Kampuni ya Madini ya Tanzanite One yakubali kulipa fidia, Kodi na tozo nyingine zote inazodaiwa na Serikali

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Kampuni ya madini ya Tanzanite One imekubali kuilipa Serikali fidia pamoja na kodi watakayokubaliana kutokana na dosari zilizojitokeza hapo awali na kuiletea Serikali hasara

Pia imekubali kulipa tozo nyingize zote inazodaiwa na Serikali

Makubaliano hayo yametiwa saini na Mwenyekiti wa Kamati ya Madini iliyoundwa na Rais Magufuli, Prof. Palamagamba Kabudi na Mkurugenzi wa Tanzanite One Faisal Juma
IMG-20180516-WA0020.jpg
IMG-20180516-WA0019.jpg
 
Awamu hii si ya kuiamini(siasa nyingi kuliko mafanikio).

Wanayokubaliana na wanayotangaza (kutekelezwa) ni vitu viwili tofauti kabisa.

Tutawapima kwa utekelezaji na sio kwa hizi press release.

Details za mazungumzo na makubaliano yao ni siri yao(hii ni taarifa ya jumla tu).

Ni hawa hawa walitutangazi kuwa mgogoro wa kiwanda cha Dangote umekiwaisha na picha za pamoja wakapiga ila leo hii jiulize ni nini kinaendelea katika hicho kiwanda.

Wanapokuja public kutoa mrejesho mara nyingi huwa wako kisiasa zaidi.

Nilitarajia katika Bunge hili kuona mabadiliko ya sheria yanafanyika hata kwa hati ya dharura kumuwezesha CAG akague migodi ila sijui kama hili litafanyika.
 
Mwanzo mzuri
Nchi hii imechezewa sana

Wananchi endeleeni kutuombea na kutuunga mkono
Tunafanya haya kwa manufaa ya Wananchi wote
 
Awamu hii si ya kuiamini(siasa nyingi kuliko mafanikio).

Wanayokubaliana na wanayotangaza (kutekelezwa) ni vitu viwili tofauti kabisa.

Tutawapima kwa utekelezaji na sio kwa hizi press release.
Hii taarifa mimi naiamini 100% kwa sababu haijataja ni fedha kiasi gani watalipa, hata wakitupa buku hakuna wa kuhoji maana watakuwa wamelipa.
 
Aaah..... hiyo kampuni hata isipo lipa poa tu mbona zikikusanywa hatuoni zinatumikaje, mbaya zaidi matumizi yake yanapagwa na mtu mmoja tu ambaye ni malaika Jiwe, aka mzee wa (T 1.5)
 
Wangetaja kiasi ili tujue tunapata tena noah kila mtanzania au kwenye Tanzanite ni bajaj
 
Back
Top Bottom