Kampeni zimepamba moto uzini CCM na Chadema vikichanja mbuga

​kuna mpambano mkali katika kampeni za mitaa kwa mitaa huku vyama viwili vikichuana kwenye kunadi sera na wagombea, na mashindano makubwa yanaelekea kubadilika kutoka CCM na CUF na kuwa CCM na Chadema

Mpambano kutoka CCM na CUF? No. Sasa hivi ni mpambano wa CCM, CUF (a.k.a CCM B) au kwa ufupi vyama vinavyoshika dola vikipambana na wapinzani CHADEMA.
 
Naona ...Mwalimu Slaaa...ameweka kambi kule ...anatoa ILMU ..taratibu...hajali kelele hata mkisema anahutubia watu kumi...hajali...,ajabu ni kuwa siku hadi siku wahudhuriaji wa mikutano ya chadema zanzibar wanazidi kuongezeka........unajuwa ukiangalia ratio......jimbo kama Arusha mjini lenye wapiga kura 600,000 ..ukifanya mkutano wakahuhuria watu 10,000 bado hustahili kutamba........,ila zanzibar jimbo lenye wapiga kura 3,000 ....ukapata wahudhuriaji 100 kwenye mkutano wako ...hao ni wengi kuliko wale 10,000 waliohudhuria Arusha........ukizingatia hawajasombwa kwa malori...so somo linaingia taratibu kama dawa....!!
 
si kazi rahisi kuamini kwamba chadema kiko juu ya CUF kule znz maneno matupu hayavunji mfupa. JF sio gazeti la udaku hapa kuna vichwa shuka nondo na sisi tutakuuliza maswali.
Sijaelewa umeandika kitu gani hapo kwenye red,

Kwamba, HAUAMINI,
Kwamba, NI KAZI SANA KUAMINI
Kwamba, UMETISHIKA?
Kwamba, kama ni kweli UTAVUNJIKA MIFUPA?

Wewe umeolewa au umeoa? yani namaanisha wewe CUF au CCM?
 
Sijaelewa umeandika kitu gani hapo kwenye red,

Kwamba, HAUAMINI,
Kwamba, NI KAZI SANA KUAMINI
Kwamba, UMETISHIKA?
Kwamba, kama ni kweli UTAVUNJIKA MIFUPA?

Wewe umeolewa au umeoa? yani namaanisha wewe CUF au CCM?

Huyo jamaa anaonekana ni gamba lililo jaa ukurutu mpaka linanuka
 
Hebu weka sawa kumbukumbu hapa.........wewe CUF au CCM?

Haueleweki wewe; Hatuelewi umeoa au umeolewa?
jamani daaa kwa hiyo hatuwezi kutofautisha kati ya ccm na cuf nimecheka mpapa basi duuuu!
 
Siasa za TZ ni siasa za ugomvi. Ujinga mwingi ukiziangalia alafu maarifa kiduchu. Na wakati mwingine wahusika ni watu wenye heshima

katika jamii. Wagombea hawana vipaji wala uchungu na nchi. Wanauzi, wao wanachopenda ni kuitwa mheshimiwa na

usipomtambulisha hivyo unaweza ukafutwa uanachama, ha ha ha! Tushapoteza muelekeo siku nyingiiiiii. Hahuna cha nationalism wala uo u.hu.ru! Ngoja tuone wantupeleka wapi?
 
kuna mpambano mkali katika kampeni za mitaa kwa mitaa huku vyama viwili vikichuana kwenye kunadi sera na wagombea, na mashindano makubwa yanaelekea kubadilika kutoka CCM na CUF na kuwa CCM na Chadema

cuf ni ccm
 
Hakika kila dalili zinaonyesha cuf watashindwa vibaya.Kama haki ikitendeka CDM wanachukua jimbo
 
CHADEMA naona munajikweza sana lakini mwisho wa siku kuna Kura zenu only 30 zinawasubiria!

yanayowapata cuf yatawapata na waume zao ccm muda si mrefu kwa kuwa haki ya mtanzania kamwe haitadhurumiwa bali itacheleweshwa tu but time ikifika kitaeleweka dhuruma zote zitatokomea, mungu ibariki tanzania na wabariki watanzania tunaodhurumiwa na kuibiwa ndani ya taifa letu na hao wanaojitangazia kuwa wanahuruma na uchungu kwa watanzania!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom