Kampeni za Uchaguzi Zanzibar katika Picha

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
Kampeni za uchaguzi wa rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani zinaendelea kwa amani na utulivu huku vyama vya siasa vikipata fursa ya kupiga kampeni zao kwa amani na utulivu.

Pichani yanaonekana mabango ya picha za wagombea wa CCM na CUF katika eneo la soko kuu la Darajani.
Kadhalika mgombea urais wa chama cha wakulima bw. Said Soud akinadi sera zake katika viwanja vya Kombawapya, wilaya ya mjini huku wananchi wakimsikiliza. Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika baada ya wiki nne zijazo (Oktoba 31, 2010)

Picha zote ni kwa hisani ya Othman Mapara, mpiga picha wa shirika la magazeti la SMZ. Mtembelee katika blog yake: JIKUMBUKE
 

Attachments

  • kampeni zanzibar.JPG
    kampeni zanzibar.JPG
    230.6 KB · Views: 89
  • afp said soud.jpg
    afp said soud.jpg
    42.6 KB · Views: 78
  • wasikilizaji.jpg
    wasikilizaji.jpg
    67.6 KB · Views: 74
Pichani Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya NRA bw. Haji Khamis Haji(picha ya mwanzo katikati), akiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni ya chama chake, mjini Zanzibar, walioketi na bendera ni akina mama washabiki wa NRA, huku makumi ya wananchi wakiwapembeni kusikiliza sera za NRA. Anaeongea uwanjani ni Katibu Mkuu wa NRA bw. Marshed Humud. Kampeni za uchaguzi wa urais Zanzibar zinaendelea vizuri kwa vyama vyote kuanya kampeni kwa amani na utulivu.

Picha zote kwa hisani ya Othman Mapara, Mpiga picha wa shirika la magazeti ya Serikali.
 

Attachments

  • Mgombea urasi wa NRA zanzibar.JPG
    Mgombea urasi wa NRA zanzibar.JPG
    145.2 KB · Views: 49
  • wananchi wakisikiliza sera.JPG
    wananchi wakisikiliza sera.JPG
    202.1 KB · Views: 50
  • marshed Humud NRA.JPG
    marshed Humud NRA.JPG
    45 KB · Views: 54
  • akina mama wa NRA.JPG
    akina mama wa NRA.JPG
    85.6 KB · Views: 46
Hii imetulia.Sipati picha maana Zanzibar CUF bara CHADEMA inabidi tuone namna watakavyofanya kazi CUF na CHADEMA.
 
Back
Top Bottom