kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,991
- 17,887
Kampuni ya Israel yaiuzia Saudia teknolojia ya ujasusi
Jun 09, 2021 08:16 UTC
[https://media]
Shirika moja la ujasusi wa mitandaoni la utawala wa Kizayuni wa Israel limeuuzia utawala wa Aal-Saud wa Saudi Arabia teknoljia ya kisasa ya kufanya ujasusi na kudukua mawasiliano ya simu-erevu za rununu.
Hayo yameripotiwa na gazeti la Kizayuni la Haaretz ambalo limefichua kuwa, kampuni ya Quadream inayoongozwa na afisa wa zamani wa Idara ya Kijasusi ya Jeshi la Israel imeiuzia serikali ya Riyadh teknolojia hiyo kwa mamilioni ya fedha kwa miaka mingi sasa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyochapishwa jana Jumanne, Saudia inatumia teknolojia hiyo ya kijasusi ya kudukua kompyuta au simu za mkononi kuwafanyia ujasusi viongozi wa upinzani na wakosoaji wa Muhammad Bin Salman (MBS), Mrithi wa Ufalme wa Saudia.
Inaarifiwa kuwa, teknolojia hiyo inaweza kudukua mawasiliano ya simu za rununu hususan iPhones, inaweza kudhibiti kamera tokea mbali, kurekodi mazungumzo na kutambua sehemu aliko mtumiaji, pasi na mwenyewe kujua.
Kwa mujibu wa gazeti hilo la Kizayuni, Saudi Arabia, Bahrain na Imarati (UAE) zina mikataba mikubwa ya siri ya kununua vifaa vya kijasusi kutoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
[https://media]
Mwaka 2019, Saudi Arabia iliripotiwa kununua programu ya kufanya ujasusi yenye thamani ya dola milioni 300 kutoka utawala wa Kizayuni wa Israel.
Itakumbukwa kuwa, shirika moja la kijasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel lilitoa msaada mkubwa kwa ufalme Saudi Arabia ili kufanikisha mauaji ya mwandishi habari Jamal Khashoggi ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa ufalme huo wa kiimla.