Kampuni 25 zilizochota CIS kufilisiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni 25 zilizochota CIS kufilisiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Feb 24, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,694
  Trophy Points: 280
  Kampuni 25 zilizochota CIS kufilisiwa
  Theopista Nsanzugwanko
  Daily News; Monday,February 23, 2009 @19:28

  Kampuni ya Msolopa Investment Limited iliyopewa jukumu la kukusanya madeni ya Sh bilioni 199 zilizochotwa serikalini kupitia mpango wa Uagizaji wa Bidhaa Nje (CIS) imeomba ulinzi wa polisi kwa ajili ya kukamata na kutaifisha mali za kampuni 25 zinazodaiwa deni hilo.

  Wakala huyo alitoa wiki mbili kwa baadhi ya wabunge na mawaziri wakiwamo wastaafu 40 ambao kampuni zao zimetaifishwa pia kuchota pesa hizo wawe wamelipa vinginevyo, atawaanika katika vyombo vya habari sambamba na kutaifisha mali zao.

  Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Ibrahim Msolopa alisema kati ya kampuni 30 (tofauti na hizo za wabunge na mawaziri) zilizopewa wiki mbili kulipa madeni hayo, kampuni tano pekee ndiyo zilijitokeza kuanza kulipa madeni.

  Alizitaja kampuni tano zilizoanza kurejesha fedha kuwa ni Shela Beach Investiment, Chichi Enterprises, Paninye Investments, Simba Resources na Avicena Pharmaceutical.

  Kampuni 25 ambazo wamiliki wake wameendelea kukaa kimya ambazo alisema zitakamatwa wakati wowote baada ya kupata ulinzi wa Polisi, ni Kiex Trading inayomilikiwa na Rajabu Maranda ambaye anatuhumiwa kuchukua fedha za Akaunti za Madeni ya Nje (EPA) na mfanyabiashara Andrew Traders.

  Nyingine ni K. Agencies International, Chawe Transport, Sikute Enterprises, Danico Ltd, Apemac, Dar es Salaam International School Trust Fund, Oriental Transport, Auxi Pharmaceutical, Family Care Clinic Pharmacy, Aliya Investiments, Agriculture Sales, Kashif Traders na Rein.

  Alizitaja kampuni nyingine kuwa ni Twins Investments, Road Conqueres, Getca International, Dodoma Oil Mills, Shivji & Sons, Tyre Centre, Rela Investments, Amazon Trading, Transport Import & Export na Pharmavet. Kwa mujibu wa Msolopa, wameshamwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kuomba ulinzi kwa ajili ya kuendesha operesheni hiyo ya kukamata kampuni hizo.

  Alisema baada ya kumaliza kukamata na kutaifisha mali ili kufidia madeni, ifikapo Machi 15 mwaka huu, wataanza kukamata mali za mawaziri na wabunge walioko madarakani na waliostaafu, ambao wako ndani ya kundi la kampuni 40 waliokaidi kulipa madeni.

  Alisema mawaziri na wabunge wanaendelea kulipa fedha zilizochotwa na wengine walianza kulipa baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwafuata bungeni katika Mkutano wa Bunge uliopita lakini wapo ambao hawalipi kabisa licha ya kuwa na taarifa za kudaiwa.

  Akizungumzia kiasi cha fedha kilichokusanywa mpaka sasa, Mkurugenzi huyo alisema wameishawaandikia makamishna wa sehemu nne zinazotumika kulipia madeni, ili kutambua kiasi cha fedha kilichokusanywa ambacho watakitangaza kwa umma ili kukifahamu baada ya kampuni hiyo kuanza kazi ya kukusanya madeni hayo.

  Alisema wadaiwa wa fedha hizo hulipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), benki za NMB, CRDB na ya Rasilimali Tanzania (TIB). Alisema serikali ilizikopesha kampuni 916 Sh bilioni 199 kwa lengo zuri lakini zilitumika kwa madhumuni yasiyokusudiwa, kampuni zingine 80 zilikuwa zimeishalipa fedha zilizokopa na nyingine ziliendelea kulipa isipokuwa hizo 30.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ukusanyaji huu wa hela za CIS -- siyo usanii tu kama vile 'urejeshaji' wa mapesa ya EPA? hatuambiwi walidaiwa ngapi na wamerejesha ngapi?
   
 3. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wanafilisi makampuni ya kwenye briefcase?

  Hii kali............
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,205
  Trophy Points: 280
  Halafu wanatwambia kuna Mawaziri na Wabunge lakini hawataki kuwataja!!! Hawa ni wezi tu wameiba mabilioni ya pesa na kamwe hawakustaili hata kupewa nyadhiza walizokuwa nazo lakini wanafichwa kama kawaida ya serikali iliyo madarakani ili kuwakingia vifua mafisadi!!!
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Huyu mjomba wake Zitto, inaonekana ni MAFIOSO wa kutupa. Khe!
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Watuandikie majina ya kampuni, wamiliki wake pia majina ya wabunge na mawaziri na kampuni zao au kama ni wao wenyewe na kiasi ambacho kila kampuni/wazrir/mbunge inadaiwa/anadaiwa kama ilivyokuwa kwa EPA. Kama zoezi ni transparent we want also wamiliki awekwe hadharani. Ni hila tu wakuu.
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Please, justify to wana Jamii Forum na umma wa Watanzani akuwa fisadi Maranda ni mjomba wa Zitto. Kutoka mkoa au wilaya au kijiji kimoja si ujomba huo. Kazi kweli kweli yaani extended family ya ajabu hiyo which includes parents, children, aunts, uncles, cousins, neighbours, villagers, ward members, district and regional citizens!!!!! Kweli bado tuna damu au mabaki ya Siasa ya Ujamaa na kujitegema kuwa tu wamoja na kukawa na ndoto la kuifanya africa moja (Kwame na Nyerere ndoto).

  Zitto ni mpiganaji na mpinga mafisadi na asihusishwe na mafisadi hata kama ni ndugu kama unavyodai (mjomba). Wizi wa relative has nothing to do with any member of the family.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  @ #7,

  Muzee mbona unaongea kwa jazba mpaka mate yanakutoka?

  Niliwahi kusoma gazeti fulani (bahti mbaya silikumbuki jina lake vyema, lakini nadhani ni la kiswahili) kuwa wakti hawa watuhumiwa wa EPA wanaanza mchakato wa Kisutu, wabunge wawili wa CHADEMA waliripotiwa kuwawekea dhamana baadhi ya watuhumiwa, mmojawapo akiwa Mh. sana Zitto Kabwe, hata hivyo alipoulizwa aliripotiwa kujitetea kuwa Maranda ni mjomba wake. Mkuu hiyo ndo background niliyonayo. Lete ya kwako.

  Haya mengine ni yako, hivyo wewe ndiye unayetakiwa kuyatolea maelezo.
   
 9. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  sidhani kama ni mwanahalisi. nafikiri gazeti lenyewe ni rai au raia mwema.

  kwenye habari hiyo ambayo ilianzia ukurasa wa kwanza na ikaendelea ukurasa wa pili kama sikosei iliandikwa kuwa mheshimiwa zk aliendelea kunong'ona kitu na miranda pale kisutu (siku ya kesi ya miranda) mpaka mheshimiwa hakimu akampiga mkwara. na zk alipoulizwa uhusiano na huyo jamaa alisema ni mjombake
  kwenye habari hiyo kiongoz mmoja wa cuf alikuwa anaelezea kuwa viongoz wa chadema wako karibu na ufisad/mafisad baada ya huyo zk kuonekana na miranda, mheshimiwa mwingine wa chadema wa kike kuonekana na mtuhumiwa mwingine na mwenyekit wao mbowe 'kujaribu' kumhonga (1m) mmoja wa watu wa cuf ili aingie chadema
   
 10. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hiyo Kampuni (in red) sina hakika kama bado ipo maana hao ndiyo walimiliki yale mabasi ya MATEMA BEACH. Nina hakika Makampuni mengi kati ya hayo yameshafilisika na yaliunda kwa makusudi ya kuchota hizo pesa kama yalivyoundwa Makampuni ya kuchota EPA!

  Yaani Nchi yetu inanishangaza sana, sidhani kama tumeshapata viongozi halisi kama ilivyokuwa Mwalimu Nyerere. Yaani Wanasiasa wetu wanapigania kuingia Madarakani kwa hali na mali, wakishaingia madarakani hamna wanachofanya (angalau JK anapambana na ufisadi potelea mabli madai ya kuwa ni Kampeni au hana namna ya kuepuka). Na sitashangaa kusikia kuwa wengi wa wamiliki wa Kampuni hizo ni Wanasiasa na waliunda Kampuni hizo kuchota pesa kwa ajili ya kupigania madaraka ya Kisiasa.
   
 11. E

  Edo JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Aliyemtembelea maranda Ni Dr Amani Walid Kaburu (ex-Chadema, kigoma MP) mwakilishi wa CCM bunge la afrika mashariki
   
 12. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2009
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ikiwa kweli mfilisi anajua kazi yake ya nini kutangaza kuwa kesho nitaanza kufilisis so and so? Alitakiwa afanye kazi yake mara moja na kuarifu nani wamekamatwa nani amekaidi nk. Unamwarifu mhalifu? Hainiingii kichwani.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2013
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hapa patamu sana/
   
 14. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #14
  Nov 6, 2013
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,550
  Likes Received: 1,601
  Trophy Points: 280
  jambo hili, cjui limefikia wapi............... na hamna hatua zilizo chukuliwa ?/!
   
Loading...