Kampeni za Ubunge ZNZ zaibua mengi, Maalim 'amuumbua' Kinana, baba amkana mwana, Lowassa na mahaba | Page 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni za Ubunge ZNZ zaibua mengi, Maalim 'amuumbua' Kinana, baba amkana mwana, Lowassa na mahaba

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by barafu, Jan 9, 2017.

 1. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 5,963
  Likes Received: 22,691
  Trophy Points: 280
  image.jpeg image.jpeg image.jpeg Nimefuatilia uzinduzi wa kampeni ktk Jimbo la Dimani kule Znz.Mkutano ulifanyika ktk uwanja wa skuli ya Fuoni.Katika machache "yaliyonivutia" ni hotuba ya Lowassa.Kwa kweli kwa hotuba tu,Mzee wangu hajambo!!Kwanza alianza na salamu...Lkn pili akamshukuru Maalim Seif kwa kumualika ktk "sherehe" hiyo hapo Dimani.2020 UKAWA andaeni hii nafasi...msirudie kosa.  Lowassa akataja idadi ya kula alizopata Znz na zile za JPM.Katika idadi yeye aliongoza,kwa hiyo akawauliza kama yeye alimshinda JPM huko Znz akiwa wa UKAWA,kwanini waseme Shein alimshinda Maalim Seif na huko ndio "ngome" ya CUF?Ukisikiliza "vigongo" vya hotuba hizi basi unaona kwanini Mzee kaamua hii mikutano isiwepo mpaka 2020.Kuna mengi sana yangetibuka.

  Maalim Seif akazibua siri,kuwa kumbe hata yale mabadiliko ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu ya chama yalifanyika bila hata Kinana kuelewa lolote;yaani hata yeye kaja kuyasikia tu mkutanoni kama vile mjumbe kutoka Wilaya ya Kalambo alivyoyasikia mlemle ukumbini Ikulu.MaalimSeif anasema

  "Kinana weee... hujui yanayoendelea ndani ya chama chako, utayajua ya nchi wewe? Ikiwa kumefanywa mabadiliko makubwa ya muundo wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu ya chama chako na pamoja na kuwa Katibu Mkuu hukuwa ukiyajua, umeyasikia vikaoni kama wajumbe wengine, utayajua ya nchi wewe?"


  Hii inastua!!Kwamba kumbe hata Kamaradi Kinana yanayoendelea ndani ya chama hayajui??Hii inaweza kuhitaji aya mpya na bandiko jipya.

  CCM waitazame Zanzibar kwa jicho la mashauriano na si kwa ubabe.Hata baba wa mgombea wa CCM jana alitoka hadharani na kusema yeye atamuunga mkono mgombea wa CUF,si kwa sababu hampendi mwanae,bali hapendi dhulma ya Chama ambacho mwanae anagombea.

  Wakati wa Ukoloni kulikuwa na msemo unasema Hence the saying: 'If the Sultan's drums sounded in Zanzibar, residents of the Great Lakes would dance to their rhythm"

  Yanapofukuta Zanzibar,bara na Maziwa makuu hutikisika...Tuyapoze ya Znz,ili tusicheze ngoma yao.
   
 2. c

  chikundi JF-Expert Member

  #81
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 7,435
  Likes Received: 1,975
  Trophy Points: 280
  Sio lazima kifungu kiseme kama amepewa dhamana ya kusimamia usalama wa nchi kama maandamano ni chanzo cha kuharibu usalama anazuia kwa kulindwa na vipengele vingine na kanuni zake kwa mfano katiba hakuna seh inayosema maandamano yanahitaji ridhaa ya polisi lkn kama chama kikiona ridhaa ya polisi inaupendeleo wowote wanatakiwa kukata rufaa ofisi ya waziri lkn haya yameelezwa kwenye kanuni zake.. Katiba ina vipengele vinavyoingiliana usikariri.
   
 3. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #82
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 6,218
  Likes Received: 4,178
  Trophy Points: 280
  Sasa mkuu ina maana kosovo ikipangwa kundi moja na serbia world cup wasishiriki???
  Ni hivi hatumkubali magufuli kuwa ni rais halali sema hayo mengine kma nilivyosema ni matakwa ya kikatiba hakuna namna ya kuyaepuka kma unataka kutumikia wananchi wako either kata halmashauri au jimbo.

  Mfano seif hta kma hamtambui shein ila akitaka kutibiwa nje lazma sign ya shein iwekwe ili apate stahiki zake sasa kma seif hamtambui kumbuka hana namna kikatiba zaidi ya kuheshim protokali kwamba shein atie saini ndio pesa itoke ila haimaanishi inamtambua kuwa mshindi halali.

  Hvi mtihani wa history ukiulizwa mwanadam alitokea wapi huwa tunajibu alianza kwa Mwenyezi Mungu au alianza kma zinjathropus?? Je ina maana kwa kuwa wwe ni mlokole au mshika dini wa kiislam utaandika mwanadam alianzia kwa Mungu ?? La hasha utajibu tu kukamilisha protokali za syllabus ya elimu dunia hta kama hutambui kuwa mwanadam alianza kma zinjathropus i hope mfano huu umeeleweka.
  Maana hii katiba yenu mbovu inampa madaraka makubwa sana rais ila kwa katiba kma ya kenya ukiamua kumsusia rais inatekelezeka kabisa maana decentralisation ni kubw akwenye katiba na mfumo wao wa uongozi wa nchi
   
 4. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #83
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 6,218
  Likes Received: 4,178
  Trophy Points: 280
  Duh mkuu uko serious??? Yaani sheria ya vyama inavunjwa wwe unafurahi??? Kwahyo mikutano kuanzia 1995 haijavunja amani afu hyo amani ikavunjwa 2016 ???? Nachotaka mmi huyo DIKTETA wenu afuate sheria unasemaje sio mizuka anayoamka nayo asbuhi trust me.kwa stahili hii 2020 atasema hakuna kampeni kupunguza gharama au atasema kampeni wiki moja tu ili kubana matumizi na nyie bado mtatetea tu......

  Sawa taratibu ila itafika siku interest zako zitaguswa ndio utaelewa kwanni tunaomkosoa tulikuwa tunamaanisha nini anapovunja sheria hku nyie mlikuwa mnashangilia kma hivi kwa kisingizio eti "ni mkuu wa nchi" sasa aliapa na katiba ili iweje?? Sasa vyama kma act vitakuwaje bila mikutano?? Niishie hapa tu ila time will tell
   
 5. c

  chikundi JF-Expert Member

  #84
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 7,435
  Likes Received: 1,975
  Trophy Points: 280
  Hajavunja katiba hata kipengele kimoja. Unashangaa mwaka 95 kuwa ok na mwaka mwingine kubadilika hata mimi nakushangaa kwa kushangaa unategemea hali ya kisiasa kuwa ya aina moja kila mwaka? Swali la kitoto sana hilo. Hata kenya uhuru kenyata alizuia maandamano ya odinga baada ya kuuwawa watu watatu japo katiba yao ambayo inasemekana ni ya tatu kwa ubora africa najua hapa kwa akili yako fupi utauliza je hapa kuna watu walikufa? Rais ni msimamizi wa amani katika nchi hivyo chochote i mean chochote completely akiona kina muelekeo wa uvunjifu wa amani anaweza kukisitisha mpk hali itakapotengemaa hata kama kitu hicho kitakuwa kina baraka za kikatiba kiasi gani.
   
 6. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #85
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 6,218
  Likes Received: 4,178
  Trophy Points: 280
  Haya kma havajunja katiba sasa sheria ya vyama vya upinzani ipo kwa ajili gani?? Bora angesema itolewe kwa vibali maalum sio kuzuia kabisa eti kigezo cha amani.... serious?? Afu cha kushangaza ameruhusu kwemye majimbo tu na wabunge wake sasa hyo amani haivunjwi kwenye majimbo yenye wabunge ila mikoa mingine ndio inavunjwa??? Ccm mmeishiwa hoja kwa kweli. Kwa hyo lema akifanya arusha mkutano hamna tishio la kuvunja amani ila akienda bahi dodoma ndio atavunja amani :D:D

  Afu Eti kuna viashiria vya kuvunjika amani hivi hyo amani kuvunjwa ni kwa wapinzani tu??? Utaskia inteligentsia imegundua uvunjifu wa amani haya wwe niambie mkutano gani wa UKAWA ulikuwa na matusi au uvunjaji wa amani?? Kuna mtu alivamia kituo cha polisi akachoma wakati wa kampeni?? Lowassa wapi kamtukana magufuli kwenye kampeni?? Huyo magufuli alitoa wapi UNABII kuwa kutatokea uvunjifu wa amani akiruhusu mikutano?? Hivi mnataka kutufanya watanzania wote ni watoto wadogo eeh mie nawaambia chuki hizi za moyoni zikikuwa mtazaa AL NUSRA front hapa tanzania na ndio mtajua kwanni libya na egypt licha ya maendeleo yote bado walipindua serikali zao na mpaka leo amani haijatengemaa tena
   
 7. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #86
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 6,218
  Likes Received: 4,178
  Trophy Points: 280
  TANGAZO LA SERIKALI NA. 215 la tarehe 12/10/2007
  SHERIA YA VYAMA VYA SIASA
  (SURA YA 258)
  -------------
  KANUNI
  (Zimetungwa chini ya fungu la 22(b))
  KANUNI ZA MAADILI YA VYAMA VYA SIASA ZA
  MWAKA 2007
  SEHEMU YA KWANZA
  UTANGULIZI
  1. Kanuni hizi zinaitwa kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa Mwaka
  2007 na zitaanza kutumika mara tu baada ya kutangazwa katika
  Gazeti la Serikali.
  2. Kanuni hizi, zitatumika Tanzania bara na vilevile Tanzania Zanzibar
  3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa pale muktadha utaelekeza vinginevyo-
  “chama cha siasa” maana yake ni chama cha siasa chenye usajili wa
  kudumu kwa mujibu wa Sheria.
  “Msajili” maana yake ni Msajili wa Vyama vya Siasa aliyeteuliwa kwa
  mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria pia itajumuisha Naibu Msajili na
  Msajili Msaidizi;
  “Sheria” maana yake ni Sheria ya Vyama vya Siasa.
  SEHEMU YA PILI
  HAKI YA CHAMA
  4.–(1) Kila chama cha siasa kitakuwa na haki zifuatazo-
  (a) Kutoa elimu ya uraia na elimu ya uchaguzi kwa wananchi kwa
  kufuata sheria na kanuni za nchi;
  (b) Kutoa maoni ya kisiasa kadri itakavyoona inafaa ili kutekeleza sera
  zake, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Katiba ya Jamhuri ya
  Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar;
  (c) Kujadili na kushindanisha sera zake na zile za chama cha siasa
  kingine kwa lengo la kutaka kukubalika na wananchi;
  (d) Kuwa na uhuru wa kutafuta kuungwa mkono na wapiga kura; na
  (e) Kila Chama cha siasa kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya
  kisiasa na maandamano kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa;
  (2) Wakati wa uchaguzi wowote utakaoendeshwa kwa mujibu wa
  Sheria ya Uchaguzi, kila chama cha siasa kitakuwa na haki na uhuru
  wa kushiriki na kushirikishwa na Tume ya Uchaguzi na au chombo
  chochote chenye mamlaka katika kufanya uchunguzi na kupata
  matokeo katika jambo au suala lolote linalohusu uchaguzi.
   
 8. c

  chikundi JF-Expert Member

  #87
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 7,435
  Likes Received: 1,975
  Trophy Points: 280
  Sheria ya vyama vingi ipo na haijavunjwa kwanini itolewe? Maandamano ya kitaifa ndiyo yenye matatizo sio ya majimbo tumia akili jimbo lina watu wangapi na jiji lina watu wangapi fikiria ukawa au chadema wakiitisha mkutano jangwani na viongozi wote wa kitaifa kuhudhuria utafanana mkutano kama huo utakaoitishwa jimbo la monduli na kuhutubiwa na mbunge wa ukawa wa monduli? Polisi haitumii unabii au utabiri fake kama wa lema kufanya shughuli zake polisi wanapambana na kuzuia uhalifu kutokana na dalili watakazoziona kulingana na mafunzo mbali mbali waliyoyapata ndani na nje ya nchi mafunzo haya yanaitwa ya kiitelijensia yaani kujua tukio kabla halijatokea ndio maana umesikia watu kadhaa wamekamatwa wakiwa wanajiandaa kwenda kufanya uhalifu.Rais anatumia vyombo vyake kupata taarifa hafanyi utabiri.
   
 9. The Mig

  The Mig Member

  #88
  Jan 10, 2017
  Joined: Jan 7, 2017
  Messages: 63
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 25
  Kama baba anaishi kwa mtoto ama anamtegemea, hapo hapatatosha. Ama pengine ataheshimu utashi wa baba ake km ambavyo asingeweza kumwingilia iwapo angehitaji kumwongezea kijana wake mama ake mwingine (mke wa pili). Nimeongea ki kufikirika fikirika kiabunuasi
   
 10. c

  chikundi JF-Expert Member

  #89
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 7,435
  Likes Received: 1,975
  Trophy Points: 280
  Huwezi kufananisha Tanzania na North African Countries hamna mwananchi mwenye sababu ya msingi ya kupindua utawala halali wa nchi hii hali kadhalika hakuna mwenye uwezo huo hata wakishawishiwa na wanasiasa wenye maono na unabii kama lema
   
 11. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #90
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 6,218
  Likes Received: 4,178
  Trophy Points: 280
  Hvi mkuu umesoma hadi level gani?? Staki kuamini kma wasomi kma nyie mnatetea ufedhuli kma huu.

  Hapo unasema vijana wa lowassa kwa mwamvuli wa LHRC ?? yaani leo hii taasisi ya TACCEO waliotumia majengo ya LHRC ndio wamekuwa vijana wa lowassa?? Ila hao hao wakileta ripoti kuhusu ukeketaji mnazikubali na kufanya warsha ila za uchaguzi hamtaki.?? Duh

  Sasa TACCEO walikuwa ofisi za LHRC na UKAWA walikuwa kijtonyama sasa hapo walikuwa wanafanya kazi eneo moja hadi muwahusishe kuwa wote ni hackers?? Kwanni unalazimisha kuunganisha matukio haya mawili wakati yametokea tofauti kabisa??

  Kuhusu january ndip aliita press conference na akaeleza wabunge walioshinda na pia akatoa matokeo eti magufuli ameshashinda wanasubiri tu NEC imtangaze hapo kumbuka ilikuwa jumanne tu hivi ina maana by 27 asbuhi NEC ilikuwa imeshamaliza kutangaza matokeo ya nchi nzima?? Mbona hakukamatwa kwa kuingilia majukumu ya NEC tofauti na maalim ni kuwa ghafala ZEC ilikataa kutangaza matokeo ya majimbo 14 yaliyosalia sasa kimya kile ndio kikanfanya maalim ajitokeze na kueleza mtanziko huo kumbuka january alikuwa hana full matokeo ya NEC kufkia 27 ila maalim alikuwa nayo ya ZEC sasa mpaka hapo kwanni maalim aliye na matokeo iwe nongwa ila january asiye kuwa na matokeo yenye muhuri wa NEC bado aliweza kutangaza ushindi wa magufuli??? Na akaachwa salama?? Huoni double standards hizi.

  Na kma kweli alikiuka sheria kwanni msimfungulue mashtaka?? Mnafuta uchaguzi afu mfanya kosa anaachwa?? Wat an excuse?? Hya maalim kajitangaza kulikoni na kufuta uchaguzi wa uwakilishi na udiwani?? Nao wawakilishi walijitangaza?? Haaaaahaaaaa ccm bhana kaz kwelikweli
   
 12. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #91
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 6,218
  Likes Received: 4,178
  Trophy Points: 280
  Sawa endeleeni na hiki kiburi kma mnafkiri kuna alietegemea kenya wangekinukisha 2007.... huo mgawanyiko visiwani hautawaacha salama wakianza mambo ya rwanda ndio mtaelewa kuwa demokrasia ni muhim zaidi ya kuwahonga wananchi khanga na madera.

  Kumbuka watu zaidi ya million 8 waliichagua UKAWA hvi kwa akili zako kwa umati kma ule wa jangwani tarehe 24 october 2015 wangeambiwa waandamane hadi ofisi za NEC nani angewazuia??? Na inngefanyika ivo nchi nzima unfkiri nni kingetokea?? Polisi mpo milion 8?? Na wale wahuni ambao hawakupiga kura ila wanaipenda chadema unafkiri kwa kupigika na maisha wasingeingia mtaani?? We jamaa usipende kuchukulia vitu kwa ulaini eti HAMNA MWENYE UWEZO HUO coz siku ikitokea hakuna atakayekuwepo na hicho kiburi tena.

  Hta Gadaffi nakumbuka alisema ana jeshi hatari zaidi africa na dunia ya kiarab hategemei vibaka wanaweza mtoa ikulu...... ila sasa hivi kabaki historia. Never underestimate the power of the masses ndugu yangu neva.... au umesahau burkina faso vibaka walizama hadi ikulu rais akakimbia bira hta raia kuwa na bunduki ila walipindua nchi kwa wingi wao tu bila kushika silaha yoyote
   
 13. makufuli

  makufuli JF-Expert Member

  #92
  Jan 10, 2017
  Joined: Jun 18, 2016
  Messages: 407
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 60
  Lowasa ni mwenyekit wa chama chetu siku hz?
   
 14. c

  chikundi JF-Expert Member

  #93
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 7,435
  Likes Received: 1,975
  Trophy Points: 280
  Wale vijana wa lowassa walikamatwa kwenye ofisi za lhrc na maeneo mengine kwanini lhrc waemploy vijana kuchakata matokeo? Wao walipewa dhamana ya kuangalia mwenendo wa uchaguzi sio kuchakata matokeo. Kutangaza idadi ya kura kwa kukusanya kutoka kwa mawakala wako sio kosa kosa ni kujitangaza mshindi ndio maana kulikuwa na mawakala kwenye vituo na vyama vyote viliruhusiwa kujumlisha matokeo ya vituo mbali mbali lkn sio kujitangazia ushindi hebu jaribu kuangalia tofauti ya kukusanya matokeo na kujumlisha na kujitangazia ushindi baada ya kukusanya matokeo hayo.

  Kuna wakati mwingine busara hutumika kwenye mambo fulani isingekaa vizuri pia ingeleta machafuko kumkamata shariff wakati ule hata kama kosa alilifanya wazi wazi kabisa jecha akatumia busara ya kufuta matokeo pekee. Uongozi sio mchezo unahitaji busara na maamuzi ya haraka wakati mwingine katiba inakuwa haijaainisha mazingira yote kwani mengine hayakufikiriwa wakati katiba kanuni au sheria inatungwa lkn yakitokea mazingira ya namna ni busara tu inatumika. Sharif hakusuburi tume itangaze alifanya makusudi akijua ccm itamkamata apate support ya vurugu lkn walimzidi ujanja hawakumgusa bali uchaguzi ukafutwa sasa anahangaika na ukosefu wa democracy ndani ya chama chake.
   
 15. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #94
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 6,218
  Likes Received: 4,178
  Trophy Points: 280
  Ila nisaidie mkuu kwanini huo UTAALAM wa intelligentsia sijawahi uskia kwenye mikutano ya ccm toka nizaliwe?? Kwanni upinzani tu?? Hilo moja.
  Pili, duh sasa inakuwaje rais akihutubia kma kule bukoba wanakujaga hta wabunge wasio wa pale na hta viongozi wa chama mkoa mbona hamsemi inteligentsia au ni kwa upinzani tu kuwa lema akimuita mbowe hali ya hewa itachafuka??
  Majaliwa akifanyaga ziara zake utakuwa kma lindi wabunge wa ccm lindi karibu wote walikuwepo sijui mwenyekiti wa ccm wilaya zote na majimbo karibu yote sasa hao wote mbona wanaenda majimbo mengine nje ya mipaka yao na wanapiga maneno sasa iweje kwa upinzani iwe nongwa???
  Mkuu inakera sana
   
 16. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #95
  Jan 10, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 5,963
  Likes Received: 22,691
  Trophy Points: 280
  Mkuu baro asante kwa changamoto
  Lkn mimi nimeleta hapa kwa ajili ya mjadala na nimeweka zote kama nukuu toka kwa hao wanasaisa na ni kwasbb jukwaa ni la kisiasa.

  Hakuna mahali nilipotia maneno yangu bali maoni...Na maoni ni haki ya msingi ya kila mtu.Haki hiyo ndio na wewe umeitumia kuweka mtazamo wako.Tuzidi kutofautiana kwa hoja
   
 17. c

  chikundi JF-Expert Member

  #96
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 7,435
  Likes Received: 1,975
  Trophy Points: 280
  Huwezi kabisa ukafananisha kenya rwanda na tz ule ugomvi wao ni wa kikabila watu walioichagua chadema sio m8 ni m6 na hawako dar tu eti wakaenda Nec halafu wakiandamana mpk nec au ikulu ndio kupindua nchi?
   
 18. c

  chikundi JF-Expert Member

  #97
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 7,435
  Likes Received: 1,975
  Trophy Points: 280
  Tanzania sio burkina faso hakuna kibaka anaweza kuingia ikulu. Mtaishia tutamwaga damu ooh mara tutafanya nchi isitawalike. Mtaishia hivyo hivyo tu
   
 19. c

  chikundi JF-Expert Member

  #98
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 7,435
  Likes Received: 1,975
  Trophy Points: 280
  Huwezi ukafananisha mikutano ya chadema/ukawa na ziara za viongozi wa serikali lkn wenye kofia za vyama vyao hata siku moja mikutano ya upinzani hamasa inaanzia kwenye mitandao ya kijamii n.k kwa lengo la kujenga chama na mkifanya mikutano yenyewe ni kejeli tupu mwanzo mwisho. Huwezi kabisa ukafananisha mikutano ya serikali hata kama wabunge wote wa ccm wangehudhuria upinzani ni vurugu tu viroba mihemko hasira za kukosa nchi n.k mkutano mmoja wa upinzani uliohamasishwa kama mlivyozoea na kuhudhuriwa na mbunge mmoja au wawili tu utakuwa na vurugu kuliko mikutano kumi ya ccm. Mna maneno ya kijinga yasiyokuwa ya kimaendeleo mtasema ndege mbovu za panga boi hazikimbii sawa na kibajaji zilimwagiwa maji wakati wa mapokezi sab zingeshika moto sab zimesafiri mwendo mrefu mara hata bus la shabiby zuri kuliko pangaboi. Badala ya kuongelea shida za wananchi na utatuzi wake. Wenyewe siasa zenu za chuki na majitaka zimeifanya intelligence ione hamfai.
   
 20. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #99
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 6,218
  Likes Received: 4,178
  Trophy Points: 280
  Haaahaaaaaa mkuu nacheka sana huku Teh Teh Teh ati jecha alitumia busara?? Haahaaaaa nmeshidnwa hata kureply Teh Teh Teh :D:D:D:D
   
 21. Muyobhyo

  Muyobhyo JF-Expert Member

  #100
  Jan 10, 2017
  Joined: Oct 9, 2014
  Messages: 6,553
  Likes Received: 4,406
  Trophy Points: 280
  kumbe hata mwaka huna jf
   
Loading...