BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,820
- 287,886
Kampuni sita zilizochota BoT zilisajiliwa siku moja
Mwandishi Wetu
Daily News; Thursday,January 24, 2008 @19:01
KAMPUNI sita kati ya 22 zilizotumiwa kuiba mabilioni ya fedha katika Benki Kuu (BoT) kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ziliandikishwa na kusajiliwa kwa siku moja.
Uchunguzi wa gazeti hili unaonyesha kuwa kampuni za Bencom International Ltd, B. V Holdings Ltd, Venus Hotels Ltd, V.B Associates Company Ltd, Bina Rosort Lt na Bora Hotels & Apartment zote zilisajiliwa kwa siku moja.
Jayantkumar Patel na Devendra Vinodbahi Patel wanatajwa kama wakurugenzi wa kampuni hizo ambazo ziliandikishwa Aprili 4, 2005 zote zikiwa na malengo yanayofanana ya kuagiza na kusafirisha bidhaa mbalimbali nje ya nchi.
Kampuni zote hizo kila moja imeandikishwa kwa mtaji wa Sh milioni 1, kila kampuni ina hisa 100 ambazo zina thamani ya Sh 10,000 kwa kila hisa moja. Kiasi cha Sh bilioni 133 zimechotwa BoT kwa kutumia kampuni 22 ambazo zililipwa kwa kutumia nyaraka bandia.
Patel peke yake anamiliki kampuni nyingine tatu hivyo kufanya aongoze katika wizi wa fedha hizo za umma. Katika mwaka 2005, kampuni nyingi zilizotajwa kuchota mabilioni ziliandikishwa na kusajiliwa.
Kuna kampuni ya Mibale Farms iliandikishwa Septemba 6, 2005, wakurugenzi wake wanatajwa kuwa ni Kiza Selemani na Farijara Hussein, Clayton Marketing Ltd inayomilikiwa na Edwin Mtoi na Elisifu Ngowi na iliandikishwa Juni 6, 2005.
Mwaka huo huo pia kampuni ya Kiloloma and Brothers iliandikishwa Aprili 14. Mkurugenzi wake anatajwa kuwa ni Charles Kissa. Money Planners & Consultants nayo iliandikishwa Machi 24, 2005 na wakurugenzi wake wanatajwa kuwa ni Paul Nyingo na Fundi Kitunga.
Lakini kampuni hizo mbili ni za mtu mmoja maana zinatumia ofisi iliyoko mtaa wa Iramba nyumba namba 7 Magomeni, Dar es Salaam ingawa zilisajiliwa kwa makusudi tofauti.
Moja imesajiliwa kama inashughulika na usambazaji wa vifaa vya ofisini wakati nyingine shughuli yake ni ukusanyaji wa madeni. Mwaka huo wa 2005 kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd pia iliandikishwa Septemba 29 na wakurugenzi wake wanatajwa kuwa ni John Kyamuhendo na Francis William.
Kampuni zingine anazomiliki Patel alizoandikisha miaka ya nyuma ambazo nazo amezitumia kuibia Benki Kuu ni Maltan Mining Company ambayo iliandikishwa Machi 1995. Katika kampuni hiyo Patel aliandikisha kampuni hiyo akiwa na mwanahisa mwingine aliyemtaja kwa jina la Haharier Radhakrishnan.
Lakini Agosti 29, mwaka huo huo, Patel akabadilisha jina la kampuni hiyo na kuiita Noble Maltan. Hata hivyo, tangu iandikishwe mwaka huo hakuwahi kuwasilisha taarifa ya mizania BRELA kama sheria inavyomtaka hali iliyosababisha msajili huyo kumwandikia barua kumtaka awasilishe mizania hiyo.
Patel pia ana kampuni nyingine ya Ndovu Soaps Ltd aliyoiandikisha Februari 18, 1992 na tangu wakati huo hakuwahi kuwasilisha wala kulipia taarifa ya mizania. BRELA pia ilimwandikia barua mwaka jana kumtaka awasilishe na kulipia taarifa hiyo muhimu la sivyo angechukuliwa hatua za kisheria.
Kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni kifungu 108, mtu anayeandikisha kampuni anatakiwa kuwasilisha taarifa za mizania kila mwaka (Annual Returns Report). Katika taarifa hiyo lazima uonyeshe wakurugenzi waliopo, mtaji wa kampuni na shughuli inayoshughulika nazo.
Kampuni yake nyingine ni Navy Cut Tobacco Tanzania Ltd ambayo aliiandikisha Oktoba 12, 1995 kwa ajili ya kusafirisha nje Tumbaku na bidhaa nyingine inayohusiana na tumbaku. Lakini pia hakuwahi kufanya malipo yoyote ya taarifa ya mizania.
Kampuni ya Liquidity Services Ltd inayomilikiwa na Thabit Katunda na Rajab Maranda iliandikishwa Desemba 17, 2004, Njake Hotel & Tours inayomilikiwa na familia ya Japhet Lema iliandikishwa Aprili 10, 2003 na ilianzishwa kwa mtaji wa milioni 200.
Lakini Mei 13, 2005 ilibadilishwa jina na kuitwa Njake Tours & Safaris Ltd. Baadaye mtaji wake uliongezeka ghafla na kufikia Sh bilioni nane. Kampuni ya Excellent Services Ltd iliandikishwa 2004 na wakurugenzi wake walikuwa ni Emil Sabbas na Elisifa Ngowi.
Kampuni hiyo ilianzishwa kwa mtaji wa Sh 500,000, lakini baadaye Sabbas alijiuzulu na kumuuzia hisa zake Massimo Fanneli Desemba 19, 2005. Ghafla mtaji wa kampuni hiyo uliongezeka hadi kufikia Sh milioni 50.
Karnel Ltd ambayo shughuli zake ni usambazaji wa vifaa vya kuzimia moto ilianzishwa Agosti 4, 1998 kwa mtaji wa Sh milioni moja; lakini kufikia Desemba 15 mtaji wake uliongozeka hadi kufikia Sh bilioni 10. Wakati kampuni ya Uwakili ya Malegesi yenyewe imesajiliwa tangu mwaka 2001 na inaongozwa na Bedery Malegesi. Nayo inatajwa katika ufisadi huo wa BoT.