Kampeni za Bukoba mjini NEC mko wapi dhidi ya Radio ya KASIBANTE ya KAGASHEKi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni za Bukoba mjini NEC mko wapi dhidi ya Radio ya KASIBANTE ya KAGASHEKi.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kenge (Eng), Oct 11, 2010.

 1. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 502
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ndio nimeingia Bukoba jioni hii na nimebahatika kusikiliza kipindi cha kimoja ndani ya radio hii mnamo saa 3.30 usiku. kilichokuwa kinazungumzwa nimeshindwa kuelewa hasa muda wa kampeni zinaisha saa ngapi? Wakati kampeni kisheria zinaisha saa kumi na mbili radio hii inaanza kampeni dhidi ya mgombea wa CHADEMA.

  Niliyoyasikia.

  1. Lwakatare anaendesha kampeni za matusi dhidi ya mgombea wa CCM (Kagasheki).
  2. Chadema wanasema mgombea wa CUF (Kasimbazi) ni kibaraka wa CCM na amepandikizwa na Kagasheki na pale pale alihojiwa studio na kutoa msimamo wake kama kweli ni kibaraka, alichosema dhidi ya mgombea wa CHADEMA wazi alidhibitisha ukibaraka.
  3. Dai kuwa mbunge wa CCM Kagasheki alihadi madawati mia kwa shule ya msingi BUNENA na hakutekeleza, walijibu kuwa mbunge anatoa ahadi na aliyeahadiwa anatakiwa kukumbusha hivyo hakutekeleza kwa sababu DIWANi wa Bunena (CUF) hakufuatilia na shule yenyewe "wanahisi iliyakataa madawati ahyo kwa sababu ni ya Kikristu RC ndo maana hawakufuatilia. Pamoja na kuahidi shule yenyewe haikuwa na sehemu ya kuweka madawati hayo kwani misheni, RC hawahitaji madawati. Lwakatare anasema Kagasheki tapeli vipi, hana sera ni matusi tu chagua CCM.
  4. Mzungumzaji mwingine mgombea udiwani wa kata ya Nyanga (Deus) yeye alisema mgombea wa CUF ni safi na mikutano yake haina matatizo kwa CCM kwani anayoongea ni mazuri na anakiri kuwa CCM ni kiboko. Ndio maana hata hapa tunaye kudhibitisha kuwa CHADEMA hawana sera na mgombea wa CHADEMA ndio kibaraka wa CCM na kumtaka atoe maoni yake kuhusu CHADEMA. HApoooo msaada kwenye TUTA. Kutaja mapungufu na ahadi hewa zisizotekelezeka ni MATUSI.
  Redio hii inapiga kampeni za Chagua CCM, Chagua KAGASHEKI, Chagua Dkt KIKWETE ili Radio iendelee kuwapo. saa 24 hakuna kitu kingine zaidi ya kuhimiza na kutangaza ratiba za wagombea wa CCM ubunge na udiwani. Hapo maadili ya vyombo vya habari yapo?
  Redio hii imesajiliwa kisheria?
  Wataaluma nisaidie.

  HIVI tuna RADIO za Kampeni za vyama fulani na waandishi au watangazaji walio bias kwa CCM tu? Naomba kuelimishwa.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mkuu nililisikia hili pia toka Bukoba.
  Kuna rafiki yangu mmoja kanitonya kuwa wanakusanya ushahidi tu wa kiredio hiki ili wawafikishe kwenye vyombo vya sheria baadhi ya watangazaji wa Kasibante wasiofuata ethics za uandishi wa habari.
  Hata hivyo udhaifu wa NEC na bodi ya utangazaji upo wazi katika mambo kama haya ya utangazaji ovyo ovyo.
  Ninalokuomba na wewe Kenge. Ukiweza rekodi kipindi kama hicho na nitumie PM kwa hatua zaidi. Tutakomesha mchezo huu vizuri tu. Sheria lazima ziheshimiwe.
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Hiyo Redio nadhani inaita kasibante FM ni ya Kagasheki huyo jamaa wa thithiemu so usishangae!
   
 4. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 502
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sio suala la kushangaa ethics za huduma ya habari zikoje? nilipata habari nilipokuwa likizo home town BK wakati redio hii ikizinduliwa kuna watu walinieleza au kusema imezinduliwa mahususi kwa kampeni 2010 sasa yametimia. Nasubirikutoa ushahidi iwapo chombo chochote cha habari kitalalamikiwa/kushitakiwa kwa hili. Bahati mbaya sitapiga kura 31/10/2010 kwani wameshanichakachua nimepangiwa kazi za nje ya eneo langu la kupigiwa kura. Mungu ibariki TZ.
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Shawishi watu 25 kupiga kura kwa Dr Slaa na Lwakatare utakuwa ni sawa na umepiga
   
 6. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180

  "More men have been elected between Sundown and Sunup than ever were elected between Sunup and Sundown."
   
Loading...