Kampuni ya kuhudumia shughuri mbali mbali ofisini imeanzishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni ya kuhudumia shughuri mbali mbali ofisini imeanzishwa

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Akiri, Sep 19, 2012.

 1. A

  Akiri JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,453
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Havilla Express Delivery

  ni kampuni inayokusaidia katika kutekeleza majukumu yako ya kila siku ofisin au nyumbani .
  tunafanya shughuri zifuatazo
  • kuchukua/kupeleka barua kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya jiji
  • kulipa bill mbali mbali umeme , maji nk
  • kufanya usafi wa ofisi yako
  • kuchukua taka zilizopo ofisini kwako
  • kupanga mafairi au vitabu ktk makabati yako hapo ofisini
  • kusambaza vipeperushi vya ofisi yako
  • kumpeleka/kumchukua mwanao shule au sehemu ya michezo
  • kumpokea mgeni uwanja wa ndege au ubungo
  • kupeleka /kuchukua mzigo dhl etc
  • kuchukua form za maombi ya passport au viza
  • kuweka booking
  • kuchukua chakula nyumbani kwako na kukuletea ofisin, shule nk

  lengo letu ni kufanya kazi pamoja na mtu au taasisi ambayo ina shughuri nyingi ili wao waendelee kufanya kazi ofisini na sisi tuwafanyie za nje ambazo wangelazimika kuancha kazi na kwenda kuzifanya tunafanya kwa gharama nafuu
  sana.

  kwa maelezo zaidi nipigie 0755 099 291 au 0657 14 5555 Akiri
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,128
  Trophy Points: 280
  Mkuu Hongera sana Kwa Ujasiriamali, ni kupongeze kwa Hilo, Ila Mkuu pamoja na Pongezi ninilikuwa na Maoini machache kuhusu sehemu nilizo Weka Red,

  1. Mkuu ulifanya Tafiti za kutosha kabla ya Kuja na haya Mawazo yako? Make hapo kwenye Red Kuna Utata mwingi sana

  - Kuchukua Bararua na kupeleka- Kwa sasa kampuni nyingi sana zinatumia email mkuu na si Hady copy tena,

  - Bili za Umeme na Maji kwa sasa zinalipwa kupitia Mitandao ya Simu na Kwenye Mabenk,

  - Ishu ya TAKA kuna kampuni maalumu za kuzoa taka na kila Offisi ni lazima ilipie bili ya Kuzoa taka hata kama itakuwa haina taka ila malipo ni lazima, sasa sijajua kampuni yako itakuwa na gari kubwa la kuzoa au vipi

  - Kupanga mafaili na Vitabu Offisini- Hii ishu ni ngumu kwa sababu Mafaili ya Offisi yoyote yana watu maalumu wa Kuyatunza na hata wafanya kazi wengine wa hiyo offisi hawaruhusiwi kuya gusa na huwa ni ishu za Siri sana ambazo offisi isingependa watu wengine wajue

  - Kupeleka Mtotoa na kumchukua kutoka shule- Shule Nyingi sana English Medium zina Magari ya kubeba watoto, au unazungumzia watoto wanao soma ST GOVERNMENT?

  - kupkea Mgeni Uwanja wa Ndege au Ubungo- Hapa inategemeana ni Mgeni wa aina gani make kama ni wa Familia mara nyingi wanafahamu nyumbani na wanaweza fika bila tatizo,

  - Mizigo DHL- Ni juavyo mimi kazi ya kumfikishia mteja mzigo wake hufanywa na DHL na sheria zao ni lazima Mfanya kazi wa DHL afikishe mzigo kwenye Offisi husika na wasaini, huwa hawatumii third party

  - Mkuu mambo ya Pasport na VISA ni ishu muhimu sana na mara nyingi huenda mhusika mwenyewe na si Ajent, kwanza hawafanyi kazi na Ma ajent

  - Kwenye Msosi hapo napo sijaelewa mtakuwa mnachukua vipi


  Kwa kifupi jaribuni kufanya Tafiti za kina kujua hizo kazi zinawezekana au haziwezekani
   
 3. CONSULT

  CONSULT JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Hongera sana Akiri, hizo kazi zinawezekana sana na soko lake ni pana sana hasa kwa dar, hakuna kazi isiyo na changamoto na kwa kazi kama hizi zenye ushindani zaweza kuwa za kudumu na zenye tija ilimradi uwe mikakati mizuri, udhamirie kwa muda mrefu, tambua kuwa mjasiliamari huona fursa lakini asiye mjasiliamari huambulia kuona changamoto, vikwazo tu.... natamani hata mimi tuwasiliane nadhani pana huduma utanisaidia ...
   
 4. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,879
  Trophy Points: 280
  Ni mawazo mazuri. Nashauri vijana wako utakaowapa ajira wawe ni wale unaowaamini wasije wakaingia mitini na mzigo wa mtu wakakuharibia jina la kampuni. Pamoja na mchangiaji mmoja kusema kuwa kuna service kama hizo zinazofanyika tayari, huu ni wakati wa ushindani wa biashara.
   
 5. O

  Orche Senior Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mungu akubariki sana kwa ujasiriamali wako. Hizo kazi zipo na zinawezekana kaza buti utafanikiwa, kutokana na juhudi na maarifa.
   
 6. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Hahaaa, kaka huyu jamaa yuko kwenye njia sahihi kabisa, aweke bidii na mafanikio yataonekana. Mimi nadhani wewe ndy haujafanya utafiti wa kutosha. Kaka Akiri ongezea huduma za kufua nguo.
   
 7. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Ongeza na huduma ya shoe shine. Pita kw maofisi, ongea na watu, chukua viatu vyao, viweke mkao, warudishie hukohuko. Hii nimeona Nairobi mkuu
   
 8. A

  Akiri JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,453
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Asante sana ndugu yangu , ni kweli zipo kampuni kubwa ambazo zinafanya shughuri ambazo sisi tunafanya lakini pia zipo kampuni ndogo ambazo ambazo hazihitaji au labda wanapenda kufanya kazi na sisi kwa sababu ambazo wao wanazijua.
  tangu tuanzishe huu ni mwaka wa 2 . na tayari tuna kampuni kama 3 tunafanya nazo kazi na watu binafsi zaidi ya 15 ambao wanatumia huduma zetu. kama nilivyosema lengo ni kukufanya wewe uliyekaa ofisini na pengine unataka kutuma mzigo kwenye basi sasa badala ya kuondoka ofisini unaweza tuita nasi tukaupeleka na kisha kukuletea risiti na utajikuta kazi ya ofisini kwako imefanyika na pia mambo yako binafsi yamefanyika.
  mfano kuna bwana mmoja anafanya kazi pale Ami hospital masaki na yeye anaishi mbezi jagwani beach mtoto wake anasoma mbezi tanki bovu ana umri wa miaka 2.5 anakwenda shule mara 3 kwa wk . asubuhi mzazi anampeleka shule saa sita anatakiwa aje amchukua sasa tumekubaliana saa tano mimi huwa naenda ofisini kwake nachukua gari yake naenda shule kwa mtoto ( tayari nilitambulishwa kwa waalimu na tukasaini mkataba) namchukua mtoto na kumpeleka nyumbani kisha narudisha gari ofisini kwa malipo ya Tsh 6000/= na pia kama wanasafiri huwa nawachukua na gari yao mpaka airport kisha narejesha gari nyumbani.
  niliwahi kuanjiriwa katika ngo ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 10 kama office attendant hivyo baada ya mkataba kuisha sikutaka kwenda kuomba kazi sehemu nyingine nikaona ni vema niendeleze zile kazi katika namna nyingine. namevutiwa na maoni yako karibu tena na usiongope kufanya kazi na sisi kama kutakuwa na mapungufu tutakuwa tayari kukosolewa
   
Loading...