Kampuni 13 jijini Dar es Salaam zakiuka mkataba ya kufanya biashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni 13 jijini Dar es Salaam zakiuka mkataba ya kufanya biashara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jul 28, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,272
  Likes Received: 5,635
  Trophy Points: 280
  Kampuni 13 jijini Dar es Salaam zakiuka mkataba ya kufanya biasharaNa Zaina Malongo

  KAMPUNI 13, jijini Dar es Salaam zimebainika kufanya biashara kinyume na taratibu za miktaba waliosaini na Serikali.

  Akipokea ripoti, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam William Lukuvi kutoka kwa Afisa biashara ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi, Mntambo Mhina alisema serikali imeanza mkakati wa kuwachukulia hatua wafanyabiashara hao.

  “Maeneo ambayo kampuni hizo, zimekutwa zikifanya biashara kinyume na taratibu ni maeneo ya Kariakoo, Gongolamboto, Mtaa wa Swahili Ilala,Tandika Muembe yanga,Vingunguti na Msimbazi.

  “Serikali inaendelea kufanya uchunguzi zaidi, tunaweza kugundua kampuni nyingine ambazo pia zinaendelea kufanya shughuli za biashara kinyume na hata kuvunja sheri ya nchi,”alisema Lukuvi.

  Alisema tarifa hiyo, itapelekwa katika ofisi ya Waziri Mkuu ili hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya wahusika wa kampuni hizo.

  Serikali itaendelea kutoa vibali kwa wakufanyabiashra kama kawaida ili kukidhi mahitaji mbalimbali. Lukuvi alisema kamati hiyo, iliundwa Juni mosi mwaka huu, na kwamba ina watu 16 ili kufanya uchunguzi.
   
 2. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Tuzifungea na hizi....
   
Loading...