Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania yampongeza Rais Magufuli na kuipongeza Tanzania, kujenga mazingira bora ya biashara ya Mafuta, Uwekezaji

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Wanabodi,

Kampuni ya Mafuta ya Total, imempongeza Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na serikali yake ya awamu ya tano, kwa kujenga mazingira wezeshi ya biashara, na uwekezaji, yanayovutia wawekezaji wa kimataifa kuleta mitaji ya uwekezaji nchini na kuwawezesha Watanzania kupatiwa fursa za kuingia katika biashara za ubia za vituo vya mafuta vya kiwango cha kimataifa.

Pongezi hizo zimetolewa leo, na Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta cha Total, Total Mchigani, kilichopo Goba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kinachomilikiwa na Mtanzania mzawa. Kituo hicho kiko kwenye moja ya barabara yenye shughuli nyingi za kiuchumi jijini Dar es salaam inayotokea Mbezi Beach hadi Mbezi Kimara hivyo kulenga kuwahudumia wakaazi wa Tegeta, Mbezi Beach na Kimara pamoja na watumiaji wote wa barabara hiyo.

“Napenda kutumia nafasi hii, kumshukuru Rais wa Tanzania, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwezesha ukuaji wa kibiashara kwenye sekta ya nishati. Pia tunatambua kuwa uzinduzi huu usingewezekana pasingekuwa na baraka za serikali ambayo waliidhinisha leseni za kuendesha kituo hiki na kwa hilo shukrani zangu za dhati zinaenda kwa EWURA na pamoja na taasisi zingine za kiserikali zilizowezesha jambo hili kufanikiwa” Alisema Bw. Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp

Bwana Jean Franchois ameongeza kuwa Total Tanzania imekuwa ikihimiza wamiliki wa biashara kukuza biashara zao kwa kuingia ubia wa kibiashara na kampuni hiyo kwa njia ya DODO ambayo itawawezesha kumiliki na kuendesha vituo vya mafuta vyenye chapa ya Total. DODO ni mfumo wa kibiashara ambao kampuni ya hiyo hutumia kuweza kuongeza mtandao wa vituo vyake nchini. Mfumo huu unawawezesha wafanyabiahsara kuingia kwenye ubia na kampuni ya Total na kuweza kumiliki, kuendesha Pamoja na kusimamia vituo vya huduma vya Mafuta vyenye chapa ya Total.

Mkurugenzi Mtendaji wa Total Tanzania Bw. Jean Franchois Schoepp alisema Total inalenga kumfikia kila Mtanzania na kuwapatia nafasi ya kufuruhia huduma na bidhaa nzuri kutoka Total. Pia tunawaalika wafanya biashara ambao wangependa kupanua biashara zao kuungana nasi kupitia mpango wetu wa DODO na kupata nafasi ya kumiliki kituo cha huduma ya mafuta na kuweza kupanua na kuimarisha biashara zao.

Aliongeza kuwa; Leo, tunafurahia kuingia katika ubia wa kibiashara na Mhandisi Frank Malle ambae ni mmiliki wa kampuni ya F.S Mshuwa Co na mmiliki wa kituo hichi. Kwa ushirikiano huu tunatarajia kuihudumia Goba na jamii inayoishi maeneo ya jirani. Pia ningependa kutumia fursa hii kuwaalika wafanya biashara ambao wangependa kupanua biashara zao kuungana nasi kupitia mpango wetu wa DODO na kupata nafasi ya kumiliki kituo cha huduma ya mafuta na kuweza kupanua na kuimarisha biashara zao.

Kwa upande wake, mmiliki wa kituo hicho, Frank Malle, ameishukuru Total sio tuu kwa kuwawezesha kumiliki kituo hicho, bali pia kuwaokoa wasiuze ardhi yao, maana walishawishiwa sana kuuza ardhi, lakini Total ikawakomboa, sasa na wao ni wamiliki wa kituo cha kisasa cha mafuta cha Total.

Paskali

Total Mchingani Service Station Launch-Photo 1.jpg
Total Mchingani Service Station Launch-Photo 2.jpg
Total Mchingani Service Station Launch-Photo 3.jpg
Total Mchingani Service Station Launch-Photo 4.jpg
Total Mchingani Service Station Launch-Photo 5.jpg
Total Mchingani Service Station Launch-Photo 6.jpg
Total Mchingani Service Station Launch-Photo 7.jpg
Total Mchingani Service Station Launch-Photo 8.jpg..jpg
20200902_110200.jpg
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,141
2,000
Hakika akutukanae hakuchagulii tusi!!

Hakuna Mwekezaji kutoka Oil and Gas Industry anayeweza kumpongeza Magufuli!

Anampongeza vipi kiongozi anayetaka kutumia serikali yake kuanzisha biashara ya mafuta ili hatimae wawe competitor wao huku wakifahamu fika hatimae magari ya serikali yataambiwa yawe yanajaza mafuta kwenye vituo vya mafuta vya "serikali" kama walivyoanmbiwa watuimishi kutumia TTCL?

Watampongeza vipi kiongozi ambae anakwamisha mchakato wa gas processing plant kule Lindi huku akitangaza hadharani kwamba gas yote ya Kusini imeshauzwa kwa njia za rushwa wakati ni UONGO?

Wazungu wabaya sana! wanapenda sana kutumia kauli kwamba "Tusi zuri kwa mjinga ni kumsifia kwamba hakuna genius kama yeye duniani kote"!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom