Kampuni ya kichina matatani kwa kutengeneza vibao vya namba za magari kinyume cha sheria

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,734

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya msako wa kushtukiza katika kampuni ya Tanzania China Trade and Tourism Development Ltd iliyoko Barabara ya Nyerere Dar es salaam baada ya kupata taarifa kutoka kwa msamaria mwema na kukamata vifaa pamoja na malighafi za kutengeneza na kutoa vibao vya namba za pikipiki kinyume na sheria.

Katika msako huo uliofanyika tarehe 19 Februari 2016 katika kampuni hiyo, Maofisa wa TRA waliweza kukamata na kutaifisha vibao vyenye namba za pikipiki 2,500 na vibao 5,600 ambavyo havikuwa na namba. Pia maofisa wa TRA walikamata malighafi za rangi ya vibao katoni tatu, pamoja na mashine ya kupaka vibao rangi yenye uzito wa kilo 155.

Mashine nyingine iliyokamatwa katika msako huo ni ya kutengeneza namba za magari yenye uzito wa kilo 902 ambayo imezuiwa isihamishwe kutoka katika kampuni hiyo pamoja na kompyuta mpakato ambayo imepelekwa katika maabara ya uchunguzi TRA kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Taarifa za kuwepo kwa utengenezaji wa vibao vya magari kinyume na taratibu na sheria zilitolewa na msamaria mwema ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni husika Donglinh Guo, Meneja wa Kiwanda Yong Qing Cheng na Meneja wa ghala Peng Zhan walikamatwa baada ya kutokea fujo wakati wa msako na kufikishwa katika kituo cha Polisi Changombe.

Kampuni ya Tanzania China Trade and Tourism Development LTd ndio waingizaji pekee wa pikipiki za Falcon tangu mwaka 2008 ambapo inatuhumiwa kutoa vibao vya namba za pikipiki kwa wateja wake kwa shilingi 5,000 kinyume na sheria.Uchunguzi wa thamani ya kodi iliyopotea bado unaendelea.

Vibao vya magari na pikipiki hutolewa na kampuni ambazo zinatambuliwa na TRA baada ya kupewa idhini. Kampuni hizo ni Masasi Sign, Auto Zone, Sign Industry, Kiboko, Budda Auto works, Parkinson Ltd na Next Telecom.
Ili kujiridhisha kuwa kadi za pikipiki zinazotolewa kwa wateja wa kampuni hiyo ni halali, TRA ilifanya uchunguzi na kugundua kuwa kadi hizo zinatolewa kihalali.

TRA inawatahadharisha wananchi kufuata taratibu na sheria ili kuepuka usumbufu unaoweza kutokea endapo watagundulika kujihusisha na vitendo ambavyo ni kinyume na sheria.
 
Mkuu kibogo sijaelewa hapo kwenye aya ya pili yenye "red",kwamba TRA imejiridhisha kuwa utolewaji wa namba hizo ni halali au si halali??Kaka Lizaboni hawa Wachina CCM imewalea sana,mpaka inafikia wanapigana na maafisa wa Serikali,huku ni kukosa nidhamu na heshima kwa mamlaka ya nchi,hivi kweli mswahili anaweza fanya hivyo Uchina?
 
Binafsi huwa nakerwa sana na utitiri wa wachina hapa nchini. Wachina wanakuwa na nguvu sana kuliko wananchi wazalendo. Na hii inatokana na majipu yaliyopo uhamiaji ambao ndio wanawalea hawa wahamiaji. Ukifuatilia sana utagundua kuwa wengi hawana vibali vya kuishi nchini na hawana vibali vya kufanya kazi. Tutafika tu
 
Musfrica anazidi kudharaulika.. Hawa chalii wana dharau sana kwa nini?
Kama mnakumbuka yuke mtoto aliyekuwa wa piki anasema kuwa huko kwao china walifundishwa kuwa africa kuna miti tu na njaaa na watu wenye utapiamlo na picha wanaonyeshwa ila walipofika huku ndio akakuta mambo tofauti...
Inawezekana hawa wachina wanaambiwa kuwa hawa weusi ni mazuzu na mazezeta mnaweza kufanya lolote mnalotaka
 
KUNA WAKATI AKILI YAKO IKO VIZURI, KAMA SASA, SIPENDI MGENI YEYOTE ANAEFANYA MTANZANIA APATE SHIDA NCHINI KWAKE. WACHINA/WAGENI NA VIDILI VYAO BUBU WAONDOKE...
 
Binafsi huwa nakerwa sana na utitiri wa wachina hapa nchini. Wachina wanakuwa na nguvu sana kuliko wananchi wazalendo. Na hii inatokana na majipu yaliyopo uhamiaji ambao ndio wanawalea hawa wahamiaji. Ukifuatilia sana utagundua kuwa wengi hawana vibali vya kuishi nchini na hawana vibali vya kufanya kazi. Tutafika tu
Wachina wengi hawana vibali halali,Urafiki wa China na Serikali ya Tz ni moja ya sbb ya Wachina kujiona kama wana uhalali wa kuishi hapa Tz kuliko sisi raia,Urafiki wa CCM na Chama cha Kikomunisti cha Uchina imechochea ujio wa Wachina kwa kiasi kikubwa sana,Wakiwa wanakuja Tz huwa wanahakikishiwa "usalama" mkubwa kwa kuambiwa kuwa serikali iliyopo madarakani imesaidiwa sana na China hivyo ni wakati wa wao kula matunda ya "Urafiki wa China na Tz"
Wao wana historia ya reli ya TAZARA,wanausema uwanja wa Taifa,wanasema jengo la Mikutano la Mwalimu Nyerere,wanasema chuo cha UDOM na kampuni yao ya CRJ,barabara na miradi ya kujenga kambi za jeshi kama Gongo la Mboto,maghorofa ya JKT Kambi ya Maramba Tanga,maghorofa ya Jeshi Wami na miradi mingi wanayopewa na serikali.Hivi vinawapa kiburi sana.Pale kiwanda cha Urafiki kwenye zile ghorofa wanaishi wengi bila vibali
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya msako wa kushtukiza katika kampuni ya Tanzania China Trade and Tourism Development Ltd iliyoko Barabara ya Nyerere Dar es salaam baada ya kupata taarifa kutoka kwa msamaria mwema na kukamata vifaa pamoja na malighafi za kutengeneza na kutoa vibao vya namba za pikipiki kinyume na sheria.
Katika msako huo uliofanyika tarehe 19 Februari 2016 katika kampuni hiyo, Maofisa wa TRA waliweza kukamata na kutaifisha vibao vyenye namba za pikipiki 2,500 na vibao 5,600 ambavyo havikuwa na namba. Pia maofisa wa TRA walikamata malighafi za rangi ya vibao katoni tatu, pamoja na mashine ya kupaka vibao rangi yenye uzito wa kilo 155.
Mashine nyingine iliyokamatwa katika msako huo ni ya kutengeneza namba za magari yenye uzito wa kilo 902 ambayo imezuiwa isihamishwe kutoka katika kampuni hiyo pamoja na kompyuta mpakato ambayo imepelekwa katika maabara ya uchunguzi TRA kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Taarifa za kuwepo kwa utengenezaji wa vibao vya magari kinyume na taratibu na sheria zilitolewa na msamaria mwema ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni husika Donglinh Guo, Meneja wa Kiwanda Yong Qing Cheng na Meneja wa ghala Peng Zhan walikamatwa baada ya kutokea fujo wakati wa msako na kufikishwa katika kituo cha Polisi Changombe.
Kampuni ya Tanzania China Trade and Tourism Development LTd ndio waingizaji pekee wa pikipiki za Falcon tangu mwaka 2008 ambapo inatuhumiwa kutoa vibao vya namba za pikipiki kwa wateja wake kwa shilingi 5,000 kinyume na sheria.Uchunguzi wa thamani ya kodi iliyopotea bado unaendelea.
Vibao vya magari na pikipiki hutolewa na kampuni ambazo zinatambuliwa na TRA baada ya kupewa idhini. Kampuni hizo ni Masasi Sign, Auto Zone, Sign Industry, Kiboko, Budda Auto works, Parkinson Ltd na Next Telecom.
Ili kujiridhisha kuwa kadi za pikipiki zinazotolewa kwa wateja wa kampuni hiyo ni halali, TRA ilifanya uchunguzi na kugundua kuwa kadi hizo zinatolewa kihalali.
TRA inawatahadharisha wananchi kufuata taratibu na sheria ili kuepuka usumbufu unaoweza kutokea endapo watagundulika kujihusisha na vitendo ambavyo ni kinyume na sheria.
wachina wanastahili kutimuliwa

wengi ni wababaishaji kuliko wahindi
wanatengeneza kila kitu fake anzia dawa mpaka barabara
viwanda vyao vingi vinachafua mazingira na kuhatarisha afya zetu
wengi sana hawana vibali vya kuishi tz
wengi ndo wezi wa pembe za ndovu wanajitia wanauza maua visu na simu fake kk..kumbe wanapiga ramani za ndovu
wananyanyasa wafanyakazi na kuwapa mtonyo wa kimaandazi

wanazalisha kataifa kao ka wachina street kuna mitaa watoto wana macho madogo tuu hasa usawa wa uwanja wa taifa

timua faida zao ni ndogo kuliko hasara walizo nazo kwetu
 
Mkuu kibogo sijaelewa hapo kwenye aya ya pili yenye "red",kwamba TRA imejiridhisha kuwa utolewaji wa namba hizo ni halali au si halali??Kaka Lizaboni hawa Wachina CCM imewalea sana,mpaka inafikia wanapigana na maafisa wa Serikali,huku ni kukosa nidhamu na heshima kwa mamlaka ya nchi,hivi kweli mswahili anaweza fanya hivyo Uchina?
Tanzania itajengwa na Wachina hutaki muulize Mkwere atakwambia.

Hapa TZ hata nani aje hamgusi mchina hii nimeiona sehemu nyingi sana na aliyewapa kiburi ni nyienyie wazee wa 'mbele kwa mbeleeee'
Magu mwenyewe akileta fyokofyoko wanambomoa.

Poor TZ
 
Musfrica anazidi kudharaulika.. Hawa chalii wana dharau sana kwa nini?
Kama mnakumbuka yuke mtoto aliyekuwa wa piki anasema kuwa huko kwao china walifundishwa kuwa africa kuna miti tu na njaaa na watu wenye utapiamlo na picha wanaonyeshwa ila walipofika huku ndio akakuta mambo tofauti...
Inawezekana hawa wachina wanaambiwa kuwa hawa weusi ni mazuzu na mazezeta mnaweza kufanya lolote mnalotaka
Jibu hilo hapo
Naona na wafadhili wa kuu wa ccm wanakamatwa .....ila hao wako juu ya sheria wataachiwa tu
 
Binafsi huwa nakerwa sana na utitiri wa wachina hapa nchini. Wachina wanakuwa na nguvu sana kuliko wananchi wazalendo. Na hii inatokana na majipu yaliyopo uhamiaji ambao ndio wanawalea hawa wahamiaji. Ukifuatilia sana utagundua kuwa wengi hawana vibali vya kuishi nchini na hawana vibali vya kufanya kazi. Tutafika tu
Aliyewaleta akawakumbatia si huyo JK au kuna mwingine?
Wapo mitaani na wana nguvu haswa huwaambiwi hawasikii lolote.
Wanatuharibia mpaka vibiashara vyetu vya rejareja huku mitaani sijui mnataka nini nyie watawala weusi.
 
Wachina bwana,kibao ki moja cha Pikipiki ni 19000 wao wanatoa kwa 5000,vya gari ni 38000 wao wana toa kwa 10000,halafu quality Sanaa..wana nipa rahaa sanaaaa..
 
Balozi Mchina!.jpg
za Kichina!.jpg

Huyu jamaa alikuwa anajua? Na hao alio nao hapo jukwaani walikuwa wanajua? Tunaposema ufisadi ni mfumo ndiyo hiki ambacho huwa tunakimaanisha!!
 
Binafsi huwa nakerwa sana na utitiri wa wachina hapa nchini. Wachina wanakuwa na nguvu sana kuliko wananchi wazalendo. Na hii inatokana na majipu yaliyopo uhamiaji ambao ndio wanawalea hawa wahamiaji. Ukifuatilia sana utagundua kuwa wengi hawana vibali vya kuishi nchini na hawana vibali vya kufanya kazi. Tutafika tu

Ndugu chanzo cha haya yote yanayotokea ni kutokana na uhalisia kama unavyoonekana katika picha hizi hapa chini kwani waChina walihalalishwa na kuthaminiwa ndani ya nchi hii kuliko wazawa, na kama sikosei wewe lizaboni ulikuwa mstari wa mbele kushabikia suala hili la huyu balozi kuwa pamoja na viongozi wa CCM huku akiwa kavaa Kofia na skafu za CCM na kusimama katika majukwaa ya CCM hivyo JIPU hilo lililolelewa na CCM ni vigumu sana kulipasua kwani limeota mizizi hadi ndani ya mishipa ya fahamu ya CCM hivyo mkilipasua tu matokeo yake hayatakuwa mazuri.
balozi+px.jpg

balozi+wa+china-xxl.jpg

IMG_2913.JPG

BALOZIWACHINA.jpg
 
Back
Top Bottom