Kampumi ya migodi Ashanti kusaini mkataba mpya wa madini
Na Mwandishi Wetu
MAJADILIANO yaliyodumu kwa takribani mwaka mmoja sasa baina ya Serikali na kampuni ya uchimbaji madini ya Anglogold Ashanti (AU) ya Afrika Kusini kuhusu mkataba mpya wa madini, sasa yamekamilika na mkataba huo unatarajiwa kusainiwa wakati wowote kuanzia sasa.
Pamoja na mambo mengine, mkataba huo mpya umeifutia kampuni hiyo msamaha wa kodi baada ya kufanya kazi zake nchini kwa miaka kadhaa sasa.
Jarida la Dow Jones Newswires limesema katika toleo lake la Jumatatu wiki hii kuwa mkataba huo mpya utasainiwa siku yoyote wiki hii jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo jarida hilo lililotoa taarifa hiyo kwa kumnukuu afisa mmoja wa Wizara ya Nishati na Madini linasematangu mwaka jana, Tanzania imekuwa ikipitia mikabata yote ya madini nchini kwa lengo la kuiboresha na kuifanya sekta ya madini ili kulinufaisha taifa zaidi kuliko wawekezaji.
Kukamilika kwa makubaliano hayo kumekuja muda mfupi baada ya serikali kupitia upya mikataba yake na kampuni za madini za Barrick Gold Corp (ABX) ya Canada na Resulute Mining Ltd (RSGAU) ya Australia.
Katika mikabata hiyo mipya makampuni yote ya madini nchini yatatakiwa kuilipa serikali hadi dola za Marekani 200,000 kwa mwaka ambazo ni pamoja na asilimia 15 ya kodi ya mgodi na asilimia 30 kodi inayotokana na mauzo ya madini kutoka kwenye mgodi husika
Kampuni ya AngloGold Ashanti ndiyo mmiliki wa mgodi wa Geita ambao ni mkubwa kuliko yote nchini ukiwa na uwezo wa kuzalisha hadi uzani wakia 600,000 za dhababu kwa mwaka.
Kwa ujumla wake Tanzania inazalisha kiasi cha wakia 1.75 milioni za madini kwa mwaka ikiwa inashika nafasi ya tatu barani Afrika baada ya Afrika Kusini na Ghana.
Source: Mwananchi