Eti Hana kadi ya benki, watu wanatumia simbanking tu mie hata sijui kadi ipo wapi?.Ndio maana mama alitulia tuli wakati mumewe anadundwa yawezekana alishapata wa kumtuliza siti ya karibu akamwambia utakula utakunywa usiwe na hofu
Safari sio kitu cha ghafla inakuwaje aanze kutaka kumpa pesa last minute
mwanamke atakuwa alizira akaona ujinga kwa nini hukunipa mapema kwa hiyo hata wakati anadundwa mwanamke aweza kuwa alikuwa akiwapongeza kimoyo moyo wadundaji kuwa loo kidume gani huyu hadi mtu unaondoka hajakupa hela njiani anasubiri unaingia hadi kwwenye ndio anaanza kujifanya anaenda kuzitafuta wacha adundwe
Daah!🙄Ndani ya basi wanatakiwa kuingia abiria tu waliokata tiketi na wafanyakazi wa basi tu sio mtu mwingine
Waliokukunja na kukuvuta miguu wamekuhurumia walitakiwa wakutandike mangumi na makofi juu
Ungempigia simu mkeo ashuke achukue hivyo vipesa vyako koko chini sio wewe upande basi
Ukome kabisa tabia hiyo ya kupanda ndani ya basi wakati wewe sio abiria
Kwa hiyo mkuu unataka kusema hiyo safari ilikua ya ghafula kiasi cha kushindwa kujipanga kabla ya siku ya safari,halafu mke wako unampatia vijihela kwenye basi badala yeye ndio awe mtunza hazina,ili ikitokea dharula yoyote achukue pesa ila wewe upewe taarifa tu ya matumizi na jinsi pesa ilivyo tumika ua bado hujakomaa,au sio mke wako huyo.Nimekuwa mpenzi wa kutumia usafiri wa basi la Shabiby mimi na familia yangu kwa miaka zaidi ya mitano
Dar, Dodoma, Dodoma Arusha.
Ila leo kwa yaliyo nikuta kupitia dereva huyu, imeniuma sana
Tulikata tiketi siti namba 4 kwa ajili ya mke wangu kusafiri toka Arusha kuelekea Dodoma ni katika basi linalo wasili Arusha saa nne asubuhi ili kuelekea Dodoma.
Katika pilikapilika za safari nikajikuta nimesahau kadi yangu ya benki ambayo nilidhamiria kuitumia kutoa pesa ili kumpa mke wangu pesa ya matumizi njiani na hii ndio ikawa sababu kwa mimi kukutana na maumivu niliyoyapata kwa dereva nisiye mfahamu jina lake ila ndiye dereva wa basi tulilo kata tiketi hii,yaani basi la Shabiby.
Kutokana na kusahau kadi ya benki nililazimika kumuacha ndani ya gari mke wangu ambaye nilikuwa nikimsindikiza kutafuta namna nyingine ya kupata pesa ili nimpe ya kula njiani,
Baada ya kufanikiwa nikarejea ndani ya gari, kwa lengo la kumpa hiyo pesa mke wangu,ndipo dereva huyu wa shabiby baada ya kuona kuwa mkononi mwangu nimeshika speaker ndogo ambayo huwa naitumia kwa ujasiliamali ,yeye akahisi labda naingia kuuza bidhaa fulani
Hata hivyo kwa upole nilimweleza kuwa, mimi siingi kuuza ila lengo langu ni kumpa mke wangu pesa ya matumizi njiani.
Kilicho niumiza, bado aliendelea kuni zuia kibabe
Hakuishia hapo tu alinikunja huku kondakta wake akinivuta mguu kwa nje,mbele za mke wangu,abiria na watu wengine,kiukweli nimedhslilishwa,naamini kosa langu ni kuutumia usafiri wa shabiby kumsafirisha mke wangu,halafu kuamua kumletea pesa ya matumizi mke wangu.
Kweli nimejaribu kumwelezea mtu niliye fahamishwa kuwa ni kiongozi wake hata sijaridhishwa na namna alivyoshughulikia kudhalilishwa kwangu,kiukweli nimeamua,maana mimi huwa hakuna aina ya biashara mbayo huwa naifanya ndani ya mabasi,zaidi ya leo kumsindikiza mke wangu.
Kweli,kama kampuni ya mabasi ya shabiby haita muwajibisha huyu,aliye nikunja hata kunitishia kunipiga,kisa,nimemweleza kuwa nampa mke wangu pesa ya matumizi njiani, basi kwa mimi binafsi na familia yangu nitafikiria kuto penda kuutukimia usafiri huu kwa mara nyingine,maana nimeaibishwa sana.
Nimejaribu kutafuta mawasiliano ya kampuni ya basi la shabiby makao makuu ili kutoa taarifa ya kero hii, ila sijatambua namna ya kuwapata,ndio maana nimeandika hapa ili wahusika wapatapo ujumbe angalau walishughulikie hili kama wana upendo na wateja wao,tafadhali wasilifumbie macho
Muda huu basi hilo bado lipo njiani kuelekea dodoma, mke wangu niliye msafirisha anaitwa Silvero Mwacha ,yupo sit namba 4, tafadhali wahusika popote mlipo nimekereka, naomba msilifumbie macho hili.
Ni mimi Emmamuel.
DuhNdio maana mama alitulia tuli wakati mumewe anadundwa yawezekana alishapata wa kumtuliza siti ya karibu akamwambia utakula utakunywa usiwe na hofu
Safari sio kitu cha ghafla inakuwaje aanze kutaka kumpa pesa last minute
mwanamke atakuwa alizira akaona ujinga kwa nini hukunipa mapema kwa hiyo hata wakati anadundwa mwanamke aweza kuwa alikuwa akiwapongeza kimoyo moyo wadundaji kuwa loo kidume gani huyu hadi mtu unaondoka hajakupa hela njiani anasubiri unaingia hadi kwwenye BASI ndio anaanza kujifanya anaenda kuzitafuta wacha adundwe
Dohdawa ya kunguni, muwasho, vipele na harara
Huyu Jamaa anadis shabiby sasa ata support kampuni gani wkt zilizobaki Karibu zote M*vi Tu.Pole kaka Emmanuel. Shabiby ni high class hawataki wauza sumu za panya ndani ya basi.
Hiyo spika imekuponza!.
😹😹Pole, ila kulikuwa kuna ulazima gani kupanda na hiyo speaker?
Au kuingia ndani ya basi?
AsantePole sana mkuu!
Shabiby sio tatizo,ila huyu dereva,maana hata ushahidi wa sababu ya mimi kuingia ndani ya basi nilimwonyesha,ila hakutaka kunielewaHuyu Jamaa anadis shabiby sasa ata support kampuni gani wkt zilizobaki Karibu zote M*vi Tu.
Yaani katka Hali ya kawaida umeenda kutaka kuingia ndani ya Basi, dereva akakukataza (maybe alishaanza kuondoka) Simply ilitakiwa umwite Wife umpe hiyo hela ya matumizi then ushuke story ingekuwa imeishia hapo, sasa inaonekana na wewe ulikomaa tu uingie kilazima huku umebeba mi speaker yako hiyo lazma angekukazia.Shabiby sio tatizo,ila huyu dereva,maana hata ushahidi wa sababu ya mimi kuingia ndani ya basi nilimwonyesha,ila hakutaka kunielewa
Hata hivyo mimi ndie nilikuwa namsafirisha mke wangu,
Shida ni huyu dereva,maana ni mteja ambaye nikitokea hapa jijini arusha ,hata wafanya kazi wa shabiby ofisini,wananitambua
Hata tangu nianze ku utumia usafiri wa shabiby,sijawahi na ubaya alio nifanyia
Wakati mwingine ninasafiri na shabiby toka dodoma mpaka tunduma,dodoma arusha,dodoma dar,
Sijawahi kutana na tatizo hili
Ndio maana naishauri shabiby,wamchunguze huyu dereva
Nadhani ana shida