Kampuni 4 zabainika kukwepa kodi Sh. Bilioni 29.2. SKOL, A. M Steel wamo...

Kosa lilikuwa likifanyika kati ya mwaka 2010 na 2014. Limegunduliwa hivi sasa tu na serikali ya sasa. (Serikali ya wakati huo ilikuwa haikuligundua). Kwa hiyo uchunguzi zaidi unaendelea. Kuna nini kigumu kukielewa hapo? Au ni kwa sababu mawazo yako yamekaa kuikosoa serikali tu ya sasa ndiyo maana kila kitu kinachofanywa na serikali ya sasa unatafuta cha kuikosoa.
Kwani ukinielekeza bila kuniwekea mawazo yako kichwani mwangu utakosa nini? Hebu nionyeshe ni wapi nimeikosoa serikali hii au hata iliyopita? Mimi nikielewa jambo huwa natoa mapendekezo, sio kukosoa japo naamini pia katika kukosoa.
 
Mkuu mfanya biashara aliyeandikishwa kwa VAT, either kampuni au mtu binafsi anatakiwa kwa kila mwezi aliofanya biashara alipe VAT kama aliuza zaidi ya vile alivyonunua au kama kwa kipindi cha miezi sita mfulilizo amekuwa akinunua bidhaa au huduma zaidi ya anazouza anatakiwa arejeshewe na TRA ile VAT ambayo atakuwa amelipa zaidi kwenye manunuzi kulinganisha na mauzo. Ni vema kujua kuwa VAT inayolipwa au kurejeshwa ni net amount ya VAT rate, ambayo ni 18% kati ya mauzo na manunuzi kwenye mwezi husika.

Mfano kama mwezi wa tano 2016, mfanya biashara alinunua bidhaa za shilingi 100,000,000 akajumlisha 18% VAT ambayo ni 18,000,000 jumla ya malipo kwenye manunuzi itakuwa 118,000,000. Kama mwezi huo aliuza bidha za shilingi 120,000,000 kabla ya VAT atakuwa amepokea 18% ya kiasi hicho kwa niaba ya serikali ambayo ni sawa na shilingi 21,600,000 hivyo net amount ambayo anatakiwa kuwasilisha TRA kwa mwezi huo ni shilingi 21,600,000 - 18,000,000 = 3,600,000

Inaonekana haya makampuni yalikuwa yanashirikiana na wafanyabiashara ambao wanawapa risiti za EFD bila kununua mizigo au kutoka huduma ili ionekane kuwa wamekuwa wakinunua zaidi ya kuuza hivyo kudai marejesho

Ni vema tukalipa kodi sahihi tujenge nchi yetu
Ambacho sielewi ni pale Rais aliposema huyo mfanyabiashara fisadi anakata kodi ya 5% badala ya 18% kwa hiyo serikali inakosa mapato ya VAT ya 18% plus 5%.

Nilidhani loss kwa serikali ingekuwa 13% (18% inayotakiwa minus 5% ambayo imelipwa) plus 18% za fake claims ambazo TRA imelipa rejesho hewa, kwa hiyo jumla ya loss kwa TRA inakuwa 31% ya kila muamala na sio 23% aliyosema Rais.

Au kama ile 5% ni kodi feki na haifiki serikalini basi loss kwa serikali ingebidi iwe 18% iliyotakiwa kulipwa plus another 18% ya fake claim ambayo TRA imelipa rejesho hewa. Jumla ya loss kwa TRA hapa inakuwa 36% kwa muamala.

Sasa sijui Rais ame calculate vipi hiyo loss ya 18% plus 5%.
 

Nilidhani loss kwa serikali ingekuwa 13% (18% inayotakiwa minus 5% ambayo imelipwa) plus 18% za fake claims ambazo TRA imelipa rejesho hewa, kwa hiyo jumla ya loss kwa TRA inakuwa 31% ya kila muamala na sio 23% aliyosema Rais.
Mkuu unachosema hapa ni kweli lakini hata hivyo hiyo 5% haijafafanuliwa vizuri?
 
kumbe basi ilikuwa inasaidia,kama hela ilikuwa inatirika mpaka chini,inamkuta mwenye bar,inamkuta mwenye toroli au suziki carry ya kubebea kreti za bia,inamkuta barmaid anaeenda shuleni kumlipia mwanawe ada,inamkuta mwenye shule anaenda sokoni kununua mchele na maharage wanafunzi wake,inamkuta wa gengeni hadi mkulima,
nakwambia mtafunga mkanda mpaka viuno viwe vyembamba kama vya nyigu mwakahuu
leo umekunya madini adimu
 
Nyumbu wala hawayaoni haya.

Chadema kwa miaka 20 wamepanga jengo chafu pale ufipa.!! Lkn ukihoji sababu ni nini unaambiwa wewe ni msaliti!!
 
Kuna siku jamaa mmoja alikuwa ananiulizia kama nina risit hizi za electronic tra. Kumbe ndio kazibzake hizo? Yaani anachukus risiti zangu mimi anajifanys km yeye ndoye kanunua ,sasa sijui wanazifanyia nini!
 
Kuna siku jamaa mmoja alikuwa ananiulizia kama nina risit hizi za electronic tra. Kumbe ndio kazibzake hizo? Yaani anachukus risiti zangu mimi anajifanys km yeye ndoye kanunua ,sasa sijui wanazifanyia nini!

Anaenda kudai refund! Atajifanya kanunua hivyo kalipa VAT hivyo kama ni VAT registered atarejeshewa alicholipa, au kama sio kurejeshewa atapunguza alichotakiwa kulipa TRA
 
Mazingira ya biashara Tanzania ni mazuri na kodi si nyingi...kama kodi zinakwepwa kwa namna hiyo mazingira yatakuwaje mazuri. Mi sipendi ubaguzi ila nahisi wafanya biashara wengi wa Tz si tu kwamba hawana uzalendo bali si wazalendo kwa maana halisi na hivyo hawaoni haja ya kulipa kodi. Kusema mazingira si mazuri mi naona ni kuionea Tz maana hiyo pesa inayokwepwa ndiyo ingeweka mazingira mazuri sasa yatatoka wapi mazingira mazuri na pesa zinaibwa? Mara online payment ya bilioni 7 kila siku, mara bomba la mafuta meta haisomi..mara hiki mara kile pesa ya kuweka mazingira safi itatoka wapi? Sheria za kodi zitumike kwa nguvu zote, nenda ukwepe kodi ulaya halafu tuaona au America...! Sisi ni shamba la bibi ndo maana kila mtu anataka kufanya biashara kwa kuwa ni namna ya kukusanya mapato ya serikali kwa faida yako mwenyewe suala lililo hatari kwa ustawi wa nchi yetu. Walipe, wafilisiwe, wanyang'anywe leseni za biashara hapa kwetu. Adabu itafuata baada ya kuona madhara ndivyo wanadamu tunapenda kujifunza
 
Anaenda kudai refund! Atajifanya kanunua hivyo kalipa VAT hivyo kama ni VAT registered atarejeshewa alicholipa, au kama sio kurejeshewa atapunguza alichotakiwa kulipa TRA
I see! Ila kwa kweli ukwepaji kodi ktk hii umekuwa mkubwa sana hasa kwa sababu viongozi wakubwa wamekuwa wanasaidia ssna hili!
 
Amini amini nakwambia, ikiwa kizazi hiki hakijabarikiwa uwezo wa kuelewa umuhimu wa "u dikteta" wa rais Magufuli, basi kizazi kijacho kitaelewa!
Hapo uko sawa mkuu! Wakiendesha nchi kwa style wanayotaka wao, mwisho wa siku mtabaki masikini wa kutubwa huku ughaibuni wanakula mali zenu nyie mnabaki mnanyoosha mikono kuwaomba,na upo uwezekano wa wao kuwaomba sababu mna kila kitu; bali tu viongozi wa kuwawezesha kuvitumia ipasavyo
 
Mkwepa kodi ni adui namba moja ndani ya nchi yeyote,watu wanaongea kuhusu haya makampuni ya wakwepa kodi,makampuni kama home shoping centre walitajwa wakabadili jina la kampuni kuitwa GSM,tuwe makini watanzania wote kila mtu aisaidie serikali tupate huduma bora,hatutaacha kuomba misaada kama akina GSM wanahamisha majina na assets zao kwenda nje ya nchi kupitia bureau de change zao.Tanzania ni yetu kwa pamoja tushirikiane kutokomeza wakwepa kodi
 
China wananyongwa na kupigwa risasi watu kama hawa JPM anyonge wakwepa kodi wataano tu wanatosha kubadili mwelekeo wa nchi yetu na kila mtu atajua umuhimu wa kodi
 
Si kila mashine ni ya vat?? Hata ukija dukani kwangu naweza kukupa hata risiti tano nikijua kuna wateja zaidi ya 5 ambao hawatadai risiti...
Kulipa kodi ni uzalendo na maamuzi ya mfanya biashara...anaweza kukwepa na asikamatwe...serikali wekeni mazingira mazuri kwa wafanya biashara ... Punguzeni rundo la kodi lisilo na lazima...na waheshimuni kwa kuwa ndio wanaendesha serikali kwa kodi zao.
Sasa nchi yetu imejaa wafanyabiashara wahindi ndo wakubwa na hao ni wa kutupia jicho la Tatu wengi watanielewa Kama Unafanya manunuzi makubwa huwa wanauliza kutoa Buddhaa bila recept uzalendo wao ni mdogo mno na Nahsi wametuambukiza sana kwani wana longo longo nyingi hawa jamaa
 
Hivi mabank yetu hapa Tanzania yana sheria gani ya kuisaidia Tanzania katika masuala ya kodi. Nchi zilizo Makini hizi financial institutions ni whistle blowers wa kwanza. Huwezi ingiza ma hela tu hayajulikani yametoka wapi . Movement ya hizi pesa yanafanyika wapi Kama si Kwenye mabank yetu mi nadhani serikali iangalie issue ya hizi institutions izidhibiti haswaa pindi zinapoonekana ku assist loss Kwa seeikali ndo ziwe za kwanza kupewa somo.
 
Mkuu unachosema hapa ni kweli lakini hata hivyo hiyo 5% haijafafanuliwa vizuri?
Right, katika ufafanuzi wa TRA hicho kitu cha 5% alichokisema Rais hakipo, Rais amejitungia kichwani mahesabu alivyoelewa yeye na amechemka.

Hiyo fake VAT ya 5% itakuwa ni malipo ya wafanyabiashara kama mlungula kwa huyo Godfather wao anaetengeneza fake claims, haiendi serikali kwa sababu hauwezi ku submit a 5% VAT charge.

Kwa hiyo serikali inapoteza 36% ya miamala, ambayo ni 18% inayotakiwa kulipwa hailipwi PLUS 18% inayodaiwa fake claims na kulipwa kutoka TRA.
 
Right, katika ufafanuzi wa TRA hicho kitu cha 5% alichokisema Rais hakipo, Rais amejitungia kichwani mahesabu alivyoelewa yeye na amechemka.

Hiyo fake VAT ya 5% itakuwa ni malipo ya wafanyabiashara kama mlungula kwa huyo Godfather wao anaetengeneza fake claims, haiendi serikali kwa sababu hauwezi ku submit a 5% VAT charge.

Kwa hiyo serikali inapoteza 36% ya miamala, ambayo ni 18% inayotakiwa kulipwa hailipwi PLUS 18% inayodaiwa fake claims na kulipwa kutoka TRA.
Inawezekana ndio alichokuwa anamaanisha Magufuli huyu anayeuza ana charge 5% lakini hakakosea kuijumlisha kwenye 18%.
 
Sijajua wewe unaesema kwamba Rais ni godfather na claim zake ni fake unamanisha nini?hujafanya research usiongee wanaoharibu Tanzania ni wahindi ni ukweli ukitaka omba ushahidi utapewa,sio kuongeaongea tu. Lete fact ndugu kama kweli wewe.mtanzania halisi
 
Back
Top Bottom