Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania yampongeza Rais Magufuli na kuipongeza Tanzania, kujenga mazingira bora ya biashara ya Mafuta, Uwekezaji

Mayalla ni msukule wa lumumba
 
Attachments

  • IMG-20200902-WA0020.jpg
    IMG-20200902-WA0020.jpg
    103.7 KB · Views: 2
Wanabodi,

Kampuni ya Mafuta ya Total, imempongeza Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na serikali yake ya awamu ya tano, kwa kujenga mazingira wezeshi ya biashara, na uwekezaji, yanayovutia wawekezaji wa kimataifa kuleta mitaji ya uwekezaji nchini na kuwawezesha Watanzania kupatiwa fursa za kuingia katika biashara za ubia za vituo vya mafuta vya kiwango cha kimataifa.

Pongezi hizo zimetolewa leo, na Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta cha Total, Total Mchigani, kilichopo Goba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kinachomilikiwa na Mtanzania mzawa. Kituo hicho kiko kwenye moja ya barabara yenye shughuli nyingi za kiuchumi jijini Dar es salaam inayotokea Mbezi Beach hadi Mbezi Kimara hivyo kulenga kuwahudumia wakaazi wa Tegeta, Mbezi Beach na Kimara pamoja na watumiaji wote wa barabara hiyo.

“Napenda kutumia nafasi hii, kumshukuru Rais wa Tanzania, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwezesha ukuaji wa kibiashara kwenye sekta ya nishati. Pia tunatambua kuwa uzinduzi huu usingewezekana pasingekuwa na baraka za serikali ambayo waliidhinisha leseni za kuendesha kituo hiki na kwa hilo shukrani zangu za dhati zinaenda kwa EWURA na pamoja na taasisi zingine za kiserikali zilizowezesha jambo hili kufanikiwa” Alisema Bw. Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp

Bwana Jean Franchois ameongeza kuwa Total Tanzania imekuwa ikihimiza wamiliki wa biashara kukuza biashara zao kwa kuingia ubia wa kibiashara na kampuni hiyo kwa njia ya DODO ambayo itawawezesha kumiliki na kuendesha vituo vya mafuta vyenye chapa ya Total. DODO ni mfumo wa kibiashara ambao kampuni ya hiyo hutumia kuweza kuongeza mtandao wa vituo vyake nchini. Mfumo huu unawawezesha wafanyabiahsara kuingia kwenye ubia na kampuni ya Total na kuweza kumiliki, kuendesha Pamoja na kusimamia vituo vya huduma vya Mafuta vyenye chapa ya Total.

Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp alisema Total inalenga kumfikia kila Mtanzania na kuwapatia nafasi ya kufuruhia huduma na bidhaa nzuri kutoka Total. Pia tunawaalika wafanya biashara ambao wangependa kupanua biashara zao kuungana nasi kupitia mpango wetu wa DODO na kupata nafasi ya kumiliki kituo cha huduma ya mafuta na kuweza kupanua na kuimarisha biashara zao.

Aliongeza kuwa; Leo, tunafurahia kuingia katika ubia wa kibiashara na Mhandisi Frank Malle ambae ni mmiliki wa kampuni ya F.S Mshuwa Co na mmiliki wa kituo hichi. Kwa ushirikiano huu tunatarajia kuihudumia Goba na jamii inayoishi maeneo ya jirani. Pia ningependa kutumia fursa hii kuwaalika wafanya biashara ambao wangependa kupanua biashara zao kuungana nasi kupitia mpango wetu wa DODO na kupata nafasi ya kumiliki kituo cha huduma ya mafuta na kuweza kupanua na kuimarisha biashara zao.

Kwa upande wake, mmiliki wa kituo hicho, Frank Malle, ameishukuru Total sio tuu kwa kuwawezesha kumiliki kituo hicho, bali pia kuwaokoa wasiuze ardhi yao, maana walishawishiwa sana kuuza ardhi, lakini Total ikawakomboa, sasa na wao ni wamiliki wa kituo cha kisasa cha mafuta cha Total.

Paskali
View attachment 1556125View attachment 1556126View attachment 1556127View attachment 1556128View attachment 1556129View attachment 1556130View attachment 1556131View attachment 1556132
Mbona wanakimbia??????
 
Pascal Mayalla Mkuu ushasikia wapi Mzungu akaponda kitu?

Tabia ya mzungu hata akija kwenye nyumba ya udogo ataisifia udongo na fito zilizojengea hiyo nyumba. Mzungu huwa hadis kitu hata siku moja.

Experience: nafanya nao kazi kwa miaka 15 sasa.
Ni kwa sababu Mtu Mweusi ni "sensitive" sana haswa linapokuja swala la "black and White"....kama inavyoendelea kule US.

Kama ilivyoandikwa kwenye Biblia kuwasihi Waume "ishini nao kwa akili" nadhani nao huwa wanahimizana vivyo hivyo dhidi yetu.
 
Ni kwa sababu Mtu Mweusi ni "sensitive" sana haswa linapokuja swala la "black anda White"....kama inavyoendelea kule US.

Kama ilivyoandikwa kwenye Biblia kuwasihi Waume "ishini nao kwa akili" nadhani nao huwa wanahimizana vivyo hivyo dhidi yetu.
Kabisa, wanacheza na akili zetu. Sisi tunaona wanatusifu kumbe wanatung'ong'a
 
Wanabodi,

Kampuni ya Mafuta ya Total, imempongeza Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na serikali yake ya awamu ya tano, kwa kujenga mazingira wezeshi ya biashara, na uwekezaji, yanayovutia wawekezaji wa kimataifa kuleta mitaji ya uwekezaji nchini na kuwawezesha Watanzania kupatiwa fursa za kuingia katika biashara za ubia za vituo vya mafuta vya kiwango cha kimataifa.

Pongezi hizo zimetolewa leo, na Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta cha Total, Total Mchigani, kilichopo Goba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kinachomilikiwa na Mtanzania mzawa. Kituo hicho kiko kwenye moja ya barabara yenye shughuli nyingi za kiuchumi jijini Dar es salaam inayotokea Mbezi Beach hadi Mbezi Kimara hivyo kulenga kuwahudumia wakaazi wa Tegeta, Mbezi Beach na Kimara pamoja na watumiaji wote wa barabara hiyo.

“Napenda kutumia nafasi hii, kumshukuru Rais wa Tanzania, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwezesha ukuaji wa kibiashara kwenye sekta ya nishati. Pia tunatambua kuwa uzinduzi huu usingewezekana pasingekuwa na baraka za serikali ambayo waliidhinisha leseni za kuendesha kituo hiki na kwa hilo shukrani zangu za dhati zinaenda kwa EWURA na pamoja na taasisi zingine za kiserikali zilizowezesha jambo hili kufanikiwa” Alisema Bw. Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp

Bwana Jean Franchois ameongeza kuwa Total Tanzania imekuwa ikihimiza wamiliki wa biashara kukuza biashara zao kwa kuingia ubia wa kibiashara na kampuni hiyo kwa njia ya DODO ambayo itawawezesha kumiliki na kuendesha vituo vya mafuta vyenye chapa ya Total. DODO ni mfumo wa kibiashara ambao kampuni ya hiyo hutumia kuweza kuongeza mtandao wa vituo vyake nchini. Mfumo huu unawawezesha wafanyabiahsara kuingia kwenye ubia na kampuni ya Total na kuweza kumiliki, kuendesha Pamoja na kusimamia vituo vya huduma vya Mafuta vyenye chapa ya Total.

Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp alisema Total inalenga kumfikia kila Mtanzania na kuwapatia nafasi ya kufuruhia huduma na bidhaa nzuri kutoka Total. Pia tunawaalika wafanya biashara ambao wangependa kupanua biashara zao kuungana nasi kupitia mpango wetu wa DODO na kupata nafasi ya kumiliki kituo cha huduma ya mafuta na kuweza kupanua na kuimarisha biashara zao.

Aliongeza kuwa; Leo, tunafurahia kuingia katika ubia wa kibiashara na Mhandisi Frank Malle ambae ni mmiliki wa kampuni ya F.S Mshuwa Co na mmiliki wa kituo hichi. Kwa ushirikiano huu tunatarajia kuihudumia Goba na jamii inayoishi maeneo ya jirani. Pia ningependa kutumia fursa hii kuwaalika wafanya biashara ambao wangependa kupanua biashara zao kuungana nasi kupitia mpango wetu wa DODO na kupata nafasi ya kumiliki kituo cha huduma ya mafuta na kuweza kupanua na kuimarisha biashara zao.

Kwa upande wake, mmiliki wa kituo hicho, Frank Malle, ameishukuru Total sio tuu kwa kuwawezesha kumiliki kituo hicho, bali pia kuwaokoa wasiuze ardhi yao, maana walishawishiwa sana kuuza ardhi, lakini Total ikawakomboa, sasa na wao ni wamiliki wa kituo cha kisasa cha mafuta cha Total.

Paskali
View attachment 1556125View attachment 1556126View attachment 1556127View attachment 1556128View attachment 1556129View attachment 1556130View attachment 1556131View attachment 1556132
Kaka Pascal, mbona hii kampuni ipo Tanznia Miaka mingi tuu na hata Ndugu yangu mmoja anamiliki sheli 3 mjini Dar za Total tokea miaka ya 1990 .
Kipi cha ajabu kusifiwa Magufuli au CCM hapa?
Labda tuisifu serikali kwa kutowa leseni kama iliivyo towa leseni kwa kampuni za Engen, BP, Camel, Oil Com,Lakes, Big Bon na nyenginezo nyingi ambazo humilikiwa na watanzania wenyewe na hutumia tuu Majina hayo ya Mabeberu ki ubia . Nini hasa hapa zaidi ya Promo?
Kule Zanzibar Kuna Shirika la kizalendo linaitw Z-Petro na Gapco la Mabeberu
Hii nayo tumsifu Dr.Miwinyi au Dr. Sheni?.
Kwanini Total tuuu?
Kwanini Ubiya kwa Mtanzania Huyu tuu?
Au na wewe umo kwenye PROMOTION YA Total?
Cheap Politicks kaka
Naona kama unafulia kuandishi?
 
Wanabodi,

Kampuni ya Mafuta ya Total, imempongeza Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na serikali yake ya awamu ya tano, kwa kujenga mazingira wezeshi ya biashara, na uwekezaji, yanayovutia wawekezaji wa kimataifa kuleta mitaji ya uwekezaji nchini na kuwawezesha Watanzania kupatiwa fursa za kuingia katika biashara za ubia za vituo vya mafuta vya kiwango cha kimataifa.

Pongezi hizo zimetolewa leo, na Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta cha Total, Total Mchigani, kilichopo Goba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kinachomilikiwa na Mtanzania mzawa. Kituo hicho kiko kwenye moja ya barabara yenye shughuli nyingi za kiuchumi jijini Dar es salaam inayotokea Mbezi Beach hadi Mbezi Kimara hivyo kulenga kuwahudumia wakaazi wa Tegeta, Mbezi Beach na Kimara pamoja na watumiaji wote wa barabara hiyo.

“Napenda kutumia nafasi hii, kumshukuru Rais wa Tanzania, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwezesha ukuaji wa kibiashara kwenye sekta ya nishati. Pia tunatambua kuwa uzinduzi huu usingewezekana pasingekuwa na baraka za serikali ambayo waliidhinisha leseni za kuendesha kituo hiki na kwa hilo shukrani zangu za dhati zinaenda kwa EWURA na pamoja na taasisi zingine za kiserikali zilizowezesha jambo hili kufanikiwa” Alisema Bw. Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp

Bwana Jean Franchois ameongeza kuwa Total Tanzania imekuwa ikihimiza wamiliki wa biashara kukuza biashara zao kwa kuingia ubia wa kibiashara na kampuni hiyo kwa njia ya DODO ambayo itawawezesha kumiliki na kuendesha vituo vya mafuta vyenye chapa ya Total. DODO ni mfumo wa kibiashara ambao kampuni ya hiyo hutumia kuweza kuongeza mtandao wa vituo vyake nchini. Mfumo huu unawawezesha wafanyabiahsara kuingia kwenye ubia na kampuni ya Total na kuweza kumiliki, kuendesha Pamoja na kusimamia vituo vya huduma vya Mafuta vyenye chapa ya Total.

Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp alisema Total inalenga kumfikia kila Mtanzania na kuwapatia nafasi ya kufuruhia huduma na bidhaa nzuri kutoka Total. Pia tunawaalika wafanya biashara ambao wangependa kupanua biashara zao kuungana nasi kupitia mpango wetu wa DODO na kupata nafasi ya kumiliki kituo cha huduma ya mafuta na kuweza kupanua na kuimarisha biashara zao.

Aliongeza kuwa; Leo, tunafurahia kuingia katika ubia wa kibiashara na Mhandisi Frank Malle ambae ni mmiliki wa kampuni ya F.S Mshuwa Co na mmiliki wa kituo hichi. Kwa ushirikiano huu tunatarajia kuihudumia Goba na jamii inayoishi maeneo ya jirani. Pia ningependa kutumia fursa hii kuwaalika wafanya biashara ambao wangependa kupanua biashara zao kuungana nasi kupitia mpango wetu wa DODO na kupata nafasi ya kumiliki kituo cha huduma ya mafuta na kuweza kupanua na kuimarisha biashara zao.

Kwa upande wake, mmiliki wa kituo hicho, Frank Malle, ameishukuru Total sio tuu kwa kuwawezesha kumiliki kituo hicho, bali pia kuwaokoa wasiuze ardhi yao, maana walishawishiwa sana kuuza ardhi, lakini Total ikawakomboa, sasa na wao ni wamiliki wa kituo cha kisasa cha mafuta cha Total.

Paskali
View attachment 1556125View attachment 1556126View attachment 1556127View attachment 1556128View attachment 1556129View attachment 1556130View attachment 1556131View attachment 1556132
Hii habari ya zamani sana,miaka kadhaa imepita
 
Pascal Mayalla Mkuu ushasikia wapi Mzungu akaponda kitu?

Tabia ya mzungu hata akija kwenye nyumba ya udogo ataisifia udongo na fito zilizojengea hiyo nyumba. Mzungu huwa hadis kitu hata siku moja.

Experience: nafanya nao kazi kwa miaka 15 sasa.
Hiki ulicho kisema ni sahihi kabisa .. Hata Mimi pia nina hii experience
 
Back
Top Bottom