Kampeni za Chama cha Mapinduzi za uchaguzi mdogo wa mbunge jimbo la Siha zimeendelea kushika kasi

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,000
Jana tar. 29 Januari, 2018 Kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Siha kupitia Chama Cha Mapinduzi Dr. Godwin Mollel ziliendelea kushika kasi ambapo mgeni rasmi Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Mh. Humphrey Polepole amemnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Siha na Mgombea Udiwani. Miongoni mwa changamoto ambazo Dr. Mollel ameahidi kuzifanyia kazi mara tu atakapochaguliwa kuwa Mbunge ni migogoro ya ardhi, ukosefu wa ardhi ya kilimo na mifugo na Ndg. Polepole ameahidi kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kuwaletea Maendeleo wanaSiha na kutatua Changamoto mbalimbali zinazowakabili mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge. Wakati huohuo Mh. Polepole amewapokea wanachama wanachama wapya ambao wameikacha CHADEMA na kukabidhi kadi zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kwa madai ya kuchoshwa na propaganda nyingi ndani ya CHADEMA na kuamua kuunga mkono Juhudi za Mh. Rais Magufuli za Kuwaletea Maendeleo Watanzania.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

Robert PJN Kaseko
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha.
Januari 30, 2018.
 

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,814
2,000
Wananchi wa moshi sasa wanajitambua. CCM itashinda kwa kishindo.
 

ZigiZaga

JF-Expert Member
May 18, 2011
937
1,000
Ovyo sana wewe!polepole ni mzee au kijana? Ukinijibu hill swali nahamia chama chakavu leoleo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom