Kampuni ya kutengeneza umeme bila kuzima kuwavuta wawekezaji bongo

racso kaunda

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
209
500
Kampuni ya Afrique Live Power Line Maintenance imefungua njia ya kuwavitia wawekezaji wa Nje kuja kuwekeza nchini kutokana na uwezo wa kutengeneza umeme bila kuzima. Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Donald Mwakamele amesema, kampuni hiyo inaweza kufanya matengenezo kama ukarabati huku umeme ukiwa unapita.

Kampuni hiyo inaweza kutengeneza umeme ukiwa laivu wenye voltage kubwa, 220000 ambao ni ule wa Kidatu mpaka wa chini kabisa. "Unajua katika kipindi hiki cha awamu ya tano, mheshimiwa Rais Magufuli anasimamia hoja ya uchumi wa viwanda. Na viwanda ni umeme, sasa sisi live line kazi yetu ni kufanya matengenezo huku umeme unapita, yaani hatuzimi umeme," alisema Mwakamele.

Hii ina maana kuwa, wakati umeme unakarabatiwa, mitaani na viwandani kunakuwa hakuna katizo la umeme, viwanda vinaendelea kuzalisha na Huduma hiyo mtaani inaendelea kupatikana. Kigezo kikubwa cha wawekezaji kwenda kuwekeza katika nchi yoyote ni upatikanaji wa umeme wa uhakika bila kukatikakatika kitu kinachofanywa na Afrique Live Line Maintenance. Wakati huohuo, Mwakamele amesema kuwa, tayari kampuni yake imefundisha waandisi 40 wanawake kama mkakati wake wa kueneza teknolojia hiyo nchi nzima. Mafunzo hayo yamefanyika kwenye Chuo cha kampuni hiyo kilichopo Wilaya ya Mvomero, Morogoro njia kuu ya kwenda Dodoma.
 

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
5,180
2,000
Asilimia kubwa ya umeme wetu kukatika katika ni kutokana na miundo mbinu ya usambazaji kuwa chakavu, hivyo mala nyingi ni KUBUTUKA!!! kwa transfoma, hapo itasaidiaje,? Labda kwenye maintenance hapo sawa ndio, huku kwetu kila wiki transfoma linabutuka, wanakuja wana shika shika tu, tayari baada ya wiki tena vile vile!! Au mimi ndio sielewi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom