Kampeni ya "Magufuli Baki" yaanzishwa. Yeyote atakayepinga atachukuliwa hatua

Wana wasiwasi mkubwa hata 2020 MACCM wenzie wanaweza kumpiga chini kwa ushahidi wa kutosha kabisa kwamba nchi imemshinda kabaki na sera za kukurupuka na chuki za kutisha na vitisho kila leo na kicheko chake cha kinafiki. Sijui hizi chuki za kutisha alizonazo huyu zinasababishwa na nini hasa.

Asubiri hawa watu wamalize Magufuli Baki, najuwa itafanikiwa, ingawa siyo katika maeneo yote

Lakini naamini hii ya kwangu kama haitapata upinzani Wa dola itapata wafuasi wengi. inaitwa Pombe Ondoka
kaeni mkao Wa kula
 
Wana wasiwasi mkubwa hata 2020 MACCM wenzie wanaweza kumpiga chini kwa ushahidi wa kutosha kabisa kwamba nchi imemshindwa kabaki na sera za kukurupuka na chuki za kutisha na vitisho kila leo na kicheko chake cha kinafiki. Sijui hizi chuki za kutisha alizonazo huyu zinasababishwa na nini hasa.
Nchi imemshinda Kwa vigezo gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aondoke haraka sana, atuachie nchi yetu tuiongoze kwa kufuata katiba yetu japokuwa ni mbovu...
Huyu dikteta uchwara hana hati miliki ya hili taifa, kwa mambo anayofanya ni haki kabisa apingwe kila kona!

Sent from my Diamond Crypto using JamiiForums mobile app
 
Mkuu.. Sisi watu wa kaskazini ivi soon tutadai uhuru wetu tuwe nchi kamili.

Subiri uone... Kodi zetu zinaendeshea kampeni zakipumbavu zinamlisha bashite zinajenga makanisa na misikiti chato.


Sent from my D6503 using JamiiForums mobile app



Kwahiyo isipokuwa kanda ya ziwa tu kanda zingine nazo ziwe nchi sio,

Halafu hizo zikiwa nchi na akatokea kiongozi kama yuleyule kila wilaya katika kanda hiyo inakuwa nchi tena au ?
 
Hii pombe chama cha makinikia walijua soda kumbe ni jamii ya CHANG'AA, GONGO, MTUKURU Sasa wanaanzisha ngonjera ATI GONGO IBAKI tutawakata m.a.g.ov.i
 
John-Pombe-Magufuli-750x375.jpg

Rais John Pombe Magufuli ameendelea kupongezwa na wananchi pamoja na Taasisi za kiraia mbalimbali kutokana na misimamo yake na kazi kubwa anayoifanya ya kupigania rasilimali za nchi, kwa masilahi ya wanyonge na masikini.

Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti leo, Julai 17, 2017 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Masjid Ridhwaa, Alhaj Suleiman Seif Nassor na aliyekuwa mgombea wa CCM wa Ubunge Jimbo la Sengerema kupitia kura ya maoni, Laurence Mabawa.

Wakati akizungumza na wanahabari, Alhaj Nassor amesema bodi hiyo imemamua kumpongea Dkt. Magufuli kutokana na kazi nzuri anayofanya tangu alipoingia madarakani.

Kwa upande wake Mabawa, amesema licha ya kumpongeza Rais Magufuli, ameandaa kampeni kabambe inayojulikana kama ‘Magufuli Baki’ inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni kwenye mikoa yote nchini, ambapo kupitia mikutano wananchi wenye nia njema watamuomba rais abaki katika msimamo wake wa kuwatetea wanyonge na masikini.

“Kampeni ya Magufuli Baki itahusisha mikoa yote ya Tanzania kwa kuwafikia wananchi wakiwemo wanafunzi wa sekondari kwa kufanya mikutano yenye nia njma ya kumwomba Rais abaki kwenye msimamo wake, kampeni hii itawapa fursa wananchi kutoa maoni yao kuhusu utendaji kazi wake iwe kwa kupongeza au kukosoa,” amesema.

Katika hatua nyingine, Mabawa amelaani baadhi ya wanasiasa na wananchi wanaotoa lugha za maudhi na kejeli kwa watu wanaojitokeza hadharani kumpongeza Rais Magufuli na serikali yake.

“Niombe TCRA kuwachukulia hatua kali wote wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwatolea maneno ya kejeli na kuudhi watu wanaojitokeza kumpongeza Rais,” amesema.
Nyerere amefanya mazuri mengi sana kwa nchi take zaidi ya JPM lakini hakuwahi kufanya UPUUZI huu unaoendelea sasa
 
Maskini nchi yangu,

Mbona watu wanashinikiza katiba ivunjwe hawaambiwi ni wachochezi wala sio Raisi au mamlaka yoyote ya serikali inayopiga marufuku uasi huu?
Inamaana wanaohisika kweli hawajadhani kwamba zinaweza zikajitokeza vurugu hata ndani ya chama dola?
Kwanini mnashinikiza abaki? Hebu tuambieni
Mbona Nyerere hamkumshinikiza?
Pia ninamkubali Magufuli LAKINI kwa hili la kusema ABAKI MADARAKANI ATAKAVYO sio demokrasia.

Nyie mnaosema hivyo nendeni mkaishi Zimbabwe yupo wakudumu kule
 
Ukiruhusu hiyo movement ruhusu na movement ya wanaosema asibaki. Maana yake ni kwamba mnaanzisha kampeni badala ya kufanya kazi kwa bidii! Namna Nzuri ya kufanya magufuli abaki ni kujenga viwanda, kuinua hali ya wanyonge kwa kupunguza bei ya bidhaa kama sukari na kutenda haki kwa watanzania wote bila ubaguzi wa Dini, vyama au Kabila . Haya mengine ni kutafuta sifa na kujipendekeza kwake na kujiona bora kuliko wengine!
sawa kabisa mkuu umenena

nitakuunga mkono pale utakapoacha chuki, ubaguzi na visasi
 
Na wasikukamate

Sent from my Siemens A-35 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom