Kampuni ya mtandao wa kijamii ya Trump yapata dola bilioni 1 kutoka kwa wawekezaji

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542

Kampuni ya mtandao wa kijamii ya Trump yapata dola bilioni 1 kutoka kwa wawekezaji​


Former US president Donald Trump

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mradi mpya wa Donald Trump wa mtandao wa kijamii umechangisha $1bn (£755m) kutoka kwa wawekezaji kabla ya kuorodheshwa katika soko la hisa.

Taasisi ya habari na teknolojia ya Trump inatarajia kuzindua programu hiyo ya mitandao ya kijamii uitwayo Truth Social mapema mwaka ujao.

Haya yanajiri wakati Bw Trump akiwa amepigwa marufuku kutoka kwa Twitter na Facebook kufuatia shambulio la Ikulu ya Marekani mwezi Januari.

"$1bn imetuma ujumbe muhimu kwa makampuni makubwa yateknolojia kwamba udhibiti na ubaguzi wa kisiasa lazima ukomeshwe," alisema.

"Kadiri karatasi yetu ya usawa inavyoongezeka, taasisi ya Trump Media & Technology itakuwa katika nafasi nzuri ya kupambana dhidi ya udhalimu wa makampuni makubwa ya teknolojia."
Bw Trump alitangaza mipango ya kuzindua mtandao wa Kijamii wa Truth (Ukweli ) mapema mwaka huu, akisema itaruhusu mazungumzo "bila ubaguzi kwa misingi ya itikadi za kisiasa".
Kampuni ya habari na teknolojia ya Trump inashirikiana na Digital World Acquisition katika mradi huo.

Siku ya Jumamosi, walisema wamechangisha $1bn kutoka kwa "kundi tofauti la wawekezaji wa taasisi" bila kufichua wao ni nani.

Kwa mujibu wa ripoti, mradi huo wa mitandao ya kijamii sasa una thamani ya karibu $4bn.
Inasisitiza uwezo wa rais huyo wa zamani wa Marekani kuvutia uungwaji mkono mkubwa wa kifedha licha ya utata uliozingira wakati wake wa uongozi.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Maandamano katika bunge la Marekani, Capitol mwezi Januari

Bwana Trump alipigwa marufuku ya kutumia majukwaa makubwa ya mitandao ya kijamii baada ya shambulio la Januari 6 la wafuasi wake kwenye Ikulu ya Marekani huko Washington DC huku kukiwa na wasiwasi kwamba rais wa wakati huo angechochea ghasia zaidi.

Ilikuja baada ya Bw Trump kutoa madai, bila ushahidi, ya udanganyifu ulioenea katika uchaguzi wa urais wa mwaka jana.

Makampuni mengi ya Wall Street yalipuuza fursa ya kuwekeza katika mradi mpya wa rais huyo wa zamani, kwa mujibu wa Reuters.

Lakini baadhi ya fedha, makampuni ya uwekezaji wa familia na watu binafsi wenye thamani ya juu wameiunga mkono.

Bw Trump alikuwa na wafuasi milioni 89 kwenye Twitter na 33 Facebook 24 instra
 
Wachina na shithole countriies hautuhusu huo mtandao.
Kama kuna mwafrika atajiunga na huo mtandao atakiwa zwazwa aka hazimtoshi.
Kilichomtoa madarani ni ubaguzi hakuna kingine, alibagua warabu,waafrika wachina,wamexico nk. Huo mtandao wake sijui afanyeje ashawish watu aliowatenda.
 
Back
Top Bottom