Kampuni ya Geita Gold Mine yasalimu amri ya Magufuli, yaanza kugawa magangwala, wananchi wahofia

Udongo ni nchi.Hata kama ni waste wacha tubakia nao wenyewe.Kuliko wao kuusafirisha kuupeleka kwao.Tutautumia hata kufukia vifusi kwenye barabara zetu hata kama utakuwa hauna dhahabu.Cha msingi ubaki nchini kwetu hapo hapo maeneo yaliyoko machimbo.Tutautumia hata kufukia mashimo ya dhahabu waliyoaacha wazi baada ya uchimbaji.Tunautaka udongo wetu wa Magwangwala uwe na dhahabu au la.

Sasa povu la nini Mkuu. Walisafirisha kwasababu waliruhusiwa na serikali hiyohiyo iliyo chini ya chama kilichomteua Magufuli kuwa na nguvu ya kuja kuwazuia kusafirisha huo udongo. Wamekubali. It seems to be a win-win situation. Tuwapongeze kwa busara yao, tumpongeze pia Magufuli kwa busara yake ktk kuliweka hili sawa. Hakuna sababu ya kutoa kauli za kishabiki zenye mwelekeo wa kuwafanya wawekezaji waonekane kama wakoloni waliovamia nchi kwa nguvu.
 
Mkuu ebu ngoja nikupe Elimu kidogo....hawa wawekezaji wanapochimba dhahabu huwa wanatenganisha high grade ore na low grade ore...hyo low grade huwa Mara nyingine wanaichanganya na high grade na kuichenjua au wanaweza kuchenjua yenyewe kulingana na bei ya dhahabu wakati husika na wakapata faida..,kwa kifupi hyo low grade siyo waste...huwa inakuwa piled sehemu fulani kwenye mgodi..

Ninachoelewa mm ni kwamba wananchi wa Geita wanaitaka hyo lowa grade ore ambayo ndo wanaita magwangala...kama ulimsikia musukuma alisema mgodi wasiwape waste bali wawape magwangala yaani low grade ore...

Sasa je ni muwekezaji gani atakubali kutumia gharama yake kuchimba ore halafu aje aigawe bure kwa wananchi wakati anajua Kabisa kuwa akiiprocess atapata faida???

Ndo maana tunasema watakachopewa wananchi sio low grade ore (magwangala) bali ni waste..

Nn kifanyike....
Badala ya kuwadanganya wananchi na magwangala a.k.a waste rais ana nafasi Nzuri sana ya kuhakikisha wananchi wake wananufaika na madini katika sehemu walipo ambapo uchimbaji unaendelea...mikataba ipitiwe upya vile vipengele kandamizi vitolewe au virekebishwe...mrabaha uongezeke ile kodi ya halmashauri ambayo migodi huwa inatoa kwa halmashauri husika iongezwe...kiasi cha dhahabu kinachopatika kwa kila kampuni husika kijulikane na kiwe ndicho kiasi halisi na sio kile ambacho kampuni inaamua kiwasilisha serikalini....misamaha ya kodi ya kijinga kijinga ifutiliwe mbali..

Kwa sasa naomba niishie hapa
Nani kaniambia kiasi cha dhahabu kinachozalishwa na migodi hakijulikani? MDA zipo na kuzifanyia marekebisho kunahitaji majadiliano kati ya mwekezaji na serikali, siyo matamko laa sivyo tunaweza tukajikuta tuna liability kubwa endapo tutakiuka vipengele bila utaratibu, kwa taarifa yako kuna mabadiliko yamefanyika kwenye hizo mda lakini kuna mambo mengine zaidi yanahitaji mabadiliko
 
Umeandika maelezo marefu ambayo kwa mantiki unaonyesha kama umeona mkataba au ulishiriki katika kuweka signature ya mkataba.

Kama hujaona mkataba, kwa nini unadhani anachokifanya Rais magufuli ni kinyume cha mkataba.

Hoja yako itakuwa ina nguvu za hoja kama umeona huo mkataba au umeshiriki katika kuandika au kuweka signature ya mkataba. Kimyume chake utakuwa unatumia hisia tu ambazo zinaweza zikawa na ukweli au uwongo.

Kumbuka Rais Magufuli anayo hiyo mikataba kwenye kabati zake ofisini.
Mkuu wangu ni Wapi nimesema anachokifanya mh rais ni kinyume na mkataba???nilisema kwenye moja ya comments zangu kuwa rais anazonyenzo zote za kujua kama tunaibiwa kwenye madini (na kimsingi tunaibiwa kweli kutokana na mikataba mibovu tuliyoongia na wawekezaji) na rais ana uwezo wa kudhibiti huo wizi ikiwa ni pamoja na kupitia mikataba upya na kuondoa vipengele vya wizi wizi..

Ninachosema ni mnavoshangilia kuwa eti rais amefanya jambo la maana kuwalazimisha wawekezaji kuwapa wananchi magwangala ni upuuzi mtupu...hayo magwangala ni uchafu...hayatakuwa na dhahabu...zaidi ya yote wananchi watatumia mercury wakati wakijaribu kurecover dhahabu kwenye hayo magwangala ambayo ina madhara kiafya...

Rais hana sababu ya kulalamika kwenye majukwaa kuwa tunaibiwa kwa mchanga kusafirishwa kwenda nje...anachotakiwa kutuambia ni kwamba amepiga marufuku mchanga kwenda nje na sasa kila kitu kitafanyika hapa nchini kwa uwazi kabisa na hatutakuwa tena na wasiwasi kuwa tunaibiwa....cha kujiuliza hapo je ana uwezo huo???tekinolojia ya kuuchenjua huo mchanga na kupata hayo madini tunayo hapa nchini??? Kama haipo tuna uwezo wa kuileta???nani atagharamia kuileta???ukiwaambia wawekezaji wailete hyo tekinolojia wanakuambia ni gharama mno ni afadhali wasafirishe mchanga kwenda nje...

Rais kama anatupenda kweli asiwalazimishe wenye viwanda vya samaki watupe mapanki...awalazimishe watupe samaki..
 
Nani kaniambia kiasi cha dhahabu kinachozalishwa na migodi hakijulikani? MDA zipo na kuzifanyia marekebisho kunahitaji majadiliano kati ya mwekezaji na serikali, siyo matamko laa sivyo tunaweza tukajikuta tuna liability kubwa endapo tutakiuka vipengele bila utaratibu, kwa taarifa yako kuna mabadiliko yamefanyika kwenye hizo mda lakini kuna mambo mengine zaidi yanahitaji mabadiliko
Naona umekurupuka usingizini na kuanza kuandika bila hata kujua unaandika nn...kanawe uso kwanza kisha rudi..
 
]Nimekuuliza nani kaniambia serikali haijui kiasi cha dhahabu inayodhalishwa?

Sijakuelewa bado...
Nakunukuu "kiasi cha dhahabu kinachopatika kwa kila kampuni husika kijulikane na kiwe ndicho kiasi halisi na sio kile ambacho kampuni inaamua kiwasilisha serikalini....misamaha ya kodi ya kiasi cha dhahabu kinachopatika kwa kila kampuni husika kijulikane na kiwe ndicho kiasi halisi na sio kile ambacho kampuni inaamua kiwasilisha serikalini....misamaha ya kodi ya kijinga kijinga ifutiliwe mbali..
kijinga ifutiliwe mbali.."

Umesema kiasi cha dhahabu kinachozalishwa na kila kampuni kijulikane, ndo nakupa taarifa kuwa kila gram ya dhahabu inayodhalishwa na migodi mkubwa serikali inajua quantity na quality.....
 
Sawa endelea kujidanganya hvo..
 
Sawa endelea kujidanganya hvo..

MDA kuwa na matatizo nakubaliana na wewe 100% , lakini kuhusu kiasi kinachozalishwa hapo hapana. Labda utujulishe loop holes kama zipo....kwenye gold room , dispatch in case o mahali pengine. ...
 
Magufuli kiboko keshadhibiti ule mchanga (Magwangala) waliyokuwa wakisafirisha nje makotainer na mkontainer kupitia bandari ya Tanga kwa kisingizio kuwa ni magwangala ambayo hayana kitu wakati kumejaa dhahabu kibao wanaenda kuupepeta huo mchanga na nyungo za kizungu wanapata dhahabu.

Magufuli anadhibiti dhahabu hadi magwangala.Safi sana
Wewe huelewi hata unachozungumza. Magwangala na mchanga (concentrate), ni vitu viwili tofauti kabisa. Geita Gold Mine hawakuwa wanasafirisha mchanga. Mchanga (Cu-Ag concentrate) unasafirishwa na Acacia, na bado unasafirishwa.
 
No matter how we sugar coat it, hayo magwangala is just waste.No investor worth their salt atakubali tu kuwapa hayo mabaki without making sure kwamba what you are going to get out of it is little to none.

Kwasababu it doesn't make sense, yeye aje ainvest halafu eti tugawane udongo which supposedly una madini.Tutakuwa tunadanganyana tu.
Nafahamu kiundani kilichokuwa kikifanyika, na nadhani Rais hakuambiwa ukweli. Hakuna magwangala yenye dhahabu, asikudanganye mtu yeyote, ni uwongo mkubwa. Kilichokuwa kikifanyika ni kwa wafanyakazi wa kampuni wasio waaminifu, walikuwa wanachanganya waste (mawe yasiyo na chochote) na mawe yenye dhahabu (ore), wanaenda kuyamwaga yote kwa pamoja kwenye waste dump. Na ilikuwa ni syndicate ya wizi. Kwa sababu huo wizi umedhibitiwa nina uhakika hayo magwangala yatakakomwagwa yatabakia yametapakaa na kuleta athari za kimazingira. Baadaye tutaanza kuilaumu kampuni na huenda tukaja kuiomba iyaondoe.
 
Afadhali wananchi watanzania wawe scavengers kwenye huo udongo kuliko usafirishwe nje wazungu ndio wakawe ma scavengers kwenye huo mchanga ukimwagwa kwenye nchi zao baada ya kusafirishwa
Unachanganya mambo mawili, yote usiyoyajua vizuri. Magwangala siyo mchanga. Magwangala ni waste, na hilo linahusu Geita.

Mchanga ni Cu-Ag concentrate, unahusu mgodi wa Bulyanhulu wa Acacia, na bado concentrate inasafirishwa na hakuna namna yoyote ambayo mwananchi anaweza hata kuigusa achilia mbali kuichukua.
 
Sasa mbona unaaandika kama mtoto mdogo asiyekuwa na logic ya kawaida? Sasa wakati wanasaini hiyo Mikataba raisi Magufuli alikuwa na uwezo gani wa kuweza kubadilisha chochote kile? Kwanza hata Waziri Muhongo mwenyewe hakuwepo, Mikataba yote ilisainiwa na akina Yona, Ngeleja chini ya Mkapa, Kikwete, fisadi Lowasa, Sumaye &Co. lkn leo hii Mikataba imeshasainiwa sasa ulitaka tufanye nini kuhusu hiyo gangwala? Toa ushauri kwa leo ulitaka Raisi na Waziri muhusika wafanye nini?
acha kuongea pumba ww.kwani mikataba mikubwa waziri anapokwenda kusaini si ni lazima baraza la mawaziri lipitie na kumbuka toka kipindi cha mkapa mikataba hiyo iliposainiwa Magufuli alikuwa Mjumbe wa baraza la mawaziri
Toa ushauri kwa leo ulitaka Raisi na Waziri muhusika wafanye nini?:SULUHUISHO HAPO NI KUVUNJA MIKATABA ,NA KUTOKANA SHERIA ZA KIMATAIFA ZA MAKAMPUNI HILO HALIWEZEKANI HASA KAMA MIKATABA ILISAINIWA NA SERIKALI ILE ILE YA MWANZO .UKITAKA USHINDE HILO NI LAZIMA KUWE NA SERIKALI MPYA ILI ICHUKUE ADVANTAGE YA KUWA SERIKALI MPYA
 
Naona kuna wanaosema huo mchanga hauna kitu, kwamba ni waste tu hauna thamani.

Sasa kwa nyie mnaojua mtujuze kama huo mchanga ni waste hauna thamani kwa nini wausafirishe mpaka ulaya?
Mchanga na magwangala ni vitu viwili tofauti kabisa. Mchanga bado unasafirishwa kwa sababu una copper na silver. Magwangala ni waste. Kuwamwagia wananchi kwenye maeneo yao badala ya kuyamwaga kwenye waste dump ni nafuu kwa mwekezaji maana tumempunguzia gharama, na haitamhusu chochote kuhusiana na uharibifu wa mazingira. Magwangala yanahusu mgodi wa Geita, mchanga unahusiana na mgodi wa Buly kule Kahama. Watu wanashangilia ujinga, tena kwa jambo wasilolijua.

Ni sawa nikawa na kiwanda cha kusindika juice, sheria inanilazimisha mabaki niyatupe eneo maalum lililojengwa kwaajili ya utunzaji mazingira, nikajenga, halafu wananchi wakawa wanakuja kufukua ule uchafu, baadaye Rais anakuja na kusema waachie huo uchafu, nenda ukamwage kwenye maeneo yao ili wauokote huo uchafu kiurahisi. Je, mimi nitakataa? Si nitakuwa nimepewa unafuu wa kumwaga uchafu ovyo?
 
acha kuongea pumba ww.kwani mikataba mikubwa waziri anapokwenda kusaini si ni lazima baraza la mawaziri lipitie na kumbuka toka kipindi cha mkapa mikataba hiyo iliposainiwa Magufuli alikuwa Mjumbe wa baraza la mawaziri
Toa ushauri kwa leo ulitaka Raisi na Waziri muhusika wafanye nini?:SULUHUISHO HAPO NI KUVUNJA MIKATABA ,NA KUTOKANA SHERIA ZA KIMATAIFA ZA MAKAMPUNI HILO HALIWEZEKANI HASA KAMA MIKATABA ILISAINIWA NA SERIKALI ILE ILE YA MWANZO .UKITAKA USHINDE HILO NI LAZIMA KUWE NA SERIKALI MPYA ILI ICHUKUE ADVANTAGE YA KUWA SERIKALI MPYA

Kama hilo ndilo unalomaanisha basi hata chadema/ ukawa pia hawana uhalali kulaumu kwa maana fisadi Lowasa pmj na Sumaye wote walikuwa Mawaziri Wakuu wkt hiyo Mikataba inasainiwa ambapo walikuwa ni wakuu wa Serikali, Raisi Magufuli hakuwa Mkuu wa Serikali hivyo hata chadema pia hawawezi kutatua tatizo kwa maana ni sehemu ya tatizo yaani ufisadi!
 
Udongo ni nchi.Hata kama ni waste wacha tubakia nao wenyewe.Kuliko wao kuusafirisha kuupeleka kwao.Tutautumia hata kufukia vifusi kwenye barabara zetu hata kama utakuwa hauna dhahabu.Cha msingi ubaki nchini kwetu hapo hapo maeneo yaliyoko machimbo.Tutautumia hata kufukia mashimo ya dhahabu waliyoaacha wazi baada ya uchimbaji.Tunautaka udongo wetu wa Magwangwala uwe na dhahabu au la.

Hii ndo akili ya CCM? Pathetic.
 
Mchanga na magwangala ni vitu viwili tofauti kabisa. Mchanga bado unasafirishwa kwa sababu una copper na silver. Magwangala ni waste. Kuwamwagia wananchi kwenye maeneo yao badala ya kuyamwaga kwenye waste dump ni nafuu kwa mwekezaji maana tumempunguzia gharama, na haitamhusu chochote kuhusiana na uharibifu wa mazingira. Magwangala yanahusu mgodi wa Geita, mchanga unahusiana na mgodi wa Buly kule Kahama. Watu wanashangilia ujinga, tena kwa jambo wasilolijua.

Ni sawa nikawa na kiwanda cha kusindika juice, sheria inanilazimisha mabaki niyatupe eneo maalum lililojengwa kwaajili ya utunzaji mazingira, nikajenga, halafu wananchi wakawa wanakuja kufukua ule uchafu, baadaye Rais anakuja na kusema waachie huo uchafu, nenda ukamwage kwenye maeneo yao ili wauokote huo uchafu kiurahisi. Je, mimi nitakataa? Si nitakuwa nimepewa unafuu wa kumwaga uchafu ovyo?
Mkuu msambichaka sijui hata ulikuwa wapi tu...ungenisaidia kuwaelimisha hawa Jamaa....yaani watu Sijui wana vichwa vya jinsi gani tu???unamwelewesha mtu kitu kile kile zaidi ya Mara tano lakini bado haelewi...sijui ni makusudi wanafanya hata Sijui..
 
w
Kama hilo ndilo unalomaanisha basi hata chadema/ ukawa pia hawana uhalali kulaumu kwa maana fisadi Lowasa pmj na Sumaye wote walikuwa Mawaziri Wakuu wkt hiyo Mikataba inasainiwa ambapo walikuwa ni wakuu wa Serikali, Raisi Magufuli hakuwa Mkuu wa Serikali hivyo hata chadema pia hawawezi kutatua tatizo kwa maana ni sehemu ya tatizo yaani ufisadi!
ww umeuliza je kunaweza kuwepo solution,nimeweka solution hapo mwishoni bado unaleta vihoja kwani leo chadema ikishika dola na lowassa ausumaye wakiwa ndani ya chama investors watajua ni chama kingine ndio kimeshika dola au watajua bado ni ccm ndio mwenye dola.
mambo ya mikitaba ya makampuni as long as CCM itaendelea kutawala hamna kipengele hata kimoja unachoweza kubadilisha suluhisho wa hilo ni kupata serikali ya chama kipya haijalishi ni cuf,cdm,au nssr
 
Wewe hoja yako uliyoiandika ni kwamba Raisi Magufuli alikuwepo kwenye Baraza la Mawazi wkt Mikataba inasainiwa hivyo nisehemu ya dhambi na mimi nikakujibu kama hivyo ndivyo basi dhambi hiyo hiyo iko chadema pia kwani Sumaye alikuwa Waziri Mkuu chini ya Mkapa wkt Mikataba inasainiwa yaani Mkuu wa Serikali na si ajabu pia Mkuu wa hilo Baraza la Mawaziri unaloliongelea, Fisadi Lowasa pia alikuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya CCM na alikuwepo wkt Mikataba inasainiwa na wote hawa wawili leo hii wako chadema hivyo chadema nao ni sehemu ya hiyo dhambi tena ni sehemu kubwa zaidi ya dhambi kwa maana wkt Mkuu wa CCM na Raisi wa JMTZ Pombe Magufuli (PhD) hakuwa Mkuu wa Serikali hawa wawili (fisadi Lowasa na Sumaye) walikuwa wakuu wa Serikali tena Sumaye kwa miaka 10 na fisadi lowasa amekulia CCM maisha yake yote sasa iweje leo mumkubali na kumpa ugombea uraisi bila hata ya kushindanishwa?!
 
Back
Top Bottom