Kampeni za KIkwete Dodoma, Kumbe wananchi wanafuata Muziki ktk kampeni za CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni za KIkwete Dodoma, Kumbe wananchi wanafuata Muziki ktk kampeni za CCM!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by analysti, Oct 3, 2010.

 1. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 677
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  Nimehudhuria Kampeni za kikwete leo hapa Dodoma katika uwanja wa jamuhuri. Mkutano ulianza kwa wanamuziki mbali mbali kutumbuiza na wananchi wakawa wanashangilia sana.
  Baada ya muda kupita Mgombea Uraisi akapanda jukwaani kwa ajili ya kuwahutubia wananchi.

  Baada ya kupanda tu jukwaani na kuanza kuongea, watu walianza kutoka kwa wingi mno mpaka wakawa wanabanana milangoni, baadhi ya mageti yalikuwa yapo upande aliotazama mgombea, nikaona Askari wakiwazuia wanachi wasitoke na kufunga mageti yote yaliyombele ya kikwete hivyo wananchi kulazimika kutoka kwa kutumia mageti ya nyuma, hata hivyo bado wananchi waliendelea kutoka.

  Je! hii inaashiria kuwa wananchi wanafuata burudani tu ktk mikutano ya CCM, na si Sera za chama?? Au wananchi wanaona hakuna jipya la kulisikia kutoka kwa CCM, kwani wamekuwa wakiimba wimbo huohuo lakini hali za maisha za wananchi ziko duni kili kukicha????

  Pia mpaka naondoka saa kumi na mbili na nusu, alikuwa bado hajaondoka uwanjani,na miziki ilikuwa ikiendelea, hapa si ameibanjua sheria ya uchaguzi????
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,125
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Unajua watu wanavutiwa tu na zile mbwembwe za msafara wa kikwete, kumwona kikwete live (wengi wamezoea kumwona kwenye TV au magazetini an kwenye mabango ya kampeni). Wengine wanataka kuona ving'ora vile na manjonjo ya wapambe wake wanapoingia uwanjani. Kwa kuwa burudani nchini kwetu ni kitu nadra, basi music na mbwembwe ninazozisema huwa ni burudani nyingine kwa wananchi. Baada ya kuona hayo huwa hawaoni tena sababu ya kuendelea kuwepo hapo.
  Kuna uwezekano mkubwa CCM wakadhani kwamba wana watu wengi sana wa kuhudhuria mikutano yao, kumbe wengi wao ndo wale wanaokuja kuangali hizo burudani tu.
   
 3. u

  urasa JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapa manyoni watoto walikuwa wakishangaa mbwa wa usalama wa taifa,walipokuja wakina dokii wakahamia kwao,jk alijua watu hawana interest naye ndio maana akatumia dakika kumi tu kuhutubia tofauti na dr slaa iringa alitumia dak 45
   
 4. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 677
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  Hata hapa alihutubia hardly dk kumi na tano tu. Kwani wananchi walikuwa wanatoka continously!! Akahofia angekuwa akiongea mwenyewe!!
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 80,447
  Likes Received: 37,838
  Trophy Points: 280

  Mbio za sakafuni za JK sasa zimefikia ukingoniiiiiiiiiiiii
   
 6. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  pumba na mchele zishaaza kutengana, na bado tutaona majaabu mengi mwaka huu
   
 7. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,222
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  we hukujua hilo kuwa watu wanakwenda futa mzikiii!!!!!

  Na ndio maana nkawambia je watoa tathimini nani ataongoza au kuwa rais wa kwanza na nai takuwa wa pili mwaangalia wingi wa watu wajao uwanjani au?? maana wakisha maliza tu kuimba watu wanaanza tawanyika kiraiiini teh teh teh
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 145
  na wewe naye bana.... unakua kama umesahau ule waraka kwa ma-DC, mimi nadhani mwisho wake haujafika ila mwanzo wa mwisho wa CCM umewadia
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 9,809
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  Jamani huyu mtu hamjui kama ni mgonjwa??

  Akiongea zaidi ya dakika 15 sehemu moja anaporomoka
   
 10. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #10
  Oct 3, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,334
  Likes Received: 1,692
  Trophy Points: 280
  TBC manyoni wameonesha kwenye taarifa ya habari sasa hivi....ni kweli imebidi waonyeshe picha kwa mbele tu...hwakuchukua aerial view......kama ilivyokawaida......watu manyoni walikuwa wachache hadi ni aibu...aibu..

  DODOMA watu wanaonekana lakini wakati aanaongea hawajaonesha picha ya watu...
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,489
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Kinana kweli hazimtoshi.

  Mie walau ningelifanya hotuba katikati na baadaye unatangaza kuwa Miziki na Ze Comedy wenzangu wataendelea.

  Ni safi sana kwenda kuwaangalia Wasanii ila tu wote wanapendwa sana isipokuwa mmoja.

  Nafikiri anawaonea wivu akina Dokiii....
   
 12. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #12
  Oct 3, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,334
  Likes Received: 1,692
  Trophy Points: 280
  ...jk ataiba kura na kufanya ubabe...lakini kama ataingia awamu ya pili atatawala kwa taabu sana ..kwani atakuwa rais asiyeheshimika kuanzia ndani ya chama chake ....ambako wanamsubiri tu uchaguzi uishe hadi kwa wananchi wa kawaida!
   
 13. M

  Mkora JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 358
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu kwani sasa hivi anaheshimika ?
  Angekuwa anaheshimika habari zake za siri zingevuja ? Waraka kwenda kwa ma DC kuchangisha fedha uteuzi mbali mbali za mabalozi
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,596
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  sasa anahutubia 10min kwenye makao makuu ya nchi??? halafu wasanii wenzake wanaimba kwa 6hrs??
  Is this a joke or what?
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  JK kazi anayo kwanza chama kimemtenga na kuiachia familia yake kwa kampeni.Watz nao ndo ivyo wanamtosa itabidi personally nianze msupport ili angalau apate kura za kufutia machozi
   
 16. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,383
  Likes Received: 459
  Trophy Points: 180
  jamaa anshabikia muziki wa bongo flava. Anajifariki zaidi ya kuomba kura

  A hopelss looser canddate
   
 17. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #17
  Oct 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,531
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 0
  jamani jk anaitia aibu nji hii. Kapita akiomba omba dunia nzima ilihali nchi yetu ina kila aina resources ambazo zingetosha kukidhi mahitaji muhimu ya mtanzania. Matokeo yake anaacha rasilmali hapa na kwenda kyomba misaada midogomidogo km chandarua huko marekani. Duh. Awamu zote zilizopita hapakutokea presdaa bogus km hutu. Ss ni muda muafaka tumpumzishe kwa amani.
   
 18. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #18
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,763
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Jamani wa TZ tuamke, tusimpe kula huyu maana akipata tena chance ya kumalizia kipindi hiki ataiharibu hii nchi zaidi! maana naona yeye na EL wana ghadhabu ya kufa mtu na nchi itazidi kupoteza mwelekeo. Msanii huyu!!!:A S 13:
   
 19. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #19
  Oct 3, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa. Tuungane kwa pamoja tumnyime kura zetu. Halafu hivi watu wa Ingunga, Bariadi (kwa Chenge), Monduli na Rombo wamelishwa nini mpaka wakubali hata kuhudhuria mikutano ya kampeni ya wahujumu uchumi wa nchi yetu?w
   
 20. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #20
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Rombo Mramba inabidi afanye kazi ya Ziada Mkuu
   
Loading...