Uchaguzi 2020 Kampeni zimeanza kimyakimya ama ni matumizi mabaya ya ofisi?

Mheikungu

JF-Expert Member
Oct 15, 2018
214
448
Heshima na taadhima kwenu wakuu.

Nimekaa naangalia runinga hapa kwenye kituo cha Star Tvkipindi kinaitwa Agenda 2020. Anahojiwa Waitara hapa naona kichefuchefu:

1. Anaonekana amelewa chakari, kimaadili kwa kiongozi kama yeye alipaswa aheshimu maadili ya hadhira kwa ujumla.

2. Kwa kutumia kofia ya unaibu waziri ametangaza kuachana na jimbo la Ukonga. Ametangaza rasmi kuwa anaenda kugombea jimbo la Tarime vijijini.

Kwangu mimi hii naona ni kampeni ya wazi kabisa. Kwa sasa jambo ambalo linawanyima haki raia wengine wenye kutaka kutia nia lakini hawana uwezekano wa kuonekana runingani.

Naomba nijuzwe labda nipo nyuma ya wakati kama kampeni zimefunguliwa na mimi nikatangaze nia huko Mchambawima kwetu.
 
Hata mimi nimeshangaa Waitara kuanza kampeni kabla ya wakati....... Huu siyo utaratibu uliozoeleka ndani ya CCM.

Anachokifanya Waitara na Nyanda ndio hicho hicho kilifanywa na Lowassa na viongozi wa dini mwaka 2015!
 
Kama alihama cdm kisha akateuliwa na genge la mwenyekiti wa ccm kugombea kwa tiketi ya ccm, unashangaa nini hivi sasa akifanya anayoyafanya?

Unajua makubaliano yake ya kuhama cdm na kuhamia ccm yalikuwa yapi? Mliamua kukaa kimya mkijua wapinzani ndio watadhurika, saa hizi mnakutana na matunda ya siasa chafu mnalalamika ni machachu!

Maadamu mmefumbia macho siasa chafu dhidi ya wapinzani, tarajieni vituko zaidi.

Heshima ilikuwepo ndani ya ccm maana ilikuwa inafanya siasa, hivi sasa rais ndio anaamua nani awe kiongozi, utaratibu ufuatwe ili iwe nini?
 
Heshima na taadhima kwenu wakuu.

Nimekaa naangalia runinga hapa kwenye kituo cha Star Tvkipindi kinaitwa Agenda 2020. Anahojiwa Waitara hapa naona kichefuchefu:

1. Anaonekana amelewa chakari, kimaadili kwa kiongozi kama yeye alipaswa aheshimu maadili ya hadhira kwa ujumla.

2. Kwa kutumia kofia ya unaibu waziri ametangaza kuachana na jimbo la Ukonga. Ametangaza rasmi kuwa anaenda kugombea jimbo la Tarime vijijini.

Kwangu mimi hii naona ni kampeni ya wazi kabisa. Kwa sasa jambo ambalo linawanyima haki raia wengine wenye kutaka kutia nia lakini hawana uwezekano wa kuonekana runingani.

Naomba nijuzwe labda nipo nyuma ya wakati kama kampeni zimefunguliwa na mimi nikatangaze nia huko Mchambawima kwetu.
Wewe Kunywa bia barabara itakusaidia nini
 
Back
Top Bottom