Kampeni zamng’oa Mkurugenzi Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni zamng’oa Mkurugenzi Arusha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Sep 19, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kampeni zamng’oa Mkurugenzi Arusha

  Harakati za uchaguzi mkuu jimbo la Arusha, sasa zimechukua sura mpya baada ya kuhamishwa ghafla Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Raphael Mbunda katika mazingira yanayohusishwa na siasa.

  Mbunda, mmoja wa wakurugenzi wa muda mrefu nchini, amehamishwa ghafla kwenda ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na amepewa siku tatu tu kuachia ofisi yake kinyume na taratibu za serikali za kupewa siku 14 kujiandaa kuondoka.

  Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais tawala za Mikoa (TAMISEMI), Selina Kombani aliliambia gazeti hili kuwa uhamisho huo kuhusishwa na siasa akisema ni uhamisho wa kawaida.

  “Uhamisho huo ni wa kawaida kama wengine wanavyohamaishwa kwa hiyo sioni kama ni habari,” alisema Kombani.

  Alifafanua zaidi kuwa Mbunda hana tatizo lolote linalohusiana na uhamisho huo na kwamba atapangiwa kazi nyingine nzuri.

  Hata hivyo baadhi vyanzo vyetu ndani ya manispaa hiyo vinaweka wazi kwamba uhamisho huo unatokana na vuguvugu la kisiasa.

  “Jambo hili ni la ajabu sana hata kama mtu ana makosa si anaheshima yake. Mbunda amekuwa Arusha muda mrefu kabla ya kuwa Mkurugenzi katika halmashauri mbalimbali halafu wanamhamisha kama mwizi… Hii sasa inatufikisha wapi,” alisema mtumishi mmoja wa Manispaa ya Arusha kwa sharti la kutotajwa gazetini.

  Mkurugenzi huyo, katika siku za karibuni, alitupilia mbali mapingamizi ya kumuondoa mgombea wa Ubunge wa Chadema jimbo la Arusha, Godbless Lema kwa tuhuma za kumchafua na kumdhalilisha mgombea wa CCM.

  Habari za uhakika kutoka ndani ya halmashauri za Arusha zimebainisha kuwa nafasi ya Mbunda sasa inachukuliwa kwa muda na na ofisa kutoka ofisi ya mkoa wa Arusha, Estonmi Chang’ah ambaye alikuwa idara ya serikali za mitaa……..

  Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili


  My take: Hivi Tume ya Uchaguzi iliafiki kuhamishwa huyu? Ilishirikishwa katika uteuzi wa huyo mwingine? Ingefaa Makame aulizwe, na akubali kuwa wasimamizi wake wa uchaguzi ni makada wa CCM na kwamba serikali ya CCM inaweza kuwafanya wanavyotaka iwapo itaona inaelemewa sehemu fulani fulani.

  Aidha Chadema inapaswa ilalamikie hili ikiwa ni pamoja nakwenda mahakamani kupinga.

  Mbona hivi jamani – demokrasia ya akina JK ina uminywaji wa waziwazi dhidi ya upinzani ili ishinde kwa kishindo?
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Khaa this is too much jamani mbona hakuna level playing field kabisaaaaaaaaaa
  Naona kwenye katiba tuweke kifungu kuwa kampeni zianzapo ni marufuku raisi kufanya uteuzi wa aina yoyote ile ata kama mtu kafa ghafla.
  Uteuzi utafanywa baadaya raisi mpya kuapishwa PERIOD.
  Bse kwa mwendo huo ata Tendwa kiamua kukifuta chama cha CCM utashangaa anapewa 24hrs notice achape mwendo this is ridiculous kbsaaaaaaaaa.
  Nchi za Afrika tutakua lini mbona ni utoto huu.
  Pole mkurugenzi naona ata sherehe ya kukuaga haitakuwepo
   
 3. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #3
  Sep 19, 2010
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwani ni mkurugenzi wa tume ya uchaguzi????? na je anateuliwa au anareport kwa tume????
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180  Sielewi mahusiano ya Mkurugenzi mtendaji wa Jiji na ishu ya kutupa malalamiko ya masuala ya uchaguzi!
  Je anaingiaje hapa?
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  niambie msimamizi wa uchaguzi ambaye si kada wa ccm.
  mbunda ni victim wa siasa za maji taka za ccm
   
 6. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hi everyone! hope everything is fine out there.
  Nafikiri uhusiano na tume ya uchaguzi upo kwa sababu wakurugenzi ndio wasimamizi wa uchaguzi majimboni. hii lazima itakuwa order from Yusuph Makamba the great, the human being that thinks using the spinal cord and not the brain, his brain is dead long time ago tangu alipobaka mwanafunzi.
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sasa nadhani wananchi tataelewa nini maana ya tume huru!!!!!!!!!!!!
   
 8. e

  emalau JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 273
  Trophy Points: 180
  Inawezekana mkurugenzi alikataa mbinu chafu za wizi wa kura, kama bwana chang'a ameletwa kufanikisha hilo tutakula naye sahani moja. Bahati nzuri namfahamu personally huyu ndiye anayeandaa hotuba zote za wakuu wa mkoani Arusha na ni mwenyeji wa hapa Arusha, asili yake iringa. mama yake mpare baba yake mnyalukolo !
   
 9. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Country in a mess! no protocols! nina uhakika ukiamua kuuliza wajibu wa kazi zao kila kiongozi sidhani kama viongozi wetu wengi wanajua what they suppose to do! nina uhakika kwa hilo! Thank you! Mungu ibariki Tanzania na wananchi wake tunaotaabika kwa sababu ya CCM chama cha wachache
   
 10. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mmm.... its sad! Public servant should be royal to bosses. so tusilalame sana watu wanapotii mamlaka nikatika kutetea vitumbua vyao.
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hakika sisiemu wamechanganyikiwa vibaya kabisa kwelikweli ile mbaya sana mweee! Hofu ya kupoteza madaraka imetanda katika ngazi zote na sasa wameanza kutumia maguvu. Na bado tutaona mengi!!!!!!
   
 12. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  ninapojaribu kuchora picha ya watawala wengi wa kiafrika, wakiwa wameketi juu ya kiti ndani ya ofisi zenye kiyoyozi, napata shida sana ama nashindwa kuwatofautisha na nyani anayepiga dive juu ya mti wa pori lake.
  Inakuwaje mtu kugombea urais huku akiwa rais? Uwezekano wa kukubali matokeo hasi kwake sii rahisi na hii ndio sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya bara hili masikini sana duniani.
  Jamani waafrika tujichunguze kwa kukubali uhalisia wa mambo isije ikawa rangi ya ngozi yetu nyeusi inawakilisha mioyo iliyo meusi pia.
   
 13. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Na kwanini isiwe kwenye majimbo mengine kama lile la Mheshimiwa Masha?!!! Why Arusha and only Arusha wakati kuna pingamizi zingine kama hizo kwenye majimbo mengine?!
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Pengine nanihii... anataka huyo mama lazima apite kwa sababu ni nanihii.. wake!!... Simpo!
   
Loading...