Kampeni za kutokomeza ukimwi zimeongeza idadi ya maambukizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni za kutokomeza ukimwi zimeongeza idadi ya maambukizi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by roby m, Dec 1, 2010.

 1. r

  roby m Member

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Leo tarehe 1 disemba 2010 ni siku maalumu iliyowekwa umoja mataifa
  kwa
  ajili ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ikiwa na malengo ya
  kuielimisha
  jamii juu ya janga hili zito la kimataifa kwa kuwafariji waathirika wote.
  Lakini kubwa
  ikiwa ni kutafuta suluhisho ili kutokomeza athari za janga hili ambazo
  imekuwa ni
  pamoja na kuongezeka kwa watoto yatima,pia kiwango cha umasikini
  hasa katika
  nchi zilizoko kusini mwa jangwa la sahara,mfano ripoti ya umoja wa
  mataifa ya
  mwaka 2010 imeonesha kuwa kila siku zaidi ya watoto 1000 waishio
  kusini mwa
  jangwa la sahara huambukizwa VVU.

  Ili kutatua tatizo hili asasi mbalimbali za kiraia na za kiserikali hasa
  Tanzania zimekua zikijihusisha na kampeni mbalimbali ili kuiepusha jamii na maambikizi ya ugonjwa huu,
  kwa mfano kuandaa matamasha,kutumia matangazo katika vyombo vya habari kama
  fataki,kampeni za ishi na vunja ukimya.
  Kinyume na matarajio ya wengi toka kampeni hizo zianze ndo kwanza maambukizi
  yanaongezeka kwani jamii badala ya kutishika sasa ndo wanaona ugonjwa kwa kawaida
  usishangae kuona mtoto wa kike anajisifia kwa wenzake eti aah jamani mi nina fataki langu bila kuhofia lolote.
  na ishu kubwa ni kama ISHI FEMA HIP yamekuwa vichocheo vya ngono kutokana na mambo ambayo wamekuwa wakiyaongea katika matamasha yanayoandaliwa na asasi hizo
  na pia mazingira yanakofanyika matamasha hayo ambapo mwishoni watu huishia kufanya ngono ambayo ni kinyume cha malengo na matarajio, ahsante wana JF na mnasemaje kuhusu hili......
   
 2. N

  Newvision JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Una data rafiki au unasema from no where Please give us data/takwimu. Hizi kampeni zimesaidia sana kuleta uelewa kwa watu wengi na kiwango sasa kipo kwenye declining trend tokana na taarifa ya World AIDS day ya leo kwa Tanzania. Isipokuwa kwa mikoa fulani fulani 2 sitaki kuitaja. Kwa hiyo kama kuna Effort ninayoweza kumsifu JK ni pamoja na hili na kutoa ARVs bure ambazo watu wanaishi karibu sawa tu na life expectancy ya mtu wa kawaida akifuata masharti ipasavyo! Siku hizi mtu ukipata ukimwi na akili zake ni kwamba umeuhitaji mwenyewe maana anaujua from A-Z labda tu watoto wachanga au sivyo rafiki?
   
Loading...