Wadau kuna yeyote ambaye amechimba kisima na hawa jamaa wa Drilling and Dam Construction Agency (DDCA) wa ubungo? Nasikia wapo shwari sana. Naomba atupe tathmini yake kama wanafaa (kwa kufanya survey na kisha kuchimba). Na kama wapo wengine basi chapisha majina yao bila kusita. Hivi diameter ya kisima kikubwa kabisa (kulingana na mabomba yaliyopo sokoni) ni ipi? Mfano kama nahitaji kisima kwa ajili ya biashara (kama nahitaji maji mengi sana) nahitaji kuchimba kisima cha diameter kiasi gani? Ni kweli kwamba diameter nayo itategemeana na uwingi wa maji eneo husika kama ilivyo kwa urefu wa kisima?