Kampuni ya Mwananchi Communication Tanzania kununuliwa na Mzawa

Shigganza

Senior Member
May 24, 2018
160
412
Nation Media Group of Kenya (NMGK) inayomiliki magazeti, television, Radio na digital Media katika Nchi za Afrika za Afrika Mashariki na kati imefikia makubaliano ya kuiuza Mwananchi Commuication Tanzania mchapishaji wa Magazeti ya Mwananchi na The Citizen kwa mfanyabiashara mzawa Jehangir Kermali Bhaloo mwenye uhusiano na Mtandao wa Aga Khan kwa dau ambalo halijawekwa wazi hadi sasa.

Kupitia mauzo hayo inatarajiwa MCL kuwa uwekezaji wa mtu binafsi "Personal Private Investment"

Ikumbukwe kuwa Nation Media Group waliinunua kampuni ya Mwananchi Communication Limited mwaka 2002 kwa kiasi ambacho hakikuweka hadharani. Hata hivyo kuna mkanganyiko kuhusu mgawanyo na umiliki wa hisa katika kampuni hiyo kwa sasa. Mathalani kwa mujibu wa dodoso zilizojazwa na Group Media of Kenya na kuonwa na gazeti la The business times, NMGK inamiliki asilimia 99 ya hisa zote na Linus Gitahi inamiliki asilimia moja.

Huku kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kurugenzi wa huduma ya habari ambaye pia ni msajili wa Magazeti Nchini NGK inamiliki asilimia 49 ya hisa MCL na zilizobaki asilimia 51 zinamilikiwa na Jehangir Kermali Bhaloo.

Chanzo cha taarifa : Business Times ya tarehe 19 hadi 25 Juni 2019
 
mwaka mpaka uishe huu mengi tutakuwa tumeyaona
tapatalk_1500201109326.gif
 
Mnunuzi mpya akiwa kada.wa kijani basi utakuwa ni mwisho wa credibility ya MCL kama zilivyo karibu media zote kwa sasa

Kiongozi,
Umeona mbali uchaguzi 2020 unakaribia CCM wameona kumtumia mzawa huyu kutaondoa makelele na ususiaji wa wananchi kutazama / kusoma habari toka kwa chombo chochote cha media kilichonunuliwa na CCM moja kwa moja mfano Channel Ten TV, Uhuru Media n.k
 
Hivi huyo Jihangir Bhaloo ni kabila gani mbn siyaoni katika Yale makabila 120 aliyotuachia mwalimu
 
Back
Top Bottom