Kampuni kutoa misaada iitwayo Corporate Social Responsibility, iwe sehemu ya uwekezaji na si hisani

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,803
1,863
Kamati ya Bunge inapendekeza kuwa sasa hii

Kuna misaada ambayo hutolewa na makampuni huku tukiwaona wakipiga picha magazetini. Mfano ni ile ambayo NMB tunapomuona Shyrose Bhanji akionekana huku na kule akitoa ama cheque, madawati kwa shule, cement nk.

Misaada hii huitwa Corporate Social Responsibility (CSR).

Niko naangalia Bunge, sasa hivi Kamati ya Bunge iliyojadili dakika hii mapendekezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu imependekeza kwamba misaada hii iwe ni sehemu ya uwekezaji na isiwe tena hisani kama ilivyo sasa.

Kaisema kwa kifupi sana na sijui matokeo ya mapendekezo hayo itakuwa ni nini?

Mnaonaje wadau
 
Hivi kumbe kuna mambo yanaenda ndivyo sivyo Tz hii eeh..tunasoma Corporate Social Responsibility (CSR) tunaambiwa ni wajibu lazima utimizwe kumbe watu na makampuni yalikuwa yanafanya kama hisani tu..hv Tanzania ni nchi iliyomkosea nini Muumba maskini..Sasa ndiyo wanaamka.........Mnyika hakukosea kusema dhaifu.
 
Back
Top Bottom