Kampeni za udiwani Lwenzera: Vicent Nyerere kuongoza mashambulizi wiki ya lala salama

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,503
1,722
Mbunge wa Musoma mjini(CHADEMA) Vicent Nyerere ataongoza kampeni za kumnadi mgombea wa udiwani wa chama chake na kufunga kampeni za chadema 27-10-2012.

CCM wamezidi kupoteza mwelekeo hali iliyomulazimu mwenyekiti mteule wa ccm mkoa wa Geita na diwani wa kata ya Nzera ambayo iko jirani kabisa na Lwenzera ndugu MSUKUMA kukodi mamuluki na kuwapa kadi feki za cdm kutoka katani kwake na kuwaleta hapa Lwenzera juzi kwenye uzinduzi wa kampeni zao ambapo walifanya tendo la kurudisha kadi feki za cdm na kuchukua za ccm zilizokuwa zimeandaliwa.

Hata hivyo zoezi hili liligeuka kuwa ze comedy kwani watu wote waliorudisha kadi hizo feki wanajulikana vyema kwa wakazi wa hapa Lwenzera kuwa ni wakazi wa Nzera na hawajawahi kuwa wanachama wa chadema.


Nawasilisha
 
Wata2mia gilba nyingi sana lakini mwisho wa siku Vicent Nyerere atafanya kama alivyofanya Arumeru Mashariki.
 
Back
Top Bottom