Kampuni 4 zabainika kukwepa kodi Sh. Bilioni 29.2. SKOL, A. M Steel wamo...

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,577
6,582
Wakuu, kuna hii Joint statement from PCCB and TRA ambayo imenishtua kidogo; makampuni haya yatawajibishwa vipi?

========

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) wamebaini kuwepo na baadhi ya Makampuni na watu binafsi ambao wamekuwa wakijihusisha na ukwepaji Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya Mapato kwa kutumia Mashine za Kielektroniki (EFDs) ambazo hazijasajiliwa na TRA na kutoa risiti bandia.

Makampuni hayo yamekuwa yakinunua risiti za manunuzi bandia kutoka kwa watu wanaomiliki mashine za kielektroniki (EFDs) ambazo hazijasajiliwa na kuzitumia risiti hizo kudai marejesho ya VAT bila kuwepo na bidhaa au huduma halisi iliyouzwa au kutolewa na muhusika, kitendo ambacho kinainyima Serikali mapato stahiki kwa mujibu wa sheria.

TRA kwa kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi ili kubaini makampuni yote yanayojihusisha na udanganyifu huu, ambapo hadi sasa jumla ya makampuni manne (4) yamebainika kujihusisha na ukwepaji kodi kwa mtindo huu kuanzia mwaka 2010 hadi 2014; na jumla ya shilingi 29,216,900,301.7 imebainika kutokulipwa Serikalini na makampuni hayo kwa kipindi hicho.

Makampuni hayo manne ni pamoja na Skol Building Material Ltd ambayo tangu mwaka 2012 hadi 2013 haikulipa jumla ya VAT ya shilingi 5,464,915,963 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya shilingi 10,960,787,861 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni shilingi 16,425,703,824 kwa kipindi hicho.

Kampuni nyingine ni Farm Plant (T) Limited, tangu mwaka 2010 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya shilingi 5,930,170,573 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya shilingi 4,948,393,516 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni shilingi 10,878,564,089.

Kwa upande wa A.M. Steel & Iron Mills Limited kuanzia mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya shilingi 79,016,112 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya shilingi 131,693,518 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni shilingi 210,709,630.

Kampuni nyingine ni A.M. Trailer Manufacturers Limited ambayo tangu mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya shilingi 638,221,034.80 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya shilingi 1,063,701,724.00 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni shilingi 1,701,922,758.80

Baada ya kubaini ukwepaji kodi wa makampuni hayo, TRA kwa kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizi na mara baada ya uchunguzi kukamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kukwepa kodi.

“Ni wito wangu kwa wafanyabiashara wote kutojihusisha na kununua risiti za bandia na kudai marejesho ya (VAT) yasiyostahili kwakuwa Mamlaka imejidhatiti kuendelea na zoezi hili la kuwabaini wafanyabiashara wanao kwepa kodi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwa hatua stahiki”.

Alisema Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata.

Imetolewa na:

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa pamoja.
 
mafuta hayana kodi ya VAT
Mi nilifikiri ni uongo. Kuna dereva wa bajaji aliniambia alienda shell kuweka mafuta wakampa risiti ya 13000 badala ya 15000.
Alipolalamika muuzaji akamwambia haina shaka anaweza kumtolea nyingine. Na kweli akampa ya 15000
Sasa dereva bajaji akawaanajiuliza inawezekana vp.
Ikabidi aangalie risit, kumbe ile risiti haioneshi makato ya vat.
Kweli watanzania ni hatari
 
Si kila mashine ni ya vat?? Hata ukija dukani kwangu naweza kukupa hata risiti tano nikijua kuna wateja zaidi ya 5 ambao hawatadai risiti...
Kulipa kodi ni uzalendo na maamuzi ya mfanya biashara...anaweza kukwepa na asikamatwe...serikali wekeni mazingira mazuri kwa wafanya biashara ... Punguzeni rundo la kodi lisilo na lazima...na waheshimuni kwa kuwa ndio wanaendesha serikali kwa kodi zao.
 
Haya mambo ndio yanawauma upinzani, walipenda wawe wanayaibua alafu wanashinikiza hatua zichukuliwe, kwao ata kama ayajachukuliwa hatua furaha inakua kwao.. Maana sasa hivi utasikia wanafanya reference kua, awamu iliopita tulikua huru kukosoa(Ata kama hatua zilikua hazichukuliwi).

JPM yeye anachukua hatua kweli kweli hata kama ulikwepa kodi Mwaka 2005, fail likifika kwa JPM linachukuliwa hatua.. HAPA KAZI TU

Ndio maana CCM ilimweka JPM ilikuiludisha Nchi katika mstari.. Serikalini Nidhamu imerejea kwa kishindo

Naona Sasa Taifa limekua kali katika issue ya kodi kama ulaya.. Maana ulaya hawana mswalie katika issue ya kodi, ata kama itapita miaka ishirini, wakikugundua tu.. Utalipa tu..
 
Shukrani mkuu kwakunielimisha
 
Vp na Lugumi kapewa 90 days? Acha maneno ya kwenye kanga angalia uhasilia, huyu anapewa siku 90 huyu anatumbuliwa hapohapo bado unasifia? Dah mchangiaji uchwara hongera

Ni baada ya Kamati ya Bunge iliyopewa kazi ya kufuatilia Sakata la Lugumi kuthibitisha kuwa vifaa mashine hizo zimefungwa katika vituo vyote.

Agizo hilo limetolewa na Bunge kupitia kwa Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson wakati akiahirisha Bunge la 11 leo mjini Dodoma
==========

Habari wakuu,

Leo akihitimisha bunge, naibu spika ametolea ufafanuzi utekelezaji wa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa alama za vidole(AFIS), hoja iliyojengwa kutokana na mkaguzi wa hesabu za serikali(CAG) kwa kutokamilika kwa mradi huo.

Agizo la bunge lilimtaka afisa masuhuli wa jeshi la polisi kuhakikisha mfumo wa AFIS unafanya kazi ndani ya kipindi cha miezi sita. Ripoti ilieleza mfumo wa AFIS ulikuwa unafanya kazi katika vituo 14 pekee kati ya vituo 108 hivyo agizo la kamati halikuwa limetekelezwa kikamilifu.

Spika ametoa agizo kwa serikali kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi ndani ya miezi mitatu ili kuboresha uwezo wa jeshi la polisi kuwa na utambuzi wa haraka wa wahusika wa matukio ya kihalifu katika vituo vyote nchini. Pili masuala yote yaliyobainika kuwa na dosari za kiutendaji yapatiwe ufumbuzi haraka.

Spika anatarajia sasa suala hilo litafikia mwisho na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali atafunga hoja yake baada ya kujiridhisha na utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa.
 
"Makampuni hayo yamekuwa yakinunua risiti za manunuzi bandia kutoka kwa watu wanaomiliki mashine za kielektroniki (EFDs) ambazo hazijasajiliwa na kuzitumia risiti hizo kudai marejesho ya VAT bila kuwepo na bidhaa au huduma halisi iliyouzwa au kutolewa na muhusika, kitendo ambacho kinainyima Serikali mapato stahiki kwa mujibu wa sheria".

sijaelewa hapo "kudai marejesho ya VAT" Ipoje?
 
HIYO FARM PLANT, NINGEPENDWA IMELIKWE TENA KWA ILE DARUBINI YA VIRUSI HATARI,MANAKE KUNA TETESI YEYE NDIO BINGWA WA kuchezesha VAT.alikuwa na mahela yako fixed kwenye mabenki chungu nzima.ningeomba waanze kunusa pale Eqity bank ndio wangeanza na dot a.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom