Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,888
Wananchi wapigwa risasi, walawitiwa na walinzi
*Mwekezaji ajinasibu ni rafiki wa Rais Kikwete
*Wananchi sasa waja juu, wataka tamko la Rais
Na Mwandishi Wetu, Korogwe
MIGOGORO kati ya wawekezaji kwenye sekta ya madini na wachimbaji wadogo wadogo wiki hii imechukua sura ya kutisha zaidi baada ya kubainika kuwa wananchi wapatao 20 wa kijiji cha Kalalani na Kigwase Kata ya Mashewa wilayani Korogwe wamefanyiwa vitendo vya kikatili na kinyama ikiwemo kulawitiwa na walinzi wa kampuni ya Amazon Trading Co. (T) Ltd.
Wakati wananchi hao wakikumbana na unyama huo, Majira Jumapili lilipotembelea eneo hilo jana limeelezwa kuwa katikati ya mateso na unyama huo, licha ya baadhi yao pia kupigwa risasi, wamekuwa wakikerwa zaidi na majigambo ya mmiliki wa mgodi huo anayejinasibu kuwa ni rafiki wa karibu wa Rais Jakaya Kikwete na kwamba hakuna mtu anayeweza kumsumbua.
Baadhi ya wananchi wakiwa na risasi miilini wamelazimika kukimbilia kwa waganga wa jadi kupata tiba wakiogopa kwenda hospitali ambako wanahofu watakamatwa na polisi waliokuwa wakiendesha msako.
Vita ya raslimali
Chanzo cha tafrani hiyo imeelezwa kuwa ni kitendo cha wananchi hao kukosa maeneo ya kujipatia riziki yao kufuatia eneo la madini kupewa mwekezaji huyo na hivyo wengi wao kulazimika kuingia katika baadhi ya maeneo yanayomilikiwa na mwekezaji huyo na kuchimba madini.
Katika kukabiliana na uvamizi huo imeelezwa kuwa mwekezaji huyo amejenga 'mahabusu' ndani ya mgodi huo ambapo wananchi mbalimbali wanapokamatwa huwekwa humo na ndipo mkasa wa unyama wa kulawitiwa unapojitokeza.
'Kambi ya mateso'
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa zaidi ya wanakijijini 15 waliowahi kushikiliwa katika 'mahabusu' ya mgodi huo walilawitiwa na baadhi ya walinzi wa mgodi huo kabla ya kuachiwa huru na wengi wameshindwa kueleza unyama huo wakiona aibu.
Mmoja wa wafugaji wa kijijini hapo ambaye ni mmasai, Bw. Maziwa Telikia alisema kuwa wamiliki wa mgodi huo pindi wanapowakamata wachimbaji wadogo wanaoingia kwenye maeneo yao huwafungia katika 'mahabusu' yao na kuwasimamia walizni wao wakiwalawiti raia.
"Kuna mwenzetu mmoja wa Kimasai ana umri wa miaka 70, alikuwa akichunga ng'ombe wake, akakamatwa na kupelekwa mahabusu, akalawitiwa na hivi sasa anatokwa na damu kila anapokaa,'' alisema mkazi mwingine Bw. Oloronyo.
Mkazi wa kijijini hapo Bw. Mohamed Saidi (30) akizungumza mbele ya Katibu wa CCM tawi la Kigwase, Bw. David Swai alionesha jeraha la risasi na kueleza kuwa amekuwa akiishi na maumivu makali kutokana na kuogopa kwenda hospitali kwa kuwahofia polisi.
Akisimulia mkasa huo alisema Aprili 12 mwaka huu akiwa anafua nguo mtoni alisikia watu wanakimbizana na askari wa FFU wakiwa na mgambo wa kampuni hiyo ya Amazon, alipohoji kulikoni alistukia anapigwa risasi kwenye makalio na kutishwa na askari hao asiende hospitali kwani watamfungulia kesi ya wizi wa madini.
'Rais, ni sisi au mwekezaji?'
Wanakijiji hao wakionesha kukerwa na ukatili huo na pia majigambo ya mwekezaji wa mgodi huo, sasa wanamtaka Rais Kikwete atoe tamko iwapo ni kweli yeye ndiye anampa nguvu mwekezaji huyo na wakasema wanaamini kuwa walimchagua Rais Kikwete ili awaletee maisha bora na si ukatili unaofanywa na watu wanaodai kuwa ni marafiki zake.
Mwenyekiti wa kijiji cha Kilalani, Bw Agustino Yustino Hassani alisema wananchi waliopigwa risasi wanazidi 20 na wengine inadaiwa wamefia porini na kuzikwa kwa siri na ndugu zao kwa kuogopa kutoa taarifa polisi.
Polisi: tunachunguza
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Bw Simoni Sirro amethibitisha kuwepo tafrani eneo hilo ambapo alisema kuwa ilianza wiki iliyopita kwa kuwahusisha ambapo askari wa FFU walilazimika kuingilia kati kuwatawannya wananchi waliokuwa wakipambana na walinzi wa mgodi.
Huku akionya kuwa uchunguzi utakapokamilika kuhusu tukio hilo askari au walinzi waliohusika watachukuliwa hatua, aliwataka wananchi nao waache kuvamia mgodi huo na kuwakaripia wamiliki wa mgodi kwa 'kujenga mahabusu.'
"Hakuna kampuni inayoruhusiwa kuwa na mahabusu yake hakuna kampuni inayoruhusiwa kuwalawiti wahalifu hata kama wamewakosea, inayotoa hukumu ni mahakama pekee, naomba wananchi wanipe ushirikiano tukomeshe vitendo hivi na wao kama wanavamia migodi ya watu waache tukibaini watafikishwa mahakamani," alisema Bw. Sirro.
DC:Ndio nasikia, ngoja nifuatilie
Akizungumza kwa simu na gazeti hili jana Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Bi. Betty Mkwasa amesema hakuwa na taarifa na tukio hilo na kuahidi kulifuatilia.
"Nimekuwa naangalia matukio ya polisi hapa sijaliona tukio hilo.Nashukuru kunijulisha, ngoja sasa nifuatilie," alisema.
Mmoja wa maofisa wa mgodi huo aliyekataa kuwekwa bayana gazetini alidai wanakijiji hao wamekuwa na tabia ya kuvamia mgodi huo mara kwa mara hali ambayo aliwalazimu kutoa taarifa polisi kwa msada zaidi.
Tangu kampuni ya Amazon iuchukue mgodi huo wa madini ya ruby na saphire mwaka 2005 kutoka kampuni ya AAPS iliyokuwa ikiumiliki mgodi huo tangu mwaka 1988, kumekuwepo na migogoro ya mara kwa mara kati ya uongozi wa mgodi huo na wananchi.