Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania yampongeza Rais Magufuli na kuipongeza Tanzania, kujenga mazingira bora ya biashara ya Mafuta, Uwekezaji

Wanabodi,

Kampuni ya Mafuta ya Total, imempongeza Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na serikali yake ya awamu ya tano, kwa kujenga mazingira wezeshi ya biashara, na uwekezaji, yanayovutia wawekezaji wa kimataifa kuleta mitaji ya uwekezaji nchini na kuwawezesha Watanzania kupatiwa fursa za kuingia katika biashara za ubia za vituo vya mafuta vya kiwango cha kimataifa.

Pongezi hizo zimetolewa leo, na Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta cha Total, Total Mchigani, kilichopo Goba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kinachomilikiwa na Mtanzania mzawa. Kituo hicho kiko kwenye moja ya barabara yenye shughuli nyingi za kiuchumi jijini Dar es salaam inayotokea Mbezi Beach hadi Mbezi Kimara hivyo kulenga kuwahudumia wakaazi wa Tegeta, Mbezi Beach na Kimara pamoja na watumiaji wote wa barabara hiyo.

“Napenda kutumia nafasi hii, kumshukuru Rais wa Tanzania, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwezesha ukuaji wa kibiashara kwenye sekta ya nishati. Pia tunatambua kuwa uzinduzi huu usingewezekana pasingekuwa na baraka za serikali ambayo waliidhinisha leseni za kuendesha kituo hiki na kwa hilo shukrani zangu za dhati zinaenda kwa EWURA na pamoja na taasisi zingine za kiserikali zilizowezesha jambo hili kufanikiwa” Alisema Bw. Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp

Bwana Jean Franchois ameongeza kuwa Total Tanzania imekuwa ikihimiza wamiliki wa biashara kukuza biashara zao kwa kuingia ubia wa kibiashara na kampuni hiyo kwa njia ya DODO ambayo itawawezesha kumiliki na kuendesha vituo vya mafuta vyenye chapa ya Total. DODO ni mfumo wa kibiashara ambao kampuni ya hiyo hutumia kuweza kuongeza mtandao wa vituo vyake nchini. Mfumo huu unawawezesha wafanyabiahsara kuingia kwenye ubia na kampuni ya Total na kuweza kumiliki, kuendesha Pamoja na kusimamia vituo vya huduma vya Mafuta vyenye chapa ya Total.

Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp alisema Total inalenga kumfikia kila Mtanzania na kuwapatia nafasi ya kufuruhia huduma na bidhaa nzuri kutoka Total. Pia tunawaalika wafanya biashara ambao wangependa kupanua biashara zao kuungana nasi kupitia mpango wetu wa DODO na kupata nafasi ya kumiliki kituo cha huduma ya mafuta na kuweza kupanua na kuimarisha biashara zao.

Aliongeza kuwa; Leo, tunafurahia kuingia katika ubia wa kibiashara na Mhandisi Frank Malle ambae ni mmiliki wa kampuni ya F.S Mshuwa Co na mmiliki wa kituo hichi. Kwa ushirikiano huu tunatarajia kuihudumia Goba na jamii inayoishi maeneo ya jirani. Pia ningependa kutumia fursa hii kuwaalika wafanya biashara ambao wangependa kupanua biashara zao kuungana nasi kupitia mpango wetu wa DODO na kupata nafasi ya kumiliki kituo cha huduma ya mafuta na kuweza kupanua na kuimarisha biashara zao.

Kwa upande wake, mmiliki wa kituo hicho, Frank Malle, ameishukuru Total sio tuu kwa kuwawezesha kumiliki kituo hicho, bali pia kuwaokoa wasiuze ardhi yao, maana walishawishiwa sana kuuza ardhi, lakini Total ikawakomboa, sasa na wao ni wamiliki wa kituo cha kisasa cha mafuta cha Total.

Paskali
View attachment 1556125View attachment 1556126View attachment 1556127View attachment 1556128View attachment 1556129View attachment 1556130View attachment 1556131View attachment 1556132View attachment 1556270
Bado kampuni za sukari na cement kumpongeza kwa bei kupanda kila mwaka
 
mayalla! mayalla! mayalla!
nimekuita mara ngapi mayalla!!?
hata ukipewa ka kazi kadogo dogo hivi serikali,
bado hautafanikiwa,
kujipendekeza kumezid
 
mayalla! mayalla! mayalla!
nimekuita mara ngapi mayalla!!?
hata ukipewa ka kazi kadogo dogo hivi serikali,
bado hautafanikiwa,
kujipendekeza kumezid
Mimi ningefurahi awamu ya NNE ilikaribisha FDI ( uwekezaji toka nje ni kiasi gani), na awmu ya 5 imekaribisha kiasi kwa muda ule ule. Mfano JK alikuta GDP ya Kila mtanzania ni $540 akaipandisha hadi $980 na JPM ameupandisha hadi $1130 . Kwa hiyo JK ametufikisha karibu na uchumi Wa kati kuliko JPM . Lakini mabingwa Wa kujikomba mbona mnaogopa namba.? Na namba hazidangayi
, ukizijua propaganda za walamba viatu unazidharau. Shikamoo takwimu, ndio maana madictator hawzipendi maana zinatoa ukweli unaowaumbua. Wenye Kazi za boot lickers mniwie radhi ,so Mimi ni takwimu.
 
Nina mashaka na hawa mabeberu.Pamoja na kwamba mabeberu huwa sio wachoyo kufanya nao biashara pamoja ila Ukiona mbwembwe zimezidi jua ndo wanaondoka hivyo.ila wanaondoka kijanja hawataki shida badae.siku tukija kushtuka watakua washasepa kitambo.Ngoja tusubiri muda ufike utatupa majibu sahihi.
 
Na hii je
IMG-20200902-WA0002.jpg
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom