Kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani kuanza December 22

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,984
Baada ya mwaka mzima wa Serikali kuzuia mikutano ya hadhara, vyama vya CCM, Ukawa, ACT Wazalendo na vingine vinatarajiwa kuwasha moto kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Dimani, Zanzibar na madiwani katika kata 22 kwenye halmashauri 21 za Tanzania Bara kwa mwezi mzima.

Mbali na ubunge, mtifuano huo utafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Singida, Mwanza, Dodoma, Iringa, Manyara, Mara, Arusha, Katavi, Ruvuma, Kagera, Shinyanga, Kilimanjaro, Simiyu na Pwani.

Uchaguzi huo unatarajiwa fursa ya kwanza kwa vyama vya siasa kupata uwanja wa kufanya mikutano ya hadhara kunadi sera zao na pengine kipimo cha utawala wa Rais John Magufuli katika uongozi wa Serikali na chama tawala.

Chanzo:Mwananchi
 
Nchi ilikuwa imetulia...sasa kelele za ukawa zikianza utafikiri wanagombea URAIS...
 
Tulimis sana. Usishangae wakatuambia wanaoruhusiwa kusimama jukwaani ni wagombea tu.
 
Natamani iwe hivyo, wagombea wengi wa nyinyiem ni vilaza na huwa hawana uwezo wa kujisemea
 
Ufalme uliofitinika...sasa wanahangaika kuzima issue ya kiwanda cha saruji cha Dangote kusimamisha uzalishaji.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom