Nicksixyo
JF-Expert Member
- Jan 11, 2011
- 944
- 263
Hii ndio kampeni ya mwamba wa kaskazini akiwa kwenye himaya yake katika kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa ndani ya mji wa Monduli. Idadi wa wananchi ndio kama uonavyo, wengi wakiwa wameletwa na malori na landrover kutoka mto wa mbu na makuyuni. Watu wanazomea kama kawa. Sare ya chama inaendelea kugawanywa kwa wasio na t-shirt za kubadilisha wanajisevia. Bodaboda zikizurura na bendera katika viunga vya mji wakijipatia kipato cha siku. Nawasilisha.