PRESS RELEASE
Taarifa iliyochapishwa na Gazeti la DIRA leo Jumatatu, tarehe 13 Juni, 2016, ukurasa wa mbele yenye kichwa cha habari: MWAKYEMBE ATUHUMIWA KUTAPELI BIL.2, ni taarifa ya kizushi na upotoshaji wa makusudi yenye lengo la kumchafua Dk. Harrison Mwakyembe katika suala lisilomhusu, bali kampuni ya Power Pool E.A. Limited ambayo yeye si kiongozi wala mwana hisa. Inasikitisha kuwa gazeti la DIRA linatumika kama kipaza sauti cha kuchafua watu bila kuzingatia misingi ya uandishi wa habari ya ukweli na haki.
Uongozi wa Power Pool unamfahamu sana Chris Chae aliyeingia nchini miaka kadhaa iliyopita kwa kujitambulisha kuwa raia wa Korea ya Kusini na ndugu wa karibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bahn Kin-Moon, wasifu ambao si wa kweli.
Power Pool haitaki malumbano kwenye magazeti, ila inamtaka Chris Chae atangulie mahakamani ili kutenganisha pumba na mchele badala ya kutumia magazeti dhaifu kupotosha ukweli na kuchafua watu bila sababu za msingi.
Isaac Mwamanga,
Mwenyekiti Mtendaji,
Power Pool E.A. Limited.