Kampuni ipi ina betri nzuri za simu au nini cha kuangalia kujua betri yenye ubora?

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
25,991
56,160
Wakuu karibuni kufahamishana ni kampuni gani zina betrii nzuri za simu au ni vigezo gani vya kuangalia ili kutambua ubora wa betrii haswa katika uimara na utunzaji wa chaji.

Karibuni.
 
Kitu kikubwa kinachoathiri battery ya simu.
1. Manufacturing process ya processor, inapimwa kwa nm jinsi nm(nanometres) inapokuwa ndogo ndio jinsi inavyokula umeme kidogo na kusababisha simu kukaa na chaji. Kwa simu za sasa 14nm kushuka chini unatakiwa utafute.

2. Display
Jinsi display inavyokuwa nzuri na resolution kubwa na refresh rate kubwa ndio jinsi inavyokula umeme mwingi na kusababisha simu isikae na chaji.

3. Optimization ya software,
Software inaweza kuwa optimized isile chaji sana, mfano inaweza kuuwa background activities kila baada ya dk 15 kutunza chaji.

4. Wingi wa Mah za battery, jinsi battery linavyokuwa na Mah nyingi ndio jinsi simu itakaa na chaji zaidi.

Kuzipa real life example hizo point za juu tutumie simu hizi hapa mbili
-realme 6i battery 5000mah
gsmarena_957.jpg


-SAMSUNG M30s battery 6000mah
gsmarean_437.jpg


Hapo ukiangalia m30s ina battery kubwa la 6000mah ila imepitwa kila idara na hio 6i kwenye ukaaji chaji,
Sababu ni hizo hapo juu
-Realme 6i kioo chake ni 720p wakati m30s ni 1080p
-oppo/BBK wapo aggressive sana kwenye kuua background tasks.

Ila kwenye upigaji simu m30 ina score kubwa zaidi sababu ndio wakati ambao kioo kinazima hivyo ulaji chaji haujalishi resolution ya kioo.

Sema jambo moja ufahamu, jinsi kampuni inavyotengeneza simu inayokaa na chaji zaidi ndio jinsi simu inavyokuwa mbaya kutumia simu ya 720p mwaka 2020 sio jambo linalopendezesha macho ama kila saa app kufungwa, hivyo ni vyema kubalance battery life na feature za simu.

Hizi ni baadhi ya simu zinazokaa sana na chaji kwa sasa
-realme 6i
-xiaomi poco F2
-xiaomi redmi note 9s
-samsung m30s/31
-realme 5
-motorola moto G8 power
-Huawei p40 lite
-vivo Iqoo 3 5g (flagship pekee)

Source gsmarena
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom