Kampeni ya kutotumiwa neno "Sub-Saharan Africa" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni ya kutotumiwa neno "Sub-Saharan Africa"

Discussion in 'International Forum' started by MAMMAMIA, Mar 30, 2012.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mzaliwa wa Nigeria Chikia Onyeani ambaye ni mwenyekiti wa Celebrate Africa Group ameanzisha kampeni ya kutotumiwa kwa maneno ya Sub-Saharan Africa yanaidharau Afrika na yanapaswa kukataliwa.

  Celebrate Africa Foundation, ambayo inaongoza kampeni hiyo anasema maneno haya ni dharau na yanazibagua nchi tano za Afrika ya kaskazini zenye Waarabu na nchi nyengine zilizobakia za bara la Afrika.

  Mawazo yake yana ukweli wowote au anajitafutia umaarufu tu? Ninawaomba tuchangie hii mada.
  Kwa maelezo zaidi, bofya hapa: Campaign Launched to Drop "Sub-Saharan-African-Phrase | Africa | English

  Pia unaweza kusaini hapa kuunga mkono wazo hili: Celebrate Africa Foundation Providing Inspirational Information about Africa
   
 2. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Jamaa yuko sahihi hiyo term sub saharan africa iko very discriminative na naunga mkono ipigwe vita na iwe marufuku. Unajua inafika mahali hata wasomali hawataki kuhesabiwa kama waafrika. Kipindi cha Ghaddaffi kuna kipindi alikuwa mjumbe wa Aranb League, lakini waarabu wasipokubali mawazo yake ndipo alikuwa anageuka na kusema anatoka Africa.
   
 3. maziwa ya mgando

  maziwa ya mgando Senior Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 167
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh . . . . .
   
 4. xjamaax

  xjamaax New Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata wakichange bado watu watatafuta neno jipya.:A S-frusty2:
   
 5. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Waarabu ni wabaguzi sana na ndiyo maana hata wakati wa slave trade inasemekana walikuwa wana wa castrate wanaume wa kiafrika ambao walikuwa wanafanya kazi za nyumbani. Waliogopa kuwa wanaweza wakawazalisha wanawake wa kiarabu hivyo basi kuchafua kizazi chao. Tatizo hili halikuonekana America na ndiyo maana tunaona population kubwa ya wwusi na machotara.

  Lakini uarabuni watu weusi ni adimu kabisa na machotara hawapo. Sometimes huwa nawaonea huruma baadhi ya waswahili hasa waswalihina ambao wanapenda kupozi kama waarabu
   
 6. mtu kitu

  mtu kitu JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  @@ Huihui2 Waarabu ni wabaguzi sana na ndiyo maana hata wakati wa slave trade inasemekana walikuwa wana wa castrate wanaume wa kiafrika ambao walikuwa wanafanya kazi za nyumbani. Waliogopa kuwa wanaweza wakawazalisha wanawake wa kiarabu hivyo basi kuchafua kizazi chao. Tatizo hili halikuonekana America na ndiyo maana tunaona population kubwa ya wwusi na machotara.

  Lakini uarabuni watu weusi ni adimu kabisa na machotara hawapo. Sometimes huwa nawaonea huruma baadhi ya waswahili hasa waswalihina ambao wanapenda kupozi kama waarabu  wangu usikurupuke tu na kusema maneno bila ya kufanya uchunguzi, tizama timu ya mpira ya Saudi Arabaia, ukienda Oman hiyo Familia ya kifalme ina damu nyeusi pia kuna mji unaitwa Sur ambapo wakaazi wake karibia 70 % ni waomani weusi.(karibu kila kituo cha polisi cha Oman kina askari mwenye damu ya kiswahili)kipa wa timu ya wigan ni muomani mweusi,Imarati ndio usiseme wapo wa kumwaga.
  Ubaguzi sio waarabu tu hata wazungu wanao,hutizami mechi za mpira ? siku chache zilopita mtoto wa kingereza kamtukana Muamba.Ubaguzi upo hata kwa sisi weusi kwa weusi kwa hiyo usilete hizo.
  Usitizame upande 1 wa sarafu !!
   
 7. Achahasira

  Achahasira JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu tabia hii usishangae,maana kwenye vibaraza ndio. uongo uliopo.kuwait kuna black matajiri hadi unashangaa.saudia nimeona wabongo waliozaliwa huko na babu zao wazao wa huko.
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Matendo na maendeleo yetu ndiyo yatatufanya tusidharauliwe!malaysia walichukua mbegu ya michikichi kigoma,leo malaysia inaongoza duniani kwa kuzalisha mafuta ya mawese!kwa nini tusidharauliwe?
   
 9. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,054
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180
  Lakini lazima Afrika ya Waarabu isichanganywe na Afrika ya weusi kwa vile kwa kweli ni majimbo mawili tofauti. Kiutamaduni wametuzidi- wanaheshimu lugha yao, mila na maadili yao- kimaendeleo pia. Hata nchi maskini kabisa kama Sudan, Mauritania inashinda nchi nyingi zetu. Ukija kwenye matatizo ya magonjwa kama UKIMWI, kwao ni mchache sana kwa vile wanafuata maadili wakati sisi hatuna maadili. Kidogo walichonacho wanakitumia vizuri na kwa kweli ufisadi si jambo lililoenea. Sisi wabantu achaa tubaguliwe, nani anayetaka kuchanganywa na mbantu ambaye uongo kwake ndio ukweli, wizi ni ujanja, ngono ni maendeleo....acheni, sisi wa mwisho!
   
 10. k

  kakolo Senior Member

  #10
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  That's a fact. Utakuta wengine wana pritend as if they are not bantus.
   
 11. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ninakubaliana kwa upande mmoja na Chikia Onyeani kuhusu kudogoshwa kwa "Afrika nyeusi" kutokana na matumizi ya haya maneno, ingawa sikubaliani na wale wanaosisitiza ubaguzi wa rangi/dini na kabila, kwani mataifa hayo tajwa ya Kiarabu yana mchanganyiko wa dini na makabila yote. Ubaguzi kama upo ni silka ya binadamu kama ambavyo hapa Tanzania ubaguzi upo miiongoni mw makabila yetu wenyewe. Ubaguzi ni kitu "complicated" ambacho hakiondoki kirahisi.

  Na hata katika maelezo yake, Onyeani ametaja matatizo muhimu zaidi kwa Afrika ambayo Waafrika tunapaswa kupambana nayo, kama anavyoelezea hapa:

  But, Onyeani said Africans must fight the little wars in order to win the bigger ones.

  "There is no doubt that we have problems of poverty, we have problems of less development, we have problems of the AIDS pandemic or whatever, we have problems of corruption".

  Na kusisitiza kuwa "We can be fighting to win those wars on those other fronts, but, at the same time, we should not allow ourselves to be degraded anymore."

  Kwa hivyo, Waafrika weusi tunapaswa kupambana na kasoro zetu kama hatutaki kudharauliwa na hata "weusi wenzetu ambao si Waafrika."
   
 12. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,682
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Karibu bwana mdogo:wink2:
   
 13. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Siku moja nilikuwa nasafiri kwa gari kupitia Singida-Dodoma kuelekea Mwanza. Nilishangaa kuona huge chunks of arid land masses, nikauliza wenyeji, jamani haya ni majira au ndio kama kawa, mmoja akanambia "kuna sababu inayofanya Africa ya chini huku kuitwa "Sub-Saharan," kwa sababu al manusura Africa nzima iwe kama Sahara!
   
 14. A

  Alpha JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2012
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Sub (below) Saharan i.e. below the Sahara desert

  Strictly as a description of location, I really don't see anything wrong with this. The problem is it has become associated with poverty and ignorance due to the fact that the countries below the Sahara in Africa are the least developed and poorest countries in Africa.

  The one we should be fighting is "Third World Country"
   
 15. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Binafsi nampongeza huyu Bw. kwa kuona hili suala. Lakini pia napenda niwajulishe kuwa siyo yeye wa kwanza kuanza mjadala huu.Wapo waandhishi wengi wa Africa na wasio Waafrika ambao wameshaandika juu ya jambo hili(siwezi kumbuka majina yao hapa kwa sasa) ila yeye anatofautiana nao tu kwa maana kuwa anatumia mtandao na wakati ule mtandao haukuwepo na kama ulikuwepo accessibility yake kwa wengi ilikuwa ndogo.

  Hoja ni kwamba, haya maneno kama vile "Sub-Saharan Africa"; "Black Africans" na mengine kama LDC (Less Developed Countries), Third World Countries etc ni maneno coined na Wazungu na siyo sisi Waafrica. Sababu zao ni kuwa 1. Kuendelea kutugawa sisi Waafrika kisaikolojia na kujisikia kuwa wapo Waafrika wa Kaskazini na Kusini mwa Jangwa la Sahara na kuwa wapo Waarika Weusi na WASIO weusi (note:this is the divide and rule strategy) 2. Kutuita LDCs, Third world, developing countries etc vilevile nikumfanya Mwaafrika aendelee kujisikia MNYONGE (inferior) mbele ya Mzungu na kujiona kuwa kweli sisi ni MASKINI na ni wa DARAJA LA TATU na hivyo tunahitaji kusaidiwa na "wao" wa daraja la kwanza, aibu kweli kweli jamani!. Kiujumla kinachoendelea hapa ni MBINU ZA KUTAWALA FIKRA ZA WAAFRIKA kwa "kutu"gawa ili "wao" waendelee kututawala na kutunyonya.

  Kwahivyo mie naunga MKONO HOJA!
   
Loading...