ni kama kutembea na ndoo za maji; watu wengi wata-opt kuunganishwa kwenye mtandao wa gas pipelines. Ukiwa na wateja 500,000 Dar es salaam, with Sales of TZS 20,000/- kwa mwezi; tayari una Total Revenue ya TZS 10 billion kwa mwezi!! Ukiweza kutoa bomba from Dar es salaam to Arusha; then hapo obvious utakuwa unapiga hodi Nairobi! Five years plan unaweza kujikuta una 5 million customers across East Africa Market. Ukija kuchanganya na outlets za kawaida.....Lakini Watanzania opportunity kama hizi hatuzioni na badala yake wote tunataka Vitalu!!!
 
Ni labda kwa sababu jamii yetu haipo kibiashara zaidi, na hili ni historical kwa maana aliyefungua milango ya biashara na kupanua mawazo ya uwekezaji ni rais wa awamu ya pili maarufu kwa jina la Bwana Rukhsa ambae ndie alifungua milango ya bidhaa za nje kuingia nchini na kukuza ama kufungua milango ya biashara.

Watanzania wengi wamebobea katika udalali (MENGI) akiwa kinara wa watu hao, hawaoni sababu ya kujishughulisha katika kufikiri namna nyingine za uwekezaji nje ya Udalali. Anachofikiria yeye ni kuwa apate kitalu ili apige besenga kwa Mzungu mmoja ambae atampa kitalu hicho na yeye abaki na ten percent yake mfukoni.

Watu wachache sana miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wanafikiria namna mpya na bora za kiuwekezaji, nawasifu Bakhresa, Mo na Manji ambao kila uchao wanatafuta mbinu mpya za kujiimarisha kwenye soko, wakati ndugu yangu mengi kila siku anabuni mbinu mpya za ukuwadi na udalali na kugombana na mawaziri na viongozi wa Serikali.
 
Forum statistics

Threads 1,324,623
Members 508,740
Posts 32,168,253
Top