Kampuni iliyomng’oa waziri yapigwa stop, Mwakiembe VS Nundu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni iliyomng’oa waziri yapigwa stop, Mwakiembe VS Nundu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Sep 18, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]
  :A S 465:Harison Mwakiembe VS Omar Nundu:A S 465:​

  KAMPUNI iliyokuwa kiini cha mjadala na hatimaye kung'olewa kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Omar Nundu, China Communications Construction Company (CCCC) Ltd, iliyokuwa ikipiganiwa na uongozi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) uliosimamishwa pamoja na wabunge kupitia Kamati ya Bunge ya Miundombinu, inatuhumiwa na Benki ya Dunia kwa kughushi na kula rushwa, imefahamika. Kutokana na tuhuma hizo ambazo hata hivyo kampuni hiyo imekanusha kupitia gazeti la Guyana Times la nchini Guyana, nchi iliyoko Pwani ya Kusini ya Amerika, Benki ya Dunia imezuia kuipa mkopo na dhamana yoyote kampuni hiyo kutokana na kuhusishwa katika kashfa hizo za rushwa na kughushi.


  Mbali na uamuzi huo wa Benki ya Dunia, Mamlaka ya Ununuzi wa Umma nchini (PPRA) imeizuia kampuni hiyo kwa miaka 10 kutopewa kazi nchini (blacklisted), huku Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, akimtupia ‘mpira' Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuamua kuinyang'anya kazi kampuni hiyo au la, kwa kuzingatia kashfa za sasa. Kwa mujibu wa taarifa ya Benki ya Dunia inayopatikana katika tovuti ya taasisi hiyo kubwa ya kifedha duniani, ambayo imekuwa na sera ya kutoa mikopo na dhamana kwa kampuni kubwa za kimataifa ili kufanikisha shughuli zao katika nchi mbalimbali wanakoshinda zabuni za uwekezaji au ujenzi, China Communicatiosn Construction Company sasa haitapewa mkataba wowote na benki ya dunia.


  "Orodha hii ni ya hivi karibuni, inahusu kampuni ambazo hazitapewa mkataba wa fedha na Benki ya Dunia kwa ajili ya shughuli zao. Amri hii ni utekelezaji wa sera ya Benki ya Dunia katika kupinga masuala ya rushwa na kughushi," inaeleza taarifa ya Benki ya Dunia iliyopo katika tovuti ya taasisi hiyo.


  Katika tuhuma dhidi yake, CCCC inadaiwa kupata baadhi ya zabuni zake kwa njia ya rushwa na kughushi katika baadhi ya nchi, kwa namna mbalimbali ikiwamo kupitia kampuni zake tanzu. Kati ya nchi hizo ni pamoja na China, ambako hadi sasa kuna kesi kati ya kampuni tanzu ya CCCC na mamlaka ya nchini humo. Lakini katika utetezi wao kupitia taarifa iliyochapishwa katikaGuyana Times, CCCC wanakanusha wakisema katika miradi yao mingi wamekuwa wakiiendesha kwa ubia kati ya mamlaka za nchi husika na kampuni yao na kwa hiyo, katika utetezi wao huo licha ya kukanusha wameeleza kuwa sehemu ya maelezo yanapaswa kutolewa na wabia wao na kusisitiza kuwa, kila upande katika mkataba una haki sambamba na wajibu.


  Moja ya kampuni tanzu ya CCCC, China Road and Bridge Corporation (CRBC) iliyochukuliwa mwaka 2005 na CCCC, inatuhumiwa kutoa mlungula ili kushinda zabuni ya ujenzi wa barabara na daraja nchini Philippine, mradi ambao ulikuwa ukifadhiliwa na Benki ya Dunia. Tuhuma dhidi ya CCCC zilianza kuiandama kampuni hiyo wiki kadhaa baada ya kutetewa na wabunge ipewe zabuni ya upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam.


  Kutokana na Waziri wa Uchukuzi kwa wakati huo, Omar Nundu kuitilia shaka kampuni hiyo kiasi cha kuhoji ni kwa nini inatetewa kwa nguvu kubwa, waziri huyo aliingia katika mgawanyiko wa dhahiri na aliyekuwa Naibu Waziri wake, Dk. Athumani Mfutakamba. Katika mvutano wao, Waziri alifikia hatua ya kumtuhumu Naibu wake kugharimiwa safari kwenda nje ya nchi na kampuni aliyokuwa akiitetea ipewe jukumu la upanuzi wa bandari, lakini hatimaye Rais Kikwete aliwatupa wote nje ya Baraza la Mawaziri na kumteua Dk. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Uchukuzi, na Naibu wake Dk. Charles Tizeba.


  Mbali na hali hiyo katika mvutano huo, Bandari pamoja na Bodi kwa kushirikiana na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba, nao walikuwa wakiipigia debe CCCC, lakini baadhi ya wabunge wakiwamo wa kambi ya upinzani walitaka suala hilo likabiliwe kwa umakini mkubwa.


  Tahadhari ya wabunge wa upinzani, hususan Zitto Kabwe na John Mnyika, ilikuwa kwamba Serikali isitoe kazi ya upanuzi wa bandari gati namba 13 na 14 hadi ijiridhishe kuhusu gharama halisi za upanuzi kwa kutafuta mkandarasi huru atakayefanya upembuzi yakinifu badala ya serikali kukariri gharama zilizotokana na upembuzi yakinifu wa CCCC ambaye ndiye mjenzi wa gati hiyo. Katika mvutano huo ulikuwa wa wazi kati ya bandari na bodi yake kwa kushirikisha wabunge kwa upande mmoja na waziri kwa upande mwingine.


  Mamlaka za Tanzania
  Wakati PPRA ikiwa tayari imeamua kuifungia kampuni hiyo kwa miaka 10 kutoshindania zabuni za umma nchini, Mwanasheria Mkuu (AG) Frederick Werema amekwishatoa ushauri wa kitaalamu kwa Waziri Mwakyembe kuhusu kampuni hiyo ambayo ilipiganiwa na wanasiasa na uongozi wa bandari. Katika ushauri wake, AG anasema kampuni hiyo tayari ilikuwa na mkataba na Mamlaka ya Bandari kuhusu upanuzi wa gati namba 13 na 14 kabla ya uamuzi wa Benki ya Dunia na kwamba kwa kuzingatia taarifa mpya za kashfa kwa kampuni hiyo, uamuzi wowote unaweza kuchukuliwa.


  Chanzo chetu cha habari kimemweleza mwandishi wetu kwamba, sasa ni jukumu la wizara kuamua kuiacha kampuni iendelee na kazi ya upanuzi wa bandari au kuinyang'anya mkataba. Hata hivyo, uchunguzi zaidi unabainisha kuwa upanuzi wa bandari hiyo unaendeshwa kwa fedha za Benki ya Exim ya China, na kwamba hata kama kampuni hiyo itanyang'anywa kazi hiyo ni lazima kampuni nyingine ya China ipewe zabuni hiyo kwa sababu masharti ya mkopo ni kwamba kazi itolewa kwa kampuni ya China.


  Mwandishi wetu aliwasiliana na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kujua uamuzi wa serikali baada ya Benki ya Dunia kuiwekea pingamizi kampuni hiyo ya China Communications and Constructions Ltd. Katika maelezo yake, Dk. Mwakyembe mbali na kuthibitisha kuwa PPRA wameiweka ‘kizuizini' kampuni hiyo kushindana katika zabuni za umma kwa miaka 10, lakini pia alithibitisha wizara yake kupokea ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. "Tumepokea ushauri wa AG (Mwanasheria Mkuu), kwa sasa tunalifanyia kazi suala hilo ili tuone namna bora ya kufanya uamuzi. Uamuzi unaweza kuwa ama kuendelea kuiacha kampuni hiyo ifanye kazi kwa sababu pengine iliingia mkataba kabla ya misukosuko hii ya sasa, au kuteua kampuni nyingine ya China ifanye kazi hiyo na kuachana na CCCC. Tutafanyia kazi suala hilo bila kuchelewa ndani ya mwezi huu, hatutaki upanuzi wa bandari kuchelewa," alisema Dk. Mwakyembe.
   
 2. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu lakini sioni uhusiano wa habari hii na connotation ya Mwakyembe Versus Omar Nundu!
  Mimi nikifikiri as far as CCCC is concerned they are on the same side-kuipinga CCCC kwa kuhusika na ufisadi.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  [​IMG] [​IMG]

  Mfupa huo ulimshinda Omar Nundu hata alipoagizwa na Bunge na akaishia kunyosheana vidole na naibu wake. Mwanasheria Mkuu amemtupia mpria Mwakiembe, je utamshinda kama Nundu au makucha ya Makiembe yataisambaratisha Kampuni hiyo?
  masopakyindi hii ndiyo falsafa ya ujumbe wangu.

  Huwe sipendi kuhitimisha au kuonyesha mapema mawazo yangu binafsi juu ya mada husika kwani nitakuwa nimehitimisha na hivyo kutotoa mwanya wa wadau kuchangia kupata mengi mazuri.
   
 4. J

  J4MAYOKA Senior Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Only in Tanzania

  Waziri aliyepiga vita rushwa (NUNDU) alifukuzwa kazi kisa ali go public na taarifa za kuhusu naibu wake.

  zaidi ya hayo hakuna sheria hata moja aliyevunja. sana sana utaambiwa ohhh asingeenda public na kuhusu naibu wake

  sasa nadhani mnaelewa kwa nini tunataka katiba mpya kama ya Kenya ili kuondoa upuuzi huu.

  Binafsi siwapendi CHADEMA lakini juzi nimetazama video ya Freeman kule DMV alisema neno moja ambalo limekosekana kwenye kuendesha nchi ya Tanzania: LAW& ORDER

  Itawezekana vipi waziri mkuu ana mpa ruhusa naibu waziri kwenda nje ya nchi kukutana na hawa wachina bila waziri husika kutojua?
   
 5. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Candid, mimi nafikiri mmpambano utakuwa kati ya Mwakyembe na CCCC na wadau wao(waliowezeshwa kwa kitu chochote na CCCC).
  Masikini Omar Nundu alifanya kosa la kiutendaji, badala ya kumshughulikia CCCC na maosa yake, yeye akaanza kumtupia lawama Naibu wake hadharani!
  Hili ni kosa kubwa la kuonyesha uwezo mdogo wa kutumia mamlaka makubwa aliyo kabidhiwa na Taifa.

  So far Mwakyembe is on the right track, na ana support ya PPRA, ambayo kisheria vile vile ina wazuia CCCC kufanyakazi nchi hii.

  Tatizo litakuwa wale waliopewa "KITU KIDOGO" na CCCC-kampuni ya kiChina hii.

  Tulio katika field tuanjua rafu nyingi zinazochezwa na makampuni ya kiChina katika miradi mingi nchini, na kama wachina waliopewa miradi ya barabara kuishia kuitusi Serikali baada ya kukosa malipo, na hawa CCCC watakuja sema yaliyo moyoni, muda si mrefu.
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu uko sawa kabisa, ila usihuzunike sana hata mwakyembe anafanya the same na ile aliyokuwa akiyafanya Nundu. in short all are good. utaona kunatofauti tu kama wewe ni wale wenzetu kama mleta mada alivyoileta kishabiki.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tatizo la Omar Nundu ni nadharia wakati alitakiwa kuonyesha utendani wake katika kuwawajibisha waliomharibia wizara yake. Mwakiembe amethubutu kuonyesha kukunjua makucha yake, hata kama kuna mapungufu fulani katika baadhi ya maamuzi yake, kwa vyo vyote hatua kadhaa alizochuku mpaka sasa zinampatia credits na kuwatishia walioona hakuna wa kuwahumbisha kwani akina Nundu walikuwa wanauzunguka mbuyu bila kuugusa, lakini Mwakiembe ameamua kuanzia kuichimbua mizizi yake na unaanza kutetereka nguvu.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tuko pamoja, tatizo la Nundu ni nadharia bila matendo, na kuona aonewe huruma kwa nadharia bila kuchukua haua stahiki akiwa kiongozi mwandamizi mwenye mamlaka katika wizara yake.

  Mangapi yalilalamikiwa ambayo aliyafumbia macho lakini Mwakiembe amechukua hatua?

  Hii reli ambayo itakuja kusaidia kupungusa tatizo la usafiri walishamshauri mara kadhaa lakini hakuwa tayari kuchukua hatua, mwenyeke Mwakiembe kuingia tu ni vidonge vya kwinini tu hadi raha virusi vya malaria vinaanza kupoteza nguvu za kujijenga damuni.
   
 9. r

  republicoftabora Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwakyembe yupi unayemzungumzia wewe?

  Yule aliyeleta ngebe kisha akaenda kuchukua residency kule Apollo au ?

  Mwakyembe hawezi kufanya lolote pale baada ya yaliyomkuta.
   
 10. r

  republicoftabora Member

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  PPRA ipi unayozungumzia wewe?

  Mikataba kibao kwenye secta zote kwenye serikali ya Tanzania imejaa rushwa. Hivi ushawahi kuskia PPRA wakatoa listi ya malalamiko wanayopelekewa na ipi ambayo wameishugulikia na ipi ambayo wametupilia mbali?

  acha kuishi kwenye giza. Tanzania ili ufanikiwe inabidi uwe kama mwenda wazimu hiyo ndio ukweli wenyewe. Narudia, Nundu ku go public ni kwa sababu alikuwa hana namna. Kuna mdau hapo juu kashasema. issue iko hivi:

  1. Kati ya kutanua gati isingezidi milioni 250

  2. MGAWE na team yake wanamwambia consultant aweke estimate ya milioni 600 usd

  3. TENDER BOARD ya TPA inakubaliana na upuuzi huu

  4. TPA BOARD nayo inakubaliana na ujinga huu wa ku over inflate bei halisi toka 250 to 600

  5. Naibu waziri anakwenda kwa pinda ambaye anampa ruhusa huyu jamaa kutembelea miradi ya wachina kwa gharama za wachina kinyume na sheria za maadili ya kazi.

  6. Bodi na KAMATI YA BUNGE pia inapewa dili la kutembelea miradi ya mafisadi wa kichina

  7. NUNDU bado hana habari jinsi naibu wake anavyo m subordinate

  8. BODI YA TPA, NAIBU WAZIRI, KAMATI YA BUNGE, MGAWE, MEDIA, PINDA wote wanatengeneza fitna kuwa Nundu hafai hivi ulitegemea Nundu akae tuuu na kutazama michoro ya Airbus A380 kwenye wikipedia kutwa nzima huku anashambuliwa left and right?

  Hao waliompa kazi waliamua kwa kusudi kumtosa na hii ni dhulma kubwa sana kwani kama walikuwa hawataki anavyofanya kazi wasingempa hicho cheo.

  Sasa alivyoamua kujibu wajuaji wa protocali wanakwambia ohhh asingeenda public. Acheni nyie

  Huyo mwakwenbe mnayetaka kumtetea tangu aingie kashaleta taarifa jinsi gani MGAWE, MANAGEMENT YA TPA, BODI YA TPA, KAMATI YA BUNGE walivyokula pesa?

  Kilichobaki anatuvalia kofia za Panama na kutafuta publicity kama Zitto.

  Katika kali ya kawaida ilitakiwa wote wasimamishwe kazi huku uchunguzi unaendelea sasa inakuwa yale ambao wazungu wanaita whitewash

  naunga mkono kuwa nchi hii ni ya wenda wazimu na GREAT THINKERS wa JF mmekuwa kama vile NON THINKERS. Hakuna anayelalamika na maisha kama kawaida yanaendelea.
   
 11. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Mkuu punguza munkari and cool down!
  nijibu swali simple.

  CCCC imekuwa blacklisted na PPRA , ni kweli au hapana?
   
 12. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Mkuu ili isionekane kuwa una chuki binafsi na Mh Mwakyembe , jibu swali nililo kuuliza hapo awali.
  Ama sivyo inaelekea nyie ndio wahanga wa CCCC na michoro yao.
   
 13. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Unamaanisha kina Peter Serukamba??
   
Loading...