Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Meneja mkuu wa Foton nchini Kenya Bw. Sun Qingzhong amesema kampuni hiyo imedhamiria kutangaza bidhaa zake duniani, imeweka mpango wa muda mrefu wa kuendeleza masoko nchini Kenya na barani Afrika kwa ujumla.
Ameongeza kuwa kampuni yake itaunganisha magari yake huko Miritini, magharibi mwa Mombasa, na kulenga kuwapatia wenyeji bidhaa zenye kiwango cha juu.
Kwa upande mwingine kampuni hiyo pia itatoa vipuri, na kuongeza nafasi za ajira, na hivyo kusaidia maendeleo ya uchumi wa Kenya.