Kampuni kutoka China yashinda zabuni ya BRT awamu ya pili kutoka Kariakoo hadi Mbagala

Sidhani vituo vilivyopo sasa kituo hadi kituo cha daladala kwenda mbagala hakizidi mita 200 Na havizidi 14.Kuwa kutakuwa Na Vituo 29 hadi mbagala sielewi kweli.Nadhani kuna kosa la kiuandishi.Haiwezekani vikawa vituo 29
Nyie jamaa wa Lumumba linapokujaga swala la Magazijuto hamuelewagi kabisa, Hapa ni hesabu tu, numbers hazidanganyi. Kama barabara ni kilometa 20 (yaani mita 20,000), na unasema kituo hadi kituo kwa sasa haizidi mita 200 ( means sometimes inapungua),

Ina maana idadi ya vituo kwa sasa ni zaidi ya (20,000/200) = vituo 100+ ??

Na kama kituo hadi kituo tuseme ndio hizo 200mita maximum, na idadi ya vituo ni hiyo 14maximum, means unataka kusema barabara ina urefu wa (200mita x 14) + mita200 = Mita 3,000 = 3km tu maximum?

Acha uongo Mjomba,
 
Hii ya ubungo mpaka mbezi magari ni machache mno na mengine yalisha haribika yapo jangwani mle na isitoshe msimu wa mvua ndio huu tena sijui wamejipanga vipi pale.
Tatizo siyo barabara hapo. Tatizo hapo ni kampuni hiyo ya mabasi kuendeshwa na kusimamiwa na Watanzania.

Tunachoweza Watanzania ni ngoma, ulevi, wizi, majungu, uzembe na kuharibu.

Tunaiona BRT inavyokufa lakini hakuna hatua yoyote inayochukuliwa ya kuinusuru. Tunabadili wafanyakazi badala ya kubadili namna nzima ya utendaji.
 
Je, kama tatizo ni ujinga wa wakandarasi, je kwa nini wasipatiwe elimu kuondoa huo ujinga kwa manufaa ya taifa zima.?
Mpaka unafikia hatua ya kuwa mkandarasi halafu huelewi faida ya kupata tenda kubwa kama hizi za BRT basi inabidi utafute shughuli nyingine ya kufanya. Ukandarasi sio wito wako.
 
Tatizo siyo barabara hapo. Tatizo hapo ni kampuni hiyo ya mabasi kuendeshwa na kusimamiwa na Watanzania.

Tunachoweza Watanzania ni ngoma, ulevi, wizi, majungu, uzembe na kuharibu.

Tunaiona BRT inavyokufa lakini hakuna hatua yoyote inayochukuliwa ya kuinusuru. Tunabadili wafanyakazi badala ya kubadili namna nzima ya utendaji.
Yale yale ya kusoma ili mtu afaulu mitihani badala ya kupata elimu itakayoyasaidia maisha yake.
 
Mbongo anapo ajiriwa anawaza atapigaje ela ili 'atoke'. Si mfagizi si mkurugenzi. matokeo yake project nyingi za wabongo azifanyi vizuri au zinakufa.
 
Sidhani vituo vilivyopo sasa kituo hadi kituo cha daladala kwenda mbagala hakizidi mita 200 Na havizidi 14.Kuwa kutakuwa Na Vituo 29 hadi mbagala sielewi kweli.Nadhani kuna kosa la kiuandishi.Haiwezekani vikawa vituo 29

Ukiusoma vizuri mradi huu wa awamu ya pili utahusisha barabara ya Kilwa means kutoka town mpaka Mbagala ambapo jumla ni Km 10+
Pia utahusisha kumalizia barabara ya Kawawa Kusini kuanzia Magomeni mataa kupitia Ilala Boma hadi Karume hadi mataa ya Chang`ombe ambapo inasemekana watajenga flyover pamoja na mataa ya Uhasibu, ikishavuka mataa ya Chang`ombe itapasua Keko yote na kupita barabara ya Chang`ombe hadi barabara ya Mgulani na kutokea kwenye ile roundabout ya Mgulani JKT na Kilwa Road ( ilipo shule ya sekondari Jitegemee ) ambapo pale ndo itakutana na hiyo route ya Mbagala to K/koo jumla yake ndo 20.3 Km
Kwa idadi hiyo ya Kms na idadi ya vituo ni sawa tuu
au chukulia mfano phase one kutoka Kimara-Morocco hadi Gerezani-Kivukoni jumla ni Km 21 na vituo ni 29 pia
Hivi kwa haraka unaweza sema kutoka Kimara hadi K/koo ni Km 21!!!? La hasha bali wamehasibia hadi kutoka Morocco kwenda town
Vivyo hivyo kwa phase two hii
 
VP kampuni za wazawa? Je, hawawezi kufanya hii project? Je, tatizo ni ujuzi mdogo, elimu duni, uzoefu mdogo ama mitaji midogo ya wakandarasi wetu?

Kama tatizo ni ujuzi na uzoefu Mdogo, je kama nchi tuliwawezesha vipi kupata ujuzi kwenye phase 1 ya huu mradi?

Kama tatizo ni elimu mbovu, je kuna hatua gani zinachukuliwa na wahusika kurekebisha hilo?

Na kama tatizo ni mitaji midogo ya wakandarasi, je taasisi zetu za kifedha nchini zina msaada wowote? Na je, mfumo mzima wa upatikanaji mitaji kwa kampuni za wazawa kwa projects kama hizi upo vipi?

Je tunaelewa madhara ya kiuchumi kwa kuwa tegemezi kitaaluma?

Haya ni maswali ambayo kila mzalendo wa kweli anatakiwa kujiuliza.
Hela.za mkopo. Na ndo moja ya masharti ya mkopo! % flan ya hela lazima irudi kwao
 
Utaalamu gani koko huo ina maana hata kama eneo ni pori hamna watu unaweka kituo kisa Ku meet rule ya kuwa Kila mita 500 kituo cha basi?
Wambie.Kwa mfano kutoka Mtongani mpaka kituo kinachofuata unapoenda Mbagala Ni mita Mia tano?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom