Kampeni ya kuzuia harakati za uchimbaji wa madini ya uranium wilaya ya bahi.

nchasi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
564
184
Ndugu wananchi, hasa wa Wilaya BAHI ninawasihi kwamba tusije tukathubutu kuridhia uchimbaji wa madini hatari sana ya Urani kwani madhara yake huathiri vizazi vingi sana. Kuna watafiti wengi sana kutoka mataifa mbalimbali ambayo yamepewa baraka na serikali yetu kwa kuwashawishi watu wa BAHI akiwemo mkuu wa wilaya na hata mbunge wa jimbo hilo OMARI BADWEL kuwadanganya wananchi kuwa madini hayo hayana kabisa madhara kwa binadamu badala ya kuwapa elimu juu ya athari za madini hayo. Nawasihi wananchi wote ha wa maeneo ambayo madini yanatarajiwa kuchimbwa i.e ILINDI, MAKANDA, CHALI, CHIPANGA, CHIMENDELI, CHIKOLA, BAHI, na vijiji vyote kwenye peripheral tuungane kukataa na kulinda na kuelimisha watu kuhusu madhara ya madini hayo. Naamini kuna wasomi wengi mnaopata nafasi ya kuuona huu ujumbe, naomba tukatoe elimu na kulipinga hili. Vinginevyo tutakaribisha janga kwenye wilaya ya BAHI. Nawasilisha.
 
Wasivyo na shukurani wakianza kuchimba, watawahamisha wananchi bila manufaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom