Kampuni ya mafuta ya Total imewaondoa maelfu ya wafanyakazi wake Msumbiji

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Wanamgambo walisambaza vijikaratasi vinavyotishia kushambulia eneo la Palma.

Kampuni ya mafuta ya Total imewaondoa maelfu ya wafanyakazi wakekatika visima vya mafuta vilivyopo kaskazini mwa Msumbiji baada ya wanamgambo walio watiifu kwa kundi la Islamic State kutishia kushambulia mji muhimu katika eneo hilo.

Vyombo vya habari vinasema kwamba Wanamgambo hao walisambaza vijikaratasi vinavyotishia kushambulia eneo la Palma katika mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Cabo Delgado.

Tishio hilo lilisababisha Total kuwaondoa wafanyakazi wake katika eneo la Afunsi karibu na Palma ambapo linaongoza ujenzi wa kiwanda cha gesi chenye thamani ya $14.9bn.

Mtandao wa Carta de Mocambique umesema kwamba wapiganaji hao walikabiliana na vikosi vya serikalikaribu na palma tarehe mosi Januari.

Mkoa wa Cabo Delgado , ambapo ni nyumbani kwa rais Fillipe Nyusi , unapakana na Tanzania na umekumbwa na ghasia mbaya zilizotekelezwa na wapiganaji hao tangu 2017.
 
Hao total ndio wenyewe sasa wenye hilo kundi

Nadhani sasa wataanza kuchota gas maelfu kwa maelfu ya tani ndio baadae sasa watajifanya hali imetulia.
 
Hao total ndio wenyewe sasa wenye hilo kundi,

Nadhani sasa wataanza kuchota gas maelfu kwa maelfu ya tani ndio baadae sasa watajifanya hali imetulia
Alafu ikawaje wakapunguza wafanyakazi? Ingekuwa ni kweli, basi wangeongeza wafanyakazi sababu shughuli za kuchota gas kama unavyosema zingeongezeka na sio kupungua.
 
Hao total ndio wenyewe sasa wenye hilo kundi,

Nadhani sasa wataanza kuchota gas maelfu kwa maelfu ya tani ndio baadae sasa watajifanya hali imetulia
Kama ndio hivyo mbona wanaondoa wafanyakazi?

Hizo tani za gas watachotaje kama wanaondoa wafanyakazi?
 
Kama ndio hivyo mbona wanaondoa wafanyakazi?

Hizo tani za gas watachotaje kama wanaondoa wafanyakazi?
Mkuu, wanapoondoa wafanyakazi ni kutoa nafasi kwa hiyo kampuni kuingiza meli na kuchota gas watakavyo.
 
Alafu ikawaje wakapunguza wafanyakazi? Ingekuwa ni kweli, basi wangeongeza wafanyakazi sababu shughuli za kuchota gas kama unavyosema zingeongezeka na sio kupungua
We unafikiri hapo shughuli za kuchota gas zimepungua? Kwani wanachota na ndoo kama unachota maji kwenye kisima?

Hapo mitambo ilishategwa na sasa meli zitaanza kuingia hapo kuchota gas, na kwa kuwa wameigiza kwamba kuna tishio la usalama hakuna mtu atashtukia.

Yani kabisa kampuni ya kibeberu iache mali za mabilioni kisa kitisho cha kundi la uasi?
 
Tuanze mchakato wa gas haraka iwezekanavyo. Ingawa Angola, Total na Exxon walikuwa wanachimba mafuta na Unita wakiwepo.
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom