Kampuni saba zaomba kuingiza mafuta nchini-(USALAMA WA TAIFA UKO MASHAKANI)

HISIA KALI

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
694
108
Nimesoma habari kwenye gazeti la Mwananchi yenye kichwa ``Kampuni saba zaomba kuingiza mafuta nchini``. mimi hili linanisumbua kwa kiasi fulani.

Kati ya hizo kampuni saba ni moja tu ambayo ni ya ndani ya nchi. Kampuni mbili zinatoka Bahamas, tatu zinatoka Singapore na moja Geneva Uswisi.

Nina wasiwasi na hizi kampuni kutokana nchi zilikotoka. Bahamas na Uswisi ni tax haven countries. Kwa kifupi watu ambao wanasajili kampuni zao kwenye tax haven countries ni wale ambao hawapendi kulipa kodi na wanafanya biashara za kuficha ficha. Sasa Tanzania ina imani gani na watu kama hawa mpaka itake kuwakabidhi biashara nyeti ya mafuta.

Tukiachana na hilo naoni ni vyema tukajiuliza hivi serikali imeshindwa kuitumia TPDC kuagiza mafuta? Mafuta ni bidhaa nyeti kwa uchumi na usalama wa Taifa kwa ujumla. Hivyo basi sio vyema hata kidogo kuipa kampuni moja au hata tatu za binafsi kufanya biashara ya kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi. Tulishuhudia hivi karibu wafanyabiashara wa mafuta walipogoma kuuza mafuta jinsi nchi ilivyoadhirika. Hawa waliogoma walikuwa wengi sasa je tukimpa mmoja au wachache itakuwaje? Si ndio itakuwa rahisi kwa wao kuamua kufanya chochote kwa sababu watakuwa na nguvu sana kwenye biashara ya mafuta.

Kwa hitimisho nasema biashara ya mafuta ni suala nyeti kwa uchumi na usalama wa taifa hivyo sio vyema kuwategemea watu binafsi kwa asilimia mia moja kuagiza mafuta nje. Nashauri serikali iitumie TPDC kufanya kazi ya kuagiza mafuta nchi. Kama serikali inaona ni kazi kubwa basi hiyo kazi igawenywe nusu kwa nusu. Nusu TPDC na nusu kampuni binafsi.

Tukumbuke tu suala la mafuta ni nyeti kupita hata suala la umeme. Mafuta yanatumika hata sehemu ambayo umeme haupo. Pia mafuta ndio yanatumika kuzalisha umeme kwa kiasi fulani.

 

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,667
Hebu wadau tutajienei hayo makampuni tutafute taarifa zake hapa kwa faida yetu wote.
 

Joel

JF-Expert Member
Sep 1, 2007
1,009
539
inabidi tuchimbe tupate info za hayo makampuni maana watu wa idara za serikali wanaohusika na uchimbuaji wa taarifa za makampuni kama haya hawawezi kufanya kazi hii, inabidi wazalendo tuwasaide kuokoa nchi yetu.tupeni majina ya hizo kampuni tuanze juchimba na kuchimbua.
 

Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,425
1,034
bot_tabimg.gif

Kampuni saba zaomba kuingiza mafuta nchini
Monday, 12 September 2011 19:57
0digg

enda%20mafuta.jpg
Karani wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Joyce Makundi, akionyesha kwa wadau baadhi ya bahasha za maombi ya kampuni nane zilizoomba zabuni ya kuingiza nishati hiyo hapa nchini. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni ya TPDC Dismas Fuko. Picha na Zacharia Osanga

Patricia Kimelemeta
KAMPUNI saba zimejitokeza kuwania zabuni ya ununuzi wa mafuta nje ya nchi iliyotangazwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Agosti 11 mwaka huu.

Kampuni sita kati ya hizo zinatoka nje ya nchi na moja ni kampuni ya ndani, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa, kampuni za ndani zimeshindwa kujitokeza kuwania zabuni za ununuzi wa mafuta.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya zabuni, Dismas Fuko alisema kuwa, baada ya kutangazwa kwa zabuni hiyo, zaidi ya kampuni 25 zilijitokeza kuchukua fomu, lakini mpaka wanafunga ni kampuni zaba tu ndizo zilizorudisha fomu hizo.

Alisema, kampuni za ndani ambazo zimejitokeza kuwania zabuni hiyo ni moja ambayo ni Kampuni ya Mafuta ya Prevail (PPTL) wakati kampuni za nje ni pamoja na Independent Petroleum Group, Galana Petroleum Limited zinazotoka Bahamas.
Alisema, kampuni zingine ni pamoja na Addax Energy Limited kutoka Geneva, Vitol SA, Agusta Energy SA na Trafigura PTE Limited zote za nchini Singapore.

"Tulitangaza zabuni ya ununuzi wa mafuta kulingana na bei ya soko la dunia na kwamba kampuni 25 zikiwamo za ndani na nje ya nchi zilijitokeza kuwania nafasi hiyo, lakini mpaka tunafunga tenda hiyo, ni kampuni saba tu ndizo zilizorudisha, kutokana na hali hiyo kampuni hizo ndizo zitakazoingia kwenye kinyang'anyiro cha kupata kampuni moja," alisema Fuko.

Aliongeza, kwa mujibu wa sheria za Mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Maji(Ewura) zabuni hiyo itafanya kazi kwa muda wa siku 90 ili kuweze kupitia nyaraka za kampuni hizo na kutoa uamuzi.

Alisema, kutokana na hali hiyo, TPDC imeunda kamati ya wataalamu ambao watapitia nyaraka hizo kwa kufuata taratibu na kanuni za manunuzi ili kuangalia kama kampuni hizo zimefuata sheria na taratibu za ununuzi kabla ya kutangaza aliyeshinda zabuni hiyo.


 

Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,425
1,034
Ebu wadau tutajienei hayo makampuni tutafute taarifa zake hapa kwa faida yetu wote.
.. kampuni za ndani ambazo zimejitokeza kuwania zabuni hiyo ni moja ambayo ni Kampuni ya Mafuta ya Prevail (PPTL) wakati kampuni za nje ni pamoja na Independent Petroleum Group, Galana Petroleum Limited zinazotoka Bahamas.
Alisema, kampuni zingine ni pamoja na Addax Energy Limited kutoka Geneva, Vitol SA, Agusta Energy SA na Trafigura PTE Limited zote za nchini Singapore.
 

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,953
2,118
Kwa kufuatilia yaliyoandikwa katika gazeti la Mwananchi la leo tarehe 13 Septemba ukurasa wa pili, kampuni hizo saba ni:

(1) Kampuni ya Mafuta ya Prevail (PPTL)-Tanzania.

(2) Independent Petroleum Group - Bahamas.

(3) Galana Petroleum Limited - Bahamas.

(4) Addax Energy Limited - Geneva.

(5) Vitol SA - Singapore.

(6) Augusta Energy SA - Singapore.

(7) Trafigura PTE Limited - Singapore.

Nawasilisha.
 

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
9,070
5,250
Kwa kufuatilia yaliyoandikwa katika gazeti la Mwananchi la leo tarehe 13 Septemba ukurasa wa pili, kampuni hizo saba ni:

(1) Kampuni ya Mafuta ya Prevail (PPTL)-Tanzania.
(2) Independent Petroleum Group - Bahamas.
(3) Galana Petroleum Limited - Bahamas.
(4) Addax Energy Limited - Geneva.
(5) Vitol SA - Singapore.
(6) Augusta Energy SA - Singapore.
(7) Trafigura PTE Limited - Singapore.

Nawasilisha.

hapo kampuni ni nne tu kwa mtiririko wa nchi hizo zinazotoka nchi moja kampuni tatu utakuta mmiliki ni mmoja mkiinyima moja anapata kwa nyingine.
 

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,319
Kuna mizengwe mingi sana kiasi cha makampuni mengi ya Tz wanaofanya biashara hiyo ya mafuta kushindwa ku tender.

Ok. Kila la kheir
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom